Posts

Showing posts from February 4, 2016

DIAMOND PLATINUMS ZARI THE BOSS LADY WALA SHAVU VODACOM

Image
 Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(wapili kushoto) Balozi wa Vodacom Tanzania, Nasibu Abdul (Diamond Platinum) Kaimu Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni hiyo, Rosalynn Mworia(kulia) na Zarina Hassan(kushoto)wakionesha mabango yenye ujumbe wa jinsi ya kujiunga na Promosheni ya “Ongea Deilee”, wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo leo jijini Dar es Salaam, Itakayowawezesha wateja wa mtandao huo kuongea kwa muda wa saa 1 bure kila siku pindi wakiongea jumla ya dakika 10 Vodacom kwenda Vodacom.  Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao( kushoto) na Zarina Hassan(Kulia) wakionyeshwa tangazo la promosheni ya”Ongea Deilee” kwenye simu lililofanywa na msaanii wa muziki wakizazi kipya Abdul Nasibu”Diamond Platinum”( katikati) wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo leo jijini Dar es Salaam, Promosheni hiyo itawawezesha wateja wa mtandao huo kuongea kwa muda wa saa 1 bure kila siku pindi wakiongea jumla ya dakika 10 Vodacom k...

BREAKING NEWS : MOTO NWA MAGUFULI WATUA KINONDONI,VIGOGO WAFIKISHWA MAHAKAMANI

Image
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Kinondoni, tarehe 02/02/2016 imewafikisha washitakiwa wafuatao mahakamani:-Bw.Bryceson Kajigiri Mwangoma mwenye umri wa miaka 54, Bw.Abel Sebabil Slaa mwenye umri wa miaka 44 na Bw.Bernard Thomas Mkude mwenye umri wa miaka 42 kwa kuiibia Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni  Tsh.33,681,780. Washitakiwa hawa Bw.Mwangoma na Bw.Slaa wakiwa Maafisa watendaji wa Kata ya Kimara kwa vipindi tofauti, na Bw.Mkude akiwa Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Kimara Baruti walitenda makosa kinyume na kifungu cha 31, 22, 28 (1) 3 vya sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007 pamoja na kifungu cha 258, 270 vya sheria ya Kanuni za Adhabu. Washitakiwa wanadaiwa kutumia madaraka yao vibaya na kujipatia manufaa kwa kufanya wizi wa fedha hizo zilizokua zimewekwa na Wananchi katika akaunti ya Urasimishaji Ardhi kata ya Kimara iliyopo benki ya Wananchi wa Dar – es- Salaam (DCB) tawi la Magomeni kwa ajili ya kupimiwa maen...

Baa za Uwanjani Legho Zavunjwa

Image
Mwanadada akiwa anaangalia vitu alivyofanikiwa kuviokoa. Katapila likiendelea na kazi yake ya kubomoa . Watu mbalimbali wakiwa kwenye vikundi wakijadili tukio hilo. Eneo lililobomolewa. Nyumba hizi mbili baadaye nazo zikabomolewa. BAADHI ya baa zilizopo katika viwanja vya Legho, Ubungo jijini Dar, leo zimevunjwa kufuatia agizo la mahakama kwa kile kilichodaiwa wamiliki walivamia eneo ambalo siyo lao. Akizungumza na mwandishi wetu, dalali wa mahakama kutoka katika kampuni ya Mem Auctioneers and General Brokers Ltd, Elieza Mbwambo, alisema mmiliki halali  wa eneo hilo ni Dar Cool Makers Limited ambaye baada ya  kuvamiwa eneo lake alifungua kesi mahakamani mwaka 1993 ambapo iliendelea mpaka ilipofikia leo. Wavamizi wa eneo hilo ambao ni John Ondoro Chacha, Jumuiya ya Wazazi CCM na mtu mwingine mmoja baada ya kuona mmiliki halali amepeleka kesi mahakamani nao wakaenda kuweka zuio ambapo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliamuru eneo hilo lirudi kwa mmliki halali ambap...

Breaking News: Wachimbaji wafukiwa na kifusi, Chunya-Mbeya

Image
Hali ya taharuki kwenye eneo la tukio Tinga tinga likiendelea na juhudi za uokoaji hivi sasa. Taarifa zilizotufikia hivi punde: Wachimbaji kadhaa wa migodi (idadi yao haijafahamika) hivi punde wamefukiwa na kifusi cha udongo katika Kijiji cha Sangambi kilichopo Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya hivi sasa, Juhudi za kuwaokoa bado zinaendelea muda huu. Endelea kufuatilia habari zetu ili kufahamu kitakachojiri kuhusu tukio hilo.

