Posts

Showing posts from September 30, 2013

Natafuta Mume wa NDOA....Nipo tayari kumpenda kwa dhati na SITAMSALITI.

Image
phars. Mimi ni binti mjasiliamali ambaye nimechoka kuishi peke yangu na sasa nahitaji mwanaume wa ndoa anayejiheshimu na anayejua kupenda.Umri wangu ni miaka 25, elimu yangu ni form six. Asilimia kubwa ya wanaume ni wasumbufu na wana wanawake wengi,kitu ambacho kwa upande wangu sikitaki maana najijua nina wivu.... Kwa yeyote mwenye sifa hasa ya kuja kuwa mume mwema ambaye atanipenda kwa dhati na hatanisaliti basi anijibu kupitia email yangu. Kwa upande wangu namhakikishia kuwa ntampenda kwa dhati, Sitamsaliti, ntamheshimu na ntawapenda ndugu na jamaa zake wote kwa moyo wangu wote. Mawasiliano: Email yangu ni nancybast4@yahoo.com   FURSA KWENU VIJANA MNAITAFUTA MCHUMBA

PICHA YETU YA LEO,"JE OFISI YAKO INA MUUNDO HUU"

Image
    FOR MORE INFORMATION LIKE OUR FACEBOOK PAGE

JE, ADHABU HII INASTAHILI KWA WATOTO?

Image
Serikali imekuwa ikipinga sana kutolewa kwa adhabu za viboko shuleni , lakini kila kunapokucha Walimu nao wanabadilisha mbinu za adhabu na kuamua kutoa adhabu kama hii kwa watoto kwa kuwalaza juani na kuwaacha hapo kwa muda pasipo kuchapwa viboko. Je,Ukiwa kama mdau wa Elimu unafikiri kutolewa kwa adhabu hizi ndio sitasaidia kukuza elimu yetu? TUPIA MAONI YAKO, NA PIA USISAHAU KULIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK

THIS IS A MOST BEATIFUL IN THE WORLD 2013.

Image
( Miss World 2013 )....Ghana washika nafasi ya tatu Mrembo wa Duinia 2013, Megan Young wa Philippines baada ya kutwaa taji hilo. Mrembo wa Duinia 2013, Megan Young (katikati) wa Philippines akiwa na mshindi wa pili Marine Lorphelin (kushoto) wa Ufaransa, na mshindi wa tatu Carranzar Naa Okailey Shooter (kulia) kutoka Ghana. Warembo mbalimbali walioshiriki shindano hilo. MREMBO wa Philippines alivishwa taji la binti mzuri zaidi duniani mwaka huu (2013) juzi huko mjini Bali, Indonesia, ambapo kulikuwa na wasiwasi kwamba Waislam wenye msimamo mkali walikuwa wamedhamiria kulivuruga tukio hilo. Mlimbwende huyo, Megan Young, mwenye umri wa miaka 23, aliyezaliwa Marekani, ambaye anachukua mafunzo ya upigaji wa filamu, alipokea taji la mashindano hayo kutoka kwa mshindi wa mwaka jana, Wenxia Yu wa China, na akaahidi kuwa “mlimbwende bora zaidi duniani ambaye hajawahi kutokea". Maelfu ya Waislam wa chama cha Islam Defenders Front waliingia mitaani t...

NORA AINGIA MATATANI MARA BAADA YA KUMCHAPA MAKOFI MHUDUMU WA HOTELI HUKO MABIBIO MARA BAADA YA KUGOMA KULIPA DENI LA TSHs. ELFU TATU...!!

Image
STAA wa filamu za Kibongo, Nuru Nassoro ‘ Nora’ anadaiwa kumzaba makofi mhudumu wa Hoteli ya Lunch Time, Mabibo, Dar aliyetajwa kwa jina la Joyce Mashika. Joyce Mashika. Katika tukio hilo lililojiri wiki iliyopita hotelini hapo, ilidaiwa kuwa kisa cha yote hayo ni kufuatia Nora kudaiwa shilingi elfu tatu za Kitanzania, deni aliloliacha kwenye gharama ya hoteli ambapo alitakiwa kulipa shiling elfu 30. Joyce aliwaambia wanahabari wetu kuwa Nora alifika hotelini hapo, akaomba chumba na alipoambiwa atoe fedha kwanza aliomba udhamini aingie hotelini kisha atalipa mpenzi wake akifika. Joyce alidai kuwa walichukua muda wa nusu saa kukubaliana naye lakini baadaye walimpigia meneja wa hoteli ambaye alikubali Nora apewe chumba. Alidai kuwa alipofika mpenzi wake ambaye ni mtu mzima, Nora alilipa shilingi elfu 20 na kuacha deni la shilingi elfu 10 aliahidi kulipa wakati anatoka. Joyce alidai kuwa usiku Nora aliagiza chakula na wakati anakilipia akampa mhudumu shilingi elfu...

ROSE NDAUKA KUJIFUNGUA BILA NDOA

Image
phars Staa wa filamu za Bongowood, Rose Ndauka ambaye ni mjamzito anadaiwa kuwa atazaa kabla ndoa mwezi Aprili, mwakani. Akizungumza na mwanahabari wetu, mchumbaa’ke, Malick Bandawe ambaye ni memba wa kundi la muziki la TNG alianika aya za Kurani kuwa katika Dini ya Kiislamu si ruhusa kufunga ndoa na mwanamke ambaye ni mjamzito kwani ni sawa na kufunga ndoa na watu wawili hivyo anamsubiri ajifungue kwanza. “Ni kweli mchumbaa’ngu hivi sasa ni mjamzito na anatarajia kujifungua mapema mwezi wanne, mwakani. “Kuhusu kufunga naye ndoa kwa sasa ni ngumu hadi ajifungue kwani kwa dini yetu (Uislam) si ruhusa kufanya hivyo lakini atakapojifungua tu tutafunga ndoa,” alisema Malick. Malick ambaye hivi sasa anatamba na Wimbo wa ‘Crazy Man’ alisema kuwa ana furaha kubwa kuitwa baba mtarajiwa na anamuomba Mwenyezi Mungu Rose ajifungue salama kwani anampenda kupita maelezo. Baada ya kuzungumza na Malick, gazeti hili lilimtafuta mama wa Rose Ndauka, Batuli kufungukia ishu ya mwanaye ...

LULU AWAONYESHA FURSA WAKAZI WA MWANZA

Image
phars  Msanii wa Filamu Bongo,Lulu akiongea jambo na wakazi wa Mwanza kwenye Semina ya Kamata Fursa Twenzetu ndani ya Ukumbi wa Golden Crista mapema hii Lulu akipokea pongezi kutoka kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mh.Steven Masele muda mfupi baada ya kushuka jukwaani kuzungumzia mambo ya Kamata Fursa Twenzetu

PHARS NYANDA BLOGGER ATOA MSAADA WA VITABU KATIKA SHULE VIZIWI DONGOBESH...

Image
  Phars akikabidhi msaada wa vitabu hivyo mbele ya Mwalimu katikati na Mwalimu Mallya kwa niaba ya Walimu wengine . Ikiwa ni Wiki ya maadhimisho ya VIZIWI Tanzania .Phars Msirikale kupitia Phars blog imeamua kutembelea shule ya Msingi DONGOBESH VIZIWI iliyoko Mkoani Manyara Wilaya ya Mbulu na kutoa msaada wa Vitabu vya Kiada na Ziada vipatavyo 147 vyenye thamani Tsh. 876,000/= kama msaada kwa watotot hao . Phars blog inapenda kutoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza kwasaidia watoto hao kwani wanayo mahitaji mbalimbali dhidi yao yanayowakabili.  The blogger akiwa na wanafunzi wakionesha vitabu ambavyo wamepelekewa kama msaada kwao  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Dongobesh Viziwi akiwa na wanafunzi wake mara baada yakupokea msaada wa vitabu  Wanafunzi wakishangilia mara baada ya kutangaziwa kuna mgeni kafika nakuwaletea zawadi ya vitabu kama wanavyoonekana hapo.  Mwalimu Rose akiwa na Mwalimu mwenzake nae akiwa na wanafunzi wake wakiangalia...