Posts

Showing posts from February 10, 2017

RAIS JOHN MAGUFULI LEO AMEMTEUA ROGERS W. SIANGA KUWA KAMISHNA MKUU WA MAMLAKA YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA.

Image

MAKAMU WA RAIS AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI MJINI DODOMA LEO

Image
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma leo.   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipitia baadhi ya ajenda wakati  kikao cha Baraza la Mawaziri mjini Dodoma.  Mawaziri wakijadiliana jambo kabla kikao cha Baraza la Mawaziri hakijaanza kutoka kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage. Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba(kushoto), Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (katikati) wakizungumza jambo na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango muda mfupi kabla ya kuanza kikao cha Baraza la Mawaziri mjini Dodoma. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Ma

UPDATES: IDD AZZAN AWASILI KITUO CHA POLISI CHA KATI KWA AJILI YA MAHOJIANO

Image
Mbunge wa zamani wa Kinondoni, Iddy Azzan ameripoti katika kituo cha polisi cha kati kama aliyotakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Azzan amewasili kituoni hapo muda wa saa 09:06 kwaajili ya mahojiano na polisi baada ya kutakiwa kufanya hivyo na mkuu wa mkoa. Azzan ni miongoni mwa watu 65 waliotajwa na mkuu wa mkoa juzi kutakiwa kufika polisi jijini Dar es Salaam. Jana. Askofu wa kanisa la ufufuo uzima Josephat Gwajima na mfanyabiashara maarufu, Yusuf Manji ambao nao wapo katika orodha hiyo ya mkuu wa mkoa waliripoti.Kamanda wa Kanda Maalumu, Simon Sirro amesema ifikikapo saa 7 mchana atazungumza na waandishi wa habari.

FREEMAN MBOWE AGOMA KWENDA KUHOJIWA POLISI ASEMA MAKONDA HANA MAMLAKA HAYO

Image
Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Aikaeli Mbowe amesema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda hana mamlaka ya kumuita kwenda Kituo cha Polisi.  Mbowe ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Mjini Dodoma kufuatia kutajwa katika orodha ya watuhumiwa 65 wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya na kutakiwa kufika Kituo cha Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam leo saa tano asubuhi. Mbowe amekanusha vikali tuhuma hizo za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na kusema kuwa anachokifanya RC Makonda ni kuwaepusha watuhumiwa wa kweli wa dawa za kulevya na mikononi mwa sheria. Aidha, Mbowe amesema kuwa yupo tayari kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi muda wowote endapo njia sahihi zitakapofuatwa.  Pia amesema atamfungulia mashtaka RC Paul Makonda kwa kumchafulia jina lake kufuatia kumtuhumu kwa biashara ya dawa za kulevya. Kiongozi huyo wa Kambi ya Upinzani Bungeni a

Jeshi la Polisi Dar Lamjibu Mbowe……Lasema Kama Hataripoti Polisi, Basi Litamfuata Popote Alipo.

Image
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema kama Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe hataripoti bila kutoa taarifa yoyote ya udhuru atafuatwa kwa kuwa jeshi hilo linahitaji  kumhoji. Kamanda wa kanda hiyo, Simon Sirro amesema hayo leo muda mfupi baada ya Mbowe kueleza kuwa hataripoti polisi kutokana na wito wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Amesema operesheni dhidi ya mihadarati bado inaendelea na kuanzia sasa hawataruhusu tena mkusanyiko wa watu katika kituo cha polisi kati na wale watakaoonekana watashughulikiwa hivyo asije kulalamika mtu kwani taarifa imeshatolewa. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ametangaza rasmi kutofika kituoni hapo kwa madai kuwa hawezi kwenda polisi kwa wito wa Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda isipokuwa pale tu taratibu za kisheria zitakapofuatwa.

STAA WEMA SEPETU KUONANA USO KWA USO NA ZARI THE BOSS LADY

Image
Akizungumza live kutoka Clouds Fm, Diamond ametamka rasmi kuwa staa Wema Sepetu ni miongoni mwa wageni waalikwa kwenye sherehe hiyo, kwa upande wa Zari Hassan nae amesema hana shida na ujio wa Wema Sepetu Kwenye Arobaini ya Nillan ambaye waliwahi kuingia kwenye bifu kipindi cha nyuma. Kama kweli Wema akifanikiwa kuhudhuria kwenye sherehe hiyo itakua ndo mara ya kwanza kwa mafahari hao wawili kuonana, na itakua sherehe ya aina yake kwa uwepo wa mastaa hao waliowahi kuingia kwenye vita nzito na kurushiana maneno mtandaoni

MUME AMKATA MASIKIO MKE WAKE, SABABU YATAJWA KUWA AMEMCHOKA

Image
Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Zarina mkazi wa mji wa Balkh, Afghanistan amekatwa masikio na mume wake kwa madai kuwa mume wake amemchoka na hataki kuishi nae. Akielezea tukio hilo la kikatili, Zarina alisema amedumu na mwanaume huyo kwa muda wa miaka saba na tukio hilo lilitokea wakati akiwa amelala usiku lakini ghafla aliamka na kukuta akifanyiwa tukio hilo.“Sikuwa nimemfanyia jambo lolote baya, sijui kwanini mme wangu alinifanyia hivi … mahusiano yetu hayakuwa mazuri,” alisema Zarina.Mwanamke huyo mwenye miaka 21 aliongeza kuwa mume wake amekuwa akimfanyia vitendo vya kikatili kwani kuna kipindi alimzuia hata kwenda kuwatembelea wazazi wake.Aidha Zarina alizungumza kuhusu mpango wake wa baadae kama ataendelea kuishi na mwanaume huyo na kusema, “Sihitaji tena kuishi nae.” Zarina kwasasa anapatiwa matibabu katika moja ya hospitali iliyopo Balkh na Polisi mjini humo wamesema mume wake amekimbia na juhudi za kumtafuta zinafanyika ili hatua za kisher