HAMISA MOBETO KUZAA NA BWANAKE… ZARI THE BOSS LADY ATINGA BONGO KUPATA UKWELI
Zarina Hassan Tiale ‘Zari The Boss Lady’ . BAADA ya maneno mengi kusemwa Bongo kufuatia madai ya bwana’ke kuzaa na mwanamitindo mwenye jina kubwa, Hamisa Hassan Mobetto, mwanamama mjasiriamali mwenye jina kubwa Afrika Mashariki, Zarina Hassan Tiale ‘Zari The Boss Lady’ anadaiwa kuendelea kuliamsha dude baada ya kutinga Bongo na kuanza kudodosa ili kupata ukweli wa ishu hiyo. Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho ni makini, awali Zari alitinga Bongo mapema wiki iliyopita na kupigwa chabo na ‘wadakuz’ AKIWA KATakiwa nyumbani kwa jamaa huyo ambaye ni msanii wa Bongo Fleva huko Madale jijini Dar. Akiwa katika pozi. Ilidaiwa kwamba, hata hivyo, hakukaa sana kwani aliondoka kwenda kwenye kumbukumbu ya siku 40 za kifo cha mama yake, Halima Hassan nchini Uganda kabla ya kurejea Bongo wikiendi iliyopita. Kwa taarifa yenu Zari amejaa tele Bongo na lengo lake n...