BREAKING NEWZ:Ukawa Yashinda Umeya Kinondoni

Image
Hali ilivyokuwa kwenye kikao hicho cha uchaguzi wa Meya wa Kinondoni na naibu wake kilichofanyika katika Ofisi za Manispaa ya Kinondoni. Mbunge wa Jimbo la Kibamba kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika (katikati) akishiriki kikao hicho. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dk.Tulia  Ackson (katikati) akiwa amehudhuria mkutano huo wa uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Kinondoni. Wajumbe wa kikao hicho wakishiriki kupiga kura za kumtafuta Naibu Meya. Zoezi la kupiga kura likiendelea. Zoezi la kuweka kura kwenye sanduku la kupigia kura likifanyika. Wajumbe walioshiriki kupiga kura wa upande wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wakishangilia baada ya washindi kutangazwa. Kutoka kushoto ni Meya Mteule wa Kinondoni kupitia Chama Cha Demokrosia na Maendeleo (Chadema), Boniphace Jacob, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumnjuri na mwenyekiti wa usimamizi wa huo, Celestine Onditi. Meya Mteule wa...

JAJI MKUU WA KENYA AFURAHIA UTENDAJI WA MAHAKAMA YA TANZANIA.

Image
Jaji Mkuu wa Kenya Mhe. Dkt. Willy Mutunga (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuipongeza Mahakama ya Tanzania kwa utendaji wake wa kusikiliza na kuamua mashauri mengi yanayopelekwa mahakamani. Kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman na Kulia ni Jaji Kiongozi Mhe. Shaan Lila. Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akizungumzia ujio wa Jaji Mkuu wa Kenya. …………………………………………………… Na. Aron Msigwa –MAELEZO. Jaji Mkuu wa Kenya Mhe. Dkt. Willy Mutunga ameipongeza Mahakama ya Tanzania kwa utendaji wake wa kusikiliza na kuamua mashauri mengi yaliyopelekwa mahakamani kwa mwaka wa sheria uliopita wa 2015 na kutoa wito kwa watendaji wa Mahakama ya Tanzania kuendelea kufanya vizuri licha ya changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo. Jaji Mkuu wa Kenya ametoa pongezi hizo mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam mara baada ya kukutana na kuongea na Majaji wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani Tanzania kufuati...

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AWASILI MKOANI SINGIDA KWA MAANDALIZI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 39 YA CHAMA HICHO

Image
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na  Mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Vicent Kone mara baada kuwasili mkoani humo jioni ya leo,tayari kwa kuanza maandalizi ya shamra shamra za maadhimisho ya chama cha Mapinduzi (CCM) kutimiza miaka 39 Kitaifa mkoani Singida.Sherehe hizo zitakazofanyika Februari 6 2016 zinatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama hicho. Ndugu Kinana akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Singida, Said Amanzi baada ya kuwasili Singida leo,kulia kwake ni MKuu wa Mkoa wa Singida  Dk.Parseko Vicent Kone    Mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Vicent Kone sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Singida Said Amanzi wakiwa na wageni wao ,Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye mara baada kupokelewa jioni ya leo mjini humo  Mwenyeki wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Singida Bi.Diana Chilolo   samba na Mkuu wa Mk...

KATIBU MKUU, WIZARA YA NISHATI NA MADINI PROF. JUSTIN NTALIKWA AFANYA ZIARA KATIKA KISIWA CHA SONGOSONGO NA KUSHUHUDIA KAZI KUBWA YA UENDELEZAJI WA GESI ASILIA INAYOFANYWA NA PANAFRICAN ENERGY.

Image
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya PanAfrican Energy David K. Roberts (kulia) akimuelezea jambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa wakati wa ziara yake huko Songosongo katika visima vya gesi asilia.  Ni katika ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa katika visiwa vya Songosongo.   PanAfrican Energy Operational SH Engineer, Onestus Mujemula akielezea jambo kwa wana habari katika ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini huko Songosongo kwenye visima vya gesi, kutoka kushoto ni PanAfrican Energy Country Chairman Patrick Rutabanzibwa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa na CSR Manager Andrew Kashangaki (wakwanza kulia)  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa akipata maelezo ya mradi kutoka PanAfrican Energy Operational SH Engineer Onestus Mujemula kuhusu mradi wa uchimbaji gesi asilia katika visima v...

BREAKING NEWS: ZITTO KABWE AMSAMEHE MBOWE KWA YALIYOPITA.

Image