LICHA YA KUSHUTUMIWA KATIKA SAKATA LA ESCROW MUHONGO AKEMEA RUSHWA TANESCO
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Surubu, Kata ya Komaswa wakati wa ziara yake wilayani Tarime Mkoa wa Mara. Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amewataka wananchi wa vijiji vya wilayani hapa kutoa taarifa za mianya ya rushwa wakati wanapoomba kuunganishiwa umeme majumbani. Muhongo alisema hayo juzi alipokuwa akikagua awamu ya pili ya Mradi wa Umeme Vijijini unaoendelea kwa nchi nzima na ambao mkoani Mara unatekelezwa katika vijiji 197. Alisema katika mradi huo, Serikali haitamwonea huruma mfanyakazi yeyote wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) atakayebainika kuomba rushwa ili atoe huduma. “Msitoe hongo,” alisema Profesa Muhongo. “Kati ya vitu ambavyo Serikali haitaki kuvisikia ni rushwa. Msidanganywe kuwa mkitoa rushwa ndiyo mtarahisishiwa kupata umeme kwa haraka.” Alisema gharama zote za kuunganishiwa umeme kwa mwanakijiji zinalipwa na Serikali na kiasi cha Sh2...