Posts

Showing posts from March 31, 2016

Rais Zuma apewa siku 105 kurejesha fedha za umma alizotumia kukarabati makazi yake

Image
Mahakama ya Kikatiba nchini Afrika ya Kusini imemuamuru Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma ndani ya siku105 awe amerejesha serikalini dola milioni 16 fedha za walipakodi ambazo alizitumia kukarabati makazi yake binafsi. Mahakama hiyo imesema Rais Zuma mwenye umri wa miaka 73 alikataa kutii agizo kutoka kwa ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu mwaka 2014 la kumtaka alipe fedha hizo zilizotumika kuifanyia ukarabati nyumba yake ya kibinafsi. Jopo la Majaji 11 wa Mahakama hiyo ya Kikatiba ya nchini Afrika ya Kusini limesema Rais Zuma alikiuka Katiba ya nchi hiyo kwa kutumia fedha hizo katika ukarabati wa nyumba yake hiyo ambayo ipo eneo la nkandla -kwazulu-natal na kuhitimisha miaka 6 ya sakata hilo. Chama cha siasa cha Democratic Alliance cha nchini humo  kimeanzisha kampeni ya kumuondoa Rais zuma madarakani baada ya mahakama ya kikatiba kutoa uamuzi kuwa alikiuka Katiba. Vyama viwili vya upinzani viliwasilisha kesi hiyo mahakamani ili kumlazimisha Rais Zuma kuzingatia...

MCHUNGAJI APOTEZA WATOTO WANNE KATIKA AJALI YEYE NA MKEWE WASALIMIKA

Image
Kama kuna jambo limefichwa usoni pa wanadamu ni Kifo, tungelijua sijui tungekuwa na aina gani ya Maisha... Labda tusingesoma, labda tusingejenga nyumba, labda tusingeoa na kuolewa, labda tusingezaa watoto na yamkini tusingenunua magari wala kusafiri kwa kutumia magari hayo...inabaki kuwa fumbo! Jana imekuwa siku ngumu na mbaya ambayo itabaki kuwa kovu kwa maisha yote kwa mchungaji Pastory Michael Kajembe ambaye ni mchungaji wa TAG-Ebenezer (Dodoma) Mwanataaluma mahiri wa Theolojia, na Mwalimu wa Chuo cha Biblia Dodoma (Central Bible College, zamani AGBC) na familia yake,Kanisa la TAG kwa ujumla, ndugu jamaa na marafiki... Baada ya kupata Ajali ya Gari akiwa na familia yake, jana alfajiri katikati ya Mtera na Mpunguzi, Mkoani Dodoma na Kupoteza Watoto wake Wanne kwa pamoja Junior, Isaac, Gabriel na Glady katika ajali hiyo. Mchungaji Pastory Kajembe na Mama, Bwana amewaponya,bado wanahitaji maombi maana nao wamepatwa na Majeraha na wanaendelea na matibabu. B...

Breaking News!! LEMBELI APIGWA CHINI KESI YA UBUNGE KAHAMA

Image
Habari tulizozipata hivi punde kutoka Kahama mkoani Shinyanga ni kwamba aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Kahama James Lembeli(Chadema) ameshindwa katika kesi ya Ubunge jimbo la Kahama iliyokuwa inaendelea mahakamani. Lembeli alikuwa amefungua kesi kupinga ushindi wa Jumanne Kishimba ambaye sasa ni mbunge wa jimbo la Kahama kwa tiketi ya CCM. ...Taarifa kamili tutawaletea hivi punde...

WATANZANIA KUNUFAIKA NA BIMA YA ELIMU KUTOKA SANLAM LIFE INSURANCE TANZANIA

Image
Meneja Mkuu wa Bima ya Maisha, Wilson Mnzava (wapili kulia), wakati wa uzinduzi wa bima hiyo.Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life Insurance, Julius Magabe na kulia ni Mchambuzi wa Mahesabu ya Bima wa kampuni hiyo, Kyenekiki Kyando.  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life Insurance, Julius Magabe, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bima ya Elimu ya 'Sanlam Education Care,Kulia ni Meneja Mkuu wa Bima ya Maisha, Wilson Mnzava. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life Insurance, Julius Magabe (wapili kushoto), akimkabidhi Hati ya Bima ya Elimu wa 'Sanlam Education Care', Meneja Mkuu wa Bima ya Maisha, Wilson Mnzava (wapili kulia), wakati wa uzinduzi wa bima hiyo, Dar es Salaam leo. Kulia ni Mchambuzi wa mahesabu ya Bima wa kampuni hiyo, Kyenekiki Kyando na kushoto ni Meneja Mkuu wa Uhusiano wa Biashara, Nura Masood. Kampuni inayoongoza kwa utoaji wa bima za maisha TanzaniaSanlam Life Insurance, leo, imezindua bima ya elimu ya kipekee inayolenga...

ZARI THE BIG BOSS NA DIAMOND PLATINUMS KIMENUKA ULAYA,MAZITO YAIBUKA.

Image
Hakuna furaha isiyo na karaha! Ndiyo kauli inayoweza kutumika kwenye habari ya ziara ya Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Familia ya Wasafi Classic Baby (WCB) huko barani Ulaya ambapo staa huyo na mama mtoto wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, wanadaiwa kukinukisha, kisa kikidaiwa ni wivu wa mapenzi, Amani limenyetishwa. NI MUDA MFUPI BAADA YA KUTUA SWEDEN Habari kutoka kwa chanzo chetu makini ambacho ni mmoja wa watu waliopo kwenye msafara wa ziara hiyo iliyopewa jina la From Tandale to the World, zilidai kuwa, mwishoni mwa wiki iliyopita, Zari na Diamond walitibuana muda mfupi baada ya kutua katika Jiji la Stockholm nchini Sweden kwa ajili ya shoo. Kilidai kwamba, Diamond alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuvamiwa na warembo wakimtaka kimapenzi huku Zari akishuhudia. CHANZO CHATIRIRIKA “Huku kuna ishu ambayo ni nyeti sana maana kilichomkuta Diamond kwa Zari walipofika hotelini kama isingekuwa sisi kuokoa jahazi basi hata shoo zingeharibika ma...

BREAKING NEWZ:Takukuru Imewapandisha Kortini Wabunge Hawa Leo kwa Rushwa.

Image
Kutoka kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Mh. Kangi Lugola, Mbunge wa Mvomero Mh. Sadiq Murad pamoja na Mbunge wa Lupa Mh. Victor Mwambalaswa . Wakijadiliana jambo Dar es Salaam Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), leo imewaburuza kwenye Mahakama ya Kisutu jijini Dar, wabunge wa 3 wa Kamati za Kudumu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaotuhumiwa kwa rushwa. Wabunge hao ni Mbunge wa jimbo la Mwibara, Mh. Kangi Lugola, Mbunge wa Mvomero Mh. Sadiq Murad pamoja na Mbunge wa Mh.Victor Mwambalaswa. Taarifa zaidi za tukio hilo zitawajia kadri tutakavyozipata.

Waziri wa Rwanda Afia Gerezani Burundi

Image
Bujumbura, Burundi WAZIRI wa zamani wa Rwanda, Jacques Bihozagara amefariki katika gereza moja nchini Burundi miezi minne baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kufanya ujasusi. Rwanda imesema marehemu Jacques alikuwa ameshikiliwa kinyume cha sheria. Balozi wa Rwanda nchini Ubelgiji ameandika na kusema kifo cha Jacques ni “mauaji”. Wafungwa katika gereza alipokuwa ameshikiliwa wanasema alionekana akiwa katika hali nzuri na kwamba alifariki dakika chache baada ya kuchukuliwa kutoka gereza kupelekwa hospitali baada ya kuugua. Umoja wa Mataifa umekuwa ukiishutumu Rwanda kwa kujaribu kuipindua serikali ya Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, madai ambayo Rwanda imekuwa ikiyakanusha.

Ruge akanusha Gerald Hando na PJ kuacha kazi!

Image
Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba. MKURUGENZI wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba,  leo kupitia kipindi cha Power Breakfast‬ amekanusha uvumi wa watangazaji wa kituo hicho, Gerald Hando, Abel Onesmo na PJ,  kuacha kazi. “Kwa nafasi yangu kama mkurugenzi,  taarifa nilizonazo ni kwamba tuna mikataba na wafanyakazi hao ambayo inaisha leo tarehe 31.  Sehemu kubwa ya wafanyakazi  wetu mikataba yao inaisha mwezi huu, hivyo  katika hali ya kawaida huwa tunatoa nafasi ya kumwambia anayetaka kuendelea na mkataba aandike barua au aseme,” alisisitiza Mutahaba

MWANZA NA ARUSHA YAONGOZA WATUMISHI HEWA.

Image
  Waziri wanchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene akizungumza na Wakuu wa Mikoa leo jijini Dar es Salaam.   Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza baada ya kukabidhi majina hewa kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam.   Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadik  akikabidhi majina hewa kwa kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam.   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  akizungumza Waziri wanchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene  baada ya kumkabidhi majina watumishi hewa , jijini Dar es Salaam.   Mkuu wa Mkoa wa Tabora , Aggrey Mwanri akikabidhi majina ya watumishi hewa kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam.   Mkuu wa Mkoa wa Lindi ,Godfrey Zambi akikabidhi majina ya watumishi hewa kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene...

SERIKALI KUSAIDIANA NA TAASISI YA MILLEN MAGESE MAPAMBANO DHIDI YA TATIZO LA ENDOMETRIOSIS

Image
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa hotuba yake katika semina hiyo. Kushoto ni Mwasisi wa Taasisi ya Millen Magese, Millen Happiness Magese. (Picha na Andrew Chale, Modewjiblog ). Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imesema kuwa ipo tayari kushirikiana na wadau mbalimbali akiwemo Mwanadada Millen Magese na Taasisi yake katika mapambano ya ugonjwa na athari za Endometriosis ambao unawapata wanawake wengi hapa nchini. Kauli hiyo imetolewa mapema leo Machi 30.2016 na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati wa kufungua rasmi semina maalum kwa vijana wapatao 500 wa shule za Sekondari zikiwemo za Turiani Sekondari,  Makurumla na zinginezo za Manispaa ya Kinondoni pamoja na walezi na walimu, ambapo katika mkutano huo, Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, juhudi zinazofanywa na Mwanadada Millen Magese ni za kuu...

MWANZA NA ARUSHA YAONGOZA WATUMISHI HEWA.

Image
  Waziri wanchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene akizungumza na Wakuu wa Mikoa leo jijini Dar es Salaam.   Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza baada ya kukabidhi majina hewa kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam.   Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadik  akikabidhi majina hewa kwa kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam.   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  akizungumza Waziri wanchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene  baada ya kumkabidhi majina watumishi hewa , jijini Dar es Salaam.   Mkuu wa Mkoa wa Tabora , Aggrey Mwanri akikabidhi majina ya watumishi hewa kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam.   Mkuu wa Mkoa wa Lindi ,Godfrey Zambi akikabidhi majina ya watumishi hewa kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawen...