Posts

Showing posts from February 26, 2017

RAIS MUSEVENI ATEMBELEA VIWANDA VYA BAKHRESA LEO JIJINI DAR

Image
  Rais wa Uganda Mhe.Yoweri Museveni(wapili kushoto) akiulizia jambo wakati wa ziara yake katika viwanda vya Kuzalisha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz, Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Hussein Sufiani na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru.   Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa    Bw. Salim Aziz akimkabidhi zawadi Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni baada ya kumaliza ziara katika viwanda vya Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni    na    Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo.  Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akifurahia zawadi aliyopewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz (wapili kulia) mara baada ya kumaliza ziara katika viwanda vya K

RC MAKONDA AELEZA KILICHOMFANYA ATAJE MAJINA YA WATUHUMIWA WA DAWA ZA KULEVYA

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa uamuzi wa kuwataja hadharani majina ya watuhumiwa wa biashara ya dawa za kulevya ni kutokana na maombi ya Watanzania waliyayotoa wakati wa serikali ya awamu ya nne. Makonda alisema kuwa licha ya watu wengi kupaza sauti zao wakitaka watuhumiwa wa dawa za kulevya watajwe hadharani, lakini Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete yeye hakuwataja huku akiacha vyombo husika vifanyekazi zao kwa usiri. Lakini kwa upande wa serikali ya awamu ya tano, waliamua kuwataja watuhumiwa hao ikiwa ni kujibu maombi ya kile watanzania walichokitaka tangu kipindi cha nyuma, alisema Makonda jana akiwa kwenye semina ya Walimu Wanaosomesha Quran Tanzania (JUWAQUTA). Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza katika unafunguzi semina ya Walimu wanaosomesha Qur-an Tanzania (JUWAQUTA) leo jijini Dar es Salaam. “Mzee Jakaya mlimpigia kelele taja, taja, taja, taja, sasa tulipoingia sisi tukaona wacha tufanye kama

HIVI NDIVYO SIMBA ILIVYOIZIMA YANGA UWANJA WA TAIFA

Image
Wachezaji wa Simba wakiwa wamembeba winga wa kulia wa timu hiyo Shiza Kichuya mara baada ya kuipatia Simba bao la ushindi katika mchezo wake wa ligi kuu ya Viodacom Tanzania Mameneja wa timu ya Simba wakiwa wamembeba mchezaji Shiza kichuya mara baada ya kuipatia timu hiyo bao la kuongoza katika mchezo wake dhidi ya Yanga Mashabiki wa Yanga wakiwa wamekaa kwa huzuni mara baada ya timu yao kupigwa bao 2-1 na timu ya Simba katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania. Mashabiki wa timu ya Simba wakishangilia kwa furaha mara baada ya timu yao kuibuka na ushindi wa bao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacoma Tanzania. Kiungo wa kati wa Yanya Haruna Niyonzima akijaribu kumtoka beki wa SimbaJanvier Bukungu Mshambuliaji wa Simba Laudit Mavugo akiweka sawa mpira mbele ya beki wa kati wa Yanga Kelvin Yondan Golkipa wa Yanga Deogratius Munishi akiokoampira uliopigwa na mshambualiaji wa Simba Laudit Mavugo Kiungo wa Simba Said Ndemla akiwania m

GARI LA MBUNGE LAUA, MWENYEWE ANUSURIKA

Image
Mtumishi wa Hospitali ya Wilaya ya Magu mkoani Mwanza, Moses Mjuni amefariki dunia baada ya kugongwa na gari la Mbunge wa Tarime Mjini (Chadema), Esther Matiko katika Kijiji cha Kishamba wilayani humo.Mkuu wa Wilaya ya Magu, Khadija Nyembo alisema jana kwamba ajali hiyo ilitokea juzi saa mbili usiku, “Gari la mbunge lilimgonga mtumishi wetu wa Hospitali ya Magu ambaye alikuwa anaendesha pikipiki na dereva wa gari hilo amekamatwa yupo polisi,” alisema Nyembo. Akizungumza kwa simu jana, Matiko alisema ajali hiyo ilitokea takribani kilomita 10 kutoka Daraja la Mto Simiyu wakati akitoka Mwanza ambako walikutana na mwendesha pikipiki na dereva wake, Kelvin Matango alikuwa akimkwepa baada ya kuingia upande wake. “Nilitoka Mwanza saa 12:00 jioni kwenda jimboni kwangu (Tarime), tulipopita mbele kidogo karibu kilomita10 kutoka daraja la Mto Simiyu, ghafla alijitokeza mwendesha pikipiki akawa anaendesha kwa kuyumbayumba na dereva alishindwa jinsi ya kumkwepa akamgonga,