WATOTO WA BOSI WA FREEMASON WAFUNGUKA HAYA BAADA YA KIFO CHA BABA YAO
Takriban miezi miwili baada ya kifo cha aliyewahi kuwa Bosi wa Jamii ya Siri (Secret Society) ya Freemason kwa Afrika Mashariki, Jayantilial Andy Chande ‘Sir Chande’, aliyefariki dunia Aprili 7, mwaka huu, watoto wake wawili wamefunguka mazito juu ya jamii hiyo. Kabla ya kupata neno la watoto hao, kufuatia kifo cha Sir Andy, kumekuwa na maswali mengi juu ya nini kinaendelea kwenye jamii hiyo kwa sasa hivyo Wikienda lilijipa kazi ya kutafuta majibu ya maswali. NINI KINAENDELEA FREEMASON? Katika nusanusa yake, Wikienda lilifika kwenye Hekalu la Freemason lililopo Mtaa wa Sokoine, mkabala na Hoteli ya Hyatt Regency, The Kilimanjaro jijini Dar, jirani na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na kutaka kujua kinachoendelea kwa kujigeuza mhitaji wa kujiunga na jamii hiyo. Gazeti hili lilipofika mahali hapo mishale ya mchana, hakukuwa na pilikapilika nyingi zaidi ya mama ntilie aliyekuwa akisubiria wateja wa msosi. Baada ya kuona kimya, ‘pand...