Posts

Showing posts from March 7, 2016

RAIS WA VIETNAM KUFANYA ZIARA YA KWANZA YA KITAIFA NCHINI

Image
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga (Mb.) (kulia), akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu ziara ya kitaifa ya siku 4 ya Rais wa Vietnam nchini, Mhe.Truong Tan Seng kuanzia tarehe 08 hadi 11 Machi, 2016. Ziara hiyo itakuwa ni ziara ya kwanza ya kuja Tanzania pia Afrika. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga naye akisikiliza kwa makini mazungumzo ya Waziri na Waandishi wa Habari. Waandishi wa Habari wakimsikiliza kwa makini Balozi Mahiga (hayupo pichani).

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AWAHUTUBIA WANAWAKE KWENYE MAADHIMISHI YA KIMATAIFA YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani iliyoandaliwa na Kampuni ya TRUMARK katika ukumbi wa Kingsolomon Kinondoni jijini Dar es salaam jana March 05,2016. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Wajasiriamali wa Vikundi vya Vikoba kutoka katika taasisi mbalimbali kwenye maonesho ya maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani yaliyondaliwa na Kampuni ya TRUMARK katika ukumbi wa Kingsolomon Kinondoni jijini Dar es salaam jana jioni March 05,2016. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA AENDELEA NA ZIARA MKOANI SIMIYU

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na watumishi wa serikali katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Metu akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 5, 2016. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipoingia kwenye uwanja wa Stendi ya Mwanhuzi wilayani Meatu kuhutubia Mkutano wa hadhara Machi 5, 2016. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipoingia kwenye uwanja wa Stendi ya Mwanhuzi wilayani Meatu kuhutubia Mkutano wa hadhara Machi 5, 2016.Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina na wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Erasto Mbwilo.  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akikagua jengo la matibabu ya wazee baada ya kulizindua kwenye hospitali ya Wilaya ya Meatu iliyopo Mwanhuzi akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 5, 2016.