Posts

Showing posts from June 21, 2017

Kauli ya Yanga Kuhusu Kuondoka kwa Niyonzima

Image
TAARIFA KWA UMMA ​ Yanga SC kupitia kwa Katibu Mkuu Boniface Mkwasa inapenda kuwajulisha wanachama, wapenzi na washabiki wa Yanga juu Mchezaji raia wa Rwanda Haruna Niyonzima ambaye amekua Mchezaji wetu kwa misimu 6 mfululizo katika kiwango cha juu. Hata hivyo Haruna Niyonzima bado ana mkataba mpaka mwezi Julai na Yanga Sc, lakini hatutaweza kuendelea kuwa nae kwa msimu ujao kwani hatukuweza kufikia mwafaka katika mazungumzo yetu na yeye licha ya timu yetu kuwa na nia za kuendelea nae kwa misimu miwili ijayo. Klabu inamtakia kila la kheri katika maisha yake na soka kwa ujumla. Imetolewa na Idara ya Habari na Maelezo Young Africans Sports club. 21-06-2017.

Hii ndio Sababu ya Wabunge wa Upinzani Kumsusia Spika Ndugai Futari

Image
WABUNGE wa kambi ya upinzani bungeni, jana waliamua kumsusia futari, Spika wa Bunge, Job Ndugai, Taarifa kutoka kiongozi mmoja mwandamizi kutoka ndani ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) zinasema, uamuzi wa wabunge hao kususia futari umetokana na madai kuwa Spika amekuwa akiendesha Bunge kwa upendeleo. Hoja ya kususia futari iliwasilisha kwenye kikao kilichofanyika jana kabla ya Bunge kukutana kupitisha bajeti. “Tulikutana jana na tukakubaliana kwa kauli moja kususia futari hiyo. Hatuwezi kushirikiana na watu wanaotubagua waziwazi,” ameeleza mbunge mmoja wa Ukawa aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina. Habari zinasema, mbali na mkakati huo, Ukawa umejipanga kukabiliana na serikali hasa kutokana na kauli kuwa “wabunge waliopinga bajeti wanyimwe fedha za maendeleo.”

Sherehe ya kula nyama ya mbwa Ilivyofanyika China

Image
Sherehe ya kula nyama ya mbwa iliogubikwa na utata katika mji wa Yullin nchini China imeanza licha ya ripoti za awali kwamba ilikuwa imepigwa marufuku mwaka huu. Sherehe hiyo hufanyika kila mwaka katika mkoa wa Guangxi. Mapema mwaka huu ,wanaharakati walidai kwamba wafanyibiashara waliagizwa na mamlaka kutouza nyama ya mbwa. Lakini wamiliki wa vibanda vinavyouza nyama hiyo waliambia BBC hawajasikia lolote kuhusu hatua hiyo kutoka kwa maafisa. Mnamo tarehe 15 mwezi Mei, maafisa wa mji walithibitisha kwamba hakuna marufuku yoyote. Siku ya Jumatano, ripoti kutoka Yullin zilisema kuwa mbwa waliokufa walionekana wakiwa wametundikwa katika ndoano za nyama katika vibanda ndani ya soko la Dongkou ambalo ndio kubwa mjini humo. Mwanaharakati mmoja aliambia BBC kwamba alikatazwa na maafisa wa polisi kuingia katika soko la Dashichang ambapo inaaminika mbwa walikuwa wanauzwa. Katika sherehe za miaka ya nyuma kumekuwa na mzozo kati ya wauzaji nyama ya

MSANII JINI KABULA ALAZWA MUHUIMBILI

Image
Staa wa filamu za Kibongo, Miriamu Jolwa ‘Jini Kabula’. Nasikitisha!  Staa wa filamu za Kibongo, Miriamu Jolwa ‘Jini Kabula’ anadaiwa kudata ‘kuchanganyikiwa’ na hivi sasa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako anapatiwa matibabu,  Risasi Mchanganyiko  limetonywa. Chanzo makini kilicho karibu na msanii huyo kililiambia  Risasi Mchanganyiko  kuwa mwanamama huyo alikuwa kwa rafiki yake ambaye pia ni msanii wa filamu, Esha Buheti kabla ya hali yake kuanza kubadilika na kuzungumza mambo yasiyoeleweka. “Jini Kabula amechanganyikiwa kabisa yaani, kwani alikuwa kwa rafiki yake huyo, ndipo alipoanzia kuumwa ikabidi ndugu zake wamchukue na kumpeleka Muhimbili ambako mpaka sasa anaendelea na matibabu. “Ukimuona anakutambua, lakini anayoyaongea hayaeleweki, ni kwamba amedata kabisa licha ya kwamba kama alikuwa anakufahamu awali hata sasa akikuona anakutambua, lakini ndiyo hivyo anaongea vitu mchanganyi-kochan-ganyiko, ukweli anatia huruma sana,” kilis

Upinzani Wampeleka Spika Ndugai Mahakamani

Image
Wabunge Watatu Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo Chadema Wamemfungua Mashitaka Mahakama Kuu Ya Dodoma Kupinga Uamuzi Wa Bunge Kuwapa Adhabu Halima Mdee, Estar Bulaya Na John Mnyika . Mdee, Mnyika Na Bulaya Wawashitaki Spika Na Mwanasheria Mkuu Hakuna kanuni inayosema Spika anao owezo wa kumfungia Mbunge siku saba. Haipo, bali anaingiza kanuni zake mwenyewe kutoka kichwani mwake.

RC ANNA MGHWIRA AMKALIA KOONI FREEMAN MBOWE

Image
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amesema kuwa hatua zilizochukuliwa na Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gellasius Byakanwa za kuondoa miundombinu ya umwagiliaji katika shamba la Kilimanjaro Veggies si za kisiasa bali ni taratibu za kisheria za kulinda vyanzo vya maji. Mghwira alitoa kauli hiyo jana alipotembelea shamba hilo lililopo Kijiji cha Nshara ili kujionea hali ya uharibifu wa mazingira uliofanywa katika shamba hilo linalomilikiwa na Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe. “Sheria iko wazi, inasema tusifanye shughuli zozote za kibinadamu zenye madhara kwenye vyanzo vya maji ndani ya mita 60 kwa mujibu wa sheria na shughuli hii ina madhara makubwa kwa mazingira na hata kwa binadamu,” alisema Mghwira. “Shughuli hii nzuri na ni uwekezaji mkubwa. Ninavyofahamu kilimo cha strawberry kikishatema maji lazima yaende mahali hata kama unatumia umwagiliaji wa kisasa wa matone. Maji yanakuwa na madhara kwa binadamu wanayoyatumia.” Mghwira alisema k

Rais Magufuli atuma rambirambi kifo cha Ali Yanga

Image
Rais John Magufuli ametuma rambirambi kwa familia, wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), uongozi wa Klabu ya Yanga na wanamichezo wote kwa jumla kutokana na kifo cha shabiki wa Klabu ya Yanga, Ali Mohamed maarufu Ali Yanga. Ali Yanga amefariki dunia jana (Jumanne), Juni 20 kwa ajali ya gari iliyotokea katika Kijiji cha Chipogolo wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma. Taarifa iliyotolewa leo (Jumatano) na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa imemkariri Rais Magufuli akisema atamkumbuka Ali Yanga kwa uzalendo na mchango wake wa kuhamasisha na kushabikia masuala mbalimbali ya kitaifa na hasa michezo, ikiwamo kuishabikia timu yake ya Yanga, timu ya soka ya Taifa, CCM  na shughuli za kiserikali kama vile Mwenge wa Uhuru na ziara za viongozi. “Nimeguswa sana na kifo cha Ali Yanga, nilikuwa naye wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na alitoa mchango mkubwa katika uhamasishaji wa wananchi kukipigia kura chama changu cha CCM, pia amekuwa akiong