Posts

Showing posts from January 9, 2015

ANGALIA PICHA VICTOR VALDES ATAMBULISHWA RASMI MANCHESTER UNITED

Image
Victor Valdes ametambulishwa rasmi kama mchezaji wa Manchester United ambapo kipa huyo wa zamani wa Barcelona amesema ana furaha kubwa kujinga na Mashetani Wekundu, timu yenye mvuto wa aina yake. Valdes mwenye umri wa miaka 32, amesaini mkataba wa miezi 18 huku kukiwa na kipengele kinachoweza kurefusha mkataba huo kwa mwaka mmoja zaidi. “Kwa mara ya kwanza nilipokuja hapa kwenye uwanja wa mazoezi - Aon Training Complex, nikaona maandishi makubwa mekundu ya Manchester United.  “Kwangu mimi ilikuwa kama njozi. Nimecheza Barcelona kwa miaka mingi, ni klabu kubwa na niliipenda kwa maisha yangu yote. “Nadhani hali hiyo imejirudia tena hapa. United ni klabu kubwa duniani na ina mashabiki wengi kila kona. “Nilifanya kazi na Louis van Gaal FC Barcelona. Kupata nafasi ya kufanya naye kazi tena hapa Manchester United, ni njozi iliyotimia,” alisema Victor Valdes.

PICHA ZA MKUTANO WA CHADEMA MKOANI MBEYA

Image
  Kabla ya kuelekea kwenye mkutano   Njiani msafara wa Mh. Mbilinyi ukielekea kwenye mkutano  Prof. Jay akizungumza na waandishi wa habari  Kutoka kushoto, Prof Jay, Mh. Mbilinyi na Msigwa  Prof. Jay akizungumza na wana Mbeya  Mh. Msigwa akizingmza na wana Mbeya  Juu na chini ni aliye vaa kimasai ni makamu mwenyekiti BAVICHA  

JK AMUAPISHA MSAJILI MAHAKAMA YA RUFANI TANZANIA, NI KATARINA REVOCATI

Image
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha, Katarina Revocati (Kulia), kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Alhamisi Januari 8, 2015 Rais akimkabidhi Katiba Rais akimpongeza Majaji wakibadilishana mawazo Majaji wakibadilishana mawazo Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman (Kulia), akizungumza na Waziri wa Sheria na Katiba, Dkt. Asha Rose Migiro wakatiwa hafla hiyo ya kumuapisha Katarina Rais akisalimianana Jaji Mkuu Mohammed Chande Othman Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi maalum), Profesa Mark Mwandosya, (Wapili kushoto), akiwa na majaji kwenye hafla hiyo picha ya pamoja Rais na familia ya Katarina Revocati Rais katika picha ya pamoja kutoka kushoto, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, Jaji Mkuu, Mohammed Chande Othman, Msajili wa Mahakama ya Rufani, Katarina Revocati, Waziri wa Sheria na Katiba, Dkt. Asha Rose Migiro, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju

YAYA TOURE NDIYO MBABE WA SOKA AFRIKA KWA MARA YA NNE

Image
Yaya Toure kiungo wa timu ya Manchester City Yaya Toure amekuwa mchezaji wa kwanza kutajwa na shirikisho la soka barani Afrika kuwa mchezaji bora wa mwaka kwa mwaka wanne mfululizo. Toure ana umri wa miaka 31,aliteuliwa baada ya kucheza kwa kujitoa na kuleta ushindi katika Premier League na League Cup, na pia alijitoa kuisaidia Ivory Coast kuingia katika kombe la mataifa ya Africa yatakayo fanyika baadaye mwaka huu. Toure amewapiku mshambuliaji kutoka Gabon, Pierre Emerick Aubameyang na golikipa mnigeria Vicent Enyeama.Toure pia alikwaa tuzo ya FIfa ya Ballon D'Or mwezi wa kumi mwaka wa jana..

Kenge 149 wanaswa Uwanja wa Ndege Dar Wakitoroshwa nje

Image
Jeshi la Polisi la   Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)linamshikilia raia wa Kuwait kwa tuhuma za kukutwa na viumbe hai aina ya Kenge 149 wenye thamani ya Sh 6.3 milioni.   Kamanda wa Polisi wa JNIA, Khamis Suleiman alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Hussain Ahmed Ally Mansour(34), raia wa Kuwait ambaye alikamatwa uwanjani hapo jana  majira ya saa 5 usiku wakati akijiandaa  na safari ya  kuelekea nchini Kuwait  kupitia Dubai  na Shirika la Ndege la Emirates  .   Kamanda  Selemani alisema Mansour alikamatwa na wanyama hao ambao aliwahifadhi  kwenye mifuko midogo midogo ilivyowekwa katika begi kubwa lenye rangi nyeusi.   “Kenge waliwekwa kwenye mifuko midogo midogo 15 na kila mmoja kuna kenge 15 na mifuko mingine walikaa wawili,” alisema kamanda Selemani.   Alisema kati ya Kenge hao, 15 walikufa na walio hai walikuwa 134 ambao  walikuwa wamefichwa kwenye mifuko hiyo....

Penzi Kinyume na Maumbile Lamtesa Lungi

Image
  Msanii wa filamu za Kibongo, Lungi Maulanga, amesema kuwa mpenzi wake amekuwa akimsaliti kila kukicha huku akihisi kuwa, huenda wanawake anaowafuata huko nje wanampa mapenzi kinyume na maumbile.   Akizungumza Gpl Lungi alisema kuwa siku chache zilizopita alilia sana kutokana na usaliti aliofanyiwa na mpenzi wake aliyemhifadhi kwa jina, akasema aliamua kumsamehe kwa kuwa anampenda.    “Naumia sana na nalia kila ninapokumbuka namna mpenzi wangu anavyonisaliti, sielewi ni kwa nini wakati mimi ni mrembo na nina umbo zuri ambalo kila mwanaume akiniona lazima anitamani.   “Nashangaa mwenzangu anavyochepuka, sijui huko nje anawafuata wale wanaotoa ‘mtandao’?” alihoji Lungi na kuongeza: “Mimi siwezi kumsaliti hata iweje, najua huko nje magonjwa ni mengi.”

PICHA NA VIDEO DIAMOND PLUTNUMZ NA P SQUARE NDIO WALIO FANIKIWA KUWATEKA HISIA MASHABIKI TUZO ZA GloCafAwards‬

Image
Wasanii wa Africa walipata nafasi yakutoa burudani katika tuzo hizo za  GloCafAwards‬    ‪ kama Uhuru Mr lavour Uhuru ,soweto gospel choir na wengineo Lakini Watu Waliguswa na Nyimbo ya diamond mdogo My Number one remix ambayo Plutnmz alionyesha uwezo wakuimba ubeti wa Davido Wote Bila yakufwata Cd Back Play nakufanya vizuri P square walifanikiwa kuwa kosha masbabiki baada ya kuimba nyimbo mbili Test MOney Na Ejajo 

YANGA YACHEZEA KIRUNGU NA KUTUPWA NJE KOMBE LA MAPINDUZI

Image
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar YANGA SC imetupwa nje ya kombe la Mapinduzi 2015 kufuatia kutandikwa bao 1-0 dhidi ya JKU katika mechi ya mwisho ya robo fainali iliyomalizika uwanja wa Amaan usiku huu. Bao pekee la Amour Omar ‘Janja’ lililofungwa katika dakika ya 72 limetosha kuwatumbukiza Wanajeshi hao katika hatua ya nusu fainali. Kipindi cha kwanza timu zote ziliuanza mchezo kwa makani na kupata nafasi kadhaa za kufunga, lakini washambuliaji wa timu zote hawakuwa makini. Yanga walianza kwa kutawala mchezo huo wakipigiana pasi za uhakika kuanzia katikati, lakini hesabu zao hazikuwa nzuri kila walipofika eneo la hatari la wapinzani wao. Dakika ya 24 kipindi cha kwanza, Amiss Tambwe aliendeleza maajabu yake ya kukosa mabao ya wazi katika michuano ya kombe la mapinduzi kwani alipata nafasi nzuri ya kufunga kufuatia mabeki wa JKU kuchanganyana na kipa wao Mohammed Abdallah, lakini Mrundi huyo alipiga mpira nje. Dakika ya 35 kwa mara nyingine tena Tambwe ...
Image
Baada ya Kupiga Show ya Nguvu Nigeria usiku wa leo, Diamond kasema haamini Macho yake 1/09/2015   habari za kitaifa   Staa Afrika Mashariki, Nasibu Abdul ‘Diamond’, amefunguka kwamba haamini kama kweli amepata nafasi ya kutumbuiza kwenye sherehe za utoaji tuzo za wanamichezo bora zilizoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ambazo zimefanyika usiku wa kuamkia leo jijini, Lagos, Nigeria.   Akizungumza na Mpekuzi, Diamond amesema amefurahi kupata nafasi ya pekee ambayo mara nyingi hutolewa kwa wasanii wakubwa Marekani na kuamini kwamba muziki wa Tanzania unathaminika kila kona.   “Nimefurahi maana hii inaonyesha jinsi gani muziki wetu umekuwa hadi kufikia Afrika kuwa moja ya kionjo hasa kwenye tamasha kubwa kama hilo, kiukweli sikuwahi kufikiria hapo mwanzo,” alisema Diamond.