Posts

Showing posts from February 16, 2016

Mume amfunga mkewe mtini kisa kutopata mimba

Image
Jeni Marwa akiwa amefungwa kamba mtini na mumewe. Stori: Gregory Nyankaira, UWAZI MARA: Nyango Hakimu mwenye umri wa miaka 37, anatafutwa na polisi akidaiwa kumfunga mkewe Jeni Marwa (23) kwenye mti na kumpa kichapo kilichomsababishia majeraha kwa madai ya kutoshika ujauzito kwenye ndoa yao. Tukio hilo lilitokea jioni ya Februari 6, mwaka huu katika Kijiji cha Singu, kilichopo Kata ya Kukirango wilayani Butiama mkoani Mara, ambako mwanamke huyo alipigwa kwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake, akidaiwa kutokuwa na faida nyumbani hapo. Mashuhuda wa tukio hilo wamesema, baada ya mumewe kumfunga mkewe kamba mikononi na miguuni kabla ya kumfunga kwenye mti na kuanza kumchapa, mwanamke huyo alipiga mayowe ya kuomba msaada ndipo watu walifika na kumkuta akitokwa damu nyingi baada ya kukatwa na kisu mguuni. Huku mumewe akiwa amekimbilia kusikojulikana, wasamaria wema walimchukua na kumpeleka Kituo cha Polisi cha Kiabakari ambako alipewa fomu ya matibabu (PF3) kabla ya

BREAKING NEWS:Waziri wa elimu amfuta kazi Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo

Image
Waziri wa Elimu Sayansi, Teknolojia na ufundi, Prof Joyce Ndalichako. Waziri wa Elimu Sayansi, Teknolojia na ufundi, Prof Joyce Ndalichako amesitisha mkataba wa kazi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo  George Nyatenga.    Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo  George Nyatenga. Pia amewasimamisha kazi wakurugezi watatu wa Bodi hiyo ambao ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Yusufu Kisare, Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo Juma Chagonja na Mkurugenzi wa Upangaji na Utoaji Mikopo. Prof Ndalichako  amemwagiza Mkaguzi wa ndani Mkuu wa Serikali ahakiki maelezo na Nyaraka zilizowasiliwa na Bodi ya Mikopo pamoja na kufanya ukaguzi maalum kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2013 hadi sasa. Mesothelioma Survival Rates About 40 percent of patients with mesothelioma survive the first year after diagnosis. That survival rate depends on many factors, including age, cancer stage,

MSANII WA BONGOFLEVA JONI WOKA AFARIKI DUNIA

Image
Maregehemu Michael Denis a.k.a Joni Woka enzi za uhai wake Akiongea kwa simu kaka wa marehemu Omari Milay, amesema walipigiwa simu alfajiri ya leo na kujulishwa kuwa Michael Denis  aliyejizolea umaarufu mkubwa kwa jina la Joni Woka amefariki katika hospitali ya Muhimbili, alipokuwa akipata matibabu ya ajali aliyopata siku ya jana. Michael Denis a.k.a Joni Woka alipata ajali ya kugongwa na kitu kizito kwenye paji la uso, alipokuwa garage maeneo ya Sinza akitengeneza gari yake, kwa bahati mbaya mtungi wa gesi ukalipuka na moja ya vipande vya chuma chenye ncha kali kikamchoma kichwani, Tarifa za awali za madaktari zilisema wanahofia kipande hiko kimefika mbali kiasi kwamba damu inamwagikia kwenye ubongo. Mipango ya mazishi familia imesema inakutana kujadili na mara itakapokamilika watajulisha watu nini kinaendelea. Msanii John Woka ambaye alikuwa kwenye kundi la Watukutu Family, alijipatia umaarufu kwa nyimbo zake za Sophia, baby gal na nyinginezo, ambazo aliziimba k

Aliyejipachika cheo cha usalama wa taifa akiona!

Image
Wakimfunga kamba. S tori: Makongoro Oging’ na Issa Mnally, UWAZI DAR ES SALAAM: Ujanja wa mjini! Jamaa aliyejipachika cheo kuwa yeye ni Afisa Usalama wa Taifa, Ofisi ya Waziri Mkuu akijitambulