Posts

Showing posts from June 17, 2016

Wabunge wengine wasimamishwa kuhudhuria vikao leo June 17 2016

Image
Leo June 17 2016 idadi ya wabunge kusimamishwa imeongezeka baada ya Naibu Sika, Tulia Ackson kutangaza kusimamishwa kwa wabunge wawili ambao ni Mbunge wa viti Maalum CHADEMA Suzan Lyimo na Anatropia Theonest. Mbune Suzan Lyimo amesimamishwa na Bunge kuhudhuria vikao vitano vya Bunge baada ya kubainika kusema uongo kwamba Jeshi la polisi nchini limenunua magari 777 ya washawasha wakati ukweli ni kwamba hiyo ni Idadi ya magari inayopangwa kuingizwa na jeshi hilo kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Licha ya Mbunge kuonesha ushirikiano kwa kamati ya maadili, haki na madaraka ya bunge, kamati imemwona Mbunge ni mzoefu wa shughuli za bunge hivyo anapaswa kusimamishwa vikao hivyo kuanzia June 17 hadi 24 mwaka huu. Aidha Mbunge Anatropia Theonest amesimamishwa kuhudhuria vikao vitatu vya bunge kwa kosa la kulidanganya Bunge kuwa waziri wa ardhi na nyumba William Lukuvi alichukua ardhi ya wananchi akiwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.

Unawafanyia nini wazazi wako kipindi hiki wakiwa hai?

Image
Amrani Kaima A ssalam aleikum mpenzi msomaji wangu. Uhali gani wewe uliyepata bahati ya kunisoma tena wiki kupitia ukurasa huu? Ni matumaini yangu kwamba kwa rehema zake Mwenyezi Mungu umzima na unaendelea vyema na mishemishe zako za kimaisha. Mimi nitakuwa mchoyo wa shukurani kama sitatumia fursa hii kumshukuru Mungu kwa kila ambalo amekuwa akinitendea katika kila siku ya maisha yangu. Niseme tu kwamba Mungu ni mwema sana kwangu. Mpenzi msomaji wangu, najua Waislam wako katika mfungo wa Mwenzi Mtukufu wa Ramadhani na wale wanaofuatilia safu hii watakumbuka niliwahi kuzungumzia suala la kila mmoja kuiheshimu imani ya mwenzake. Asitokee hata mmoja wa kujiona yeye ni bora zaidi ya mwingine au kwamba yeye ndiye ambaye yuko kwenye mstari ulionyooka. Wote  tuko sawa na sote ni ndugu, tofauti zetu za kiimani, kikabila na kirangi zisitufanye tukafarakana. Baada ya kusema hayo nirudi sasa kwenye mada yangu ambayo nimedhamiria kukuletea kwa wiki hii. Nawazungum...

WATANZANIA WATAKIWA KUTUMIA FURSA ZA SOKO LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

Image
Na. Immaculate Makilika- MAELEZO, Tarehe 16.06.2016 WAFANYABIASHARA wa Tanzania wametakiwa kutumia fursa za biashara zinazopatikana katika soko la nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuuza bidhaa zao ndani ya Jumuiya hiyo.Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari. “Wafanyabiashara wanatakiwa kuchangamkia fursa ya biashara katika soko la pamoja kwa kuwa ni haki yao na ni utekelezaji wa malengo ya Mkataba wa uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kifungu cha tano ambapo ilianzishwa itifaki ya umoja wa forodha ” ,alisema Bi. Mindi Wafanyabiashara hao pamoja na wasafirishaji wanaotaka kufanya biashara katika soko la Jumuiya hiyo watatakiwa kuonesha cheti cha uasilia wa bidhaa wakati wakiingia nchi wananchama wa Jumuiya hasa kwa wafanyabiashara wadogo wenye bidhaa zisizozidi dola za kima...

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ALIPOKUWA AKIJIBU MASWALI BUNGENI LEO MJINI DODOMA

Image
Wabunge wa Upinzani wakitoka Bungeni baada ya dua kusomwa na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson Juni 16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali bungeni mjini Dodoma Juni 16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri .kuu) Wageni waliofika Bungeni mjini Dodoma kujionea shughuli  mbalimbali za bunge wakifuatilia kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu  Juni 16, 2016. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiteta na Mbunge wa Nkansi Kaskazini, Ally Kessy bungeni mjini Dodoma Juni16, 2016. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa zamani wa Singida mjini , Mohammed Dewji kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 16, 2016.