Lowassa, Sumaye Hatarini Kushtakiwa
KAMISHNA wa Sekretarieti ya Maadili kwa Viongozi wa Umma, Jaji mstaafu Salome Kaganda, amewataka viongozi wastaafu kuacha kutoa siri za serikali kwani bado wapo kwenye kiapo na kuonya wakikaidi, watachukuliwa hatua. Bila kuwataja kwa majina wala siri walizotoa, Jaji Kaganda alisema: “Tusiweke maslahi binafsi mbele kwa kutoa siri za mikataba kwa kuangalia manufaa binafsi, jambo ambalo limelifikisha taifa pabaya. Viongozi wastaafu wafunge midomo yao kwani bado wako ndani ya kiapo hata kama wamestaafu.” Waziri mstaafu, Frederick Sumaye. Jaji Kaganda alisema wapo wastaafu ambao wameingia kwenye nyanja mbalimbali ikiwamo siasa, ambapo hutumia majukwaa kutoa siri za serikali na kwamba wanapaswa kukumbuka wanaweza kuchukuliwa hatua za kisheria. Jaji Kaganda aliyasema hayo juzi alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na Kituo cha Runinga cha ITV. Kwa siku za karibuni, mbali na watumishi wa umma walioacha kazi zao na kushiriki siasa ikiwa ni pamoja na ku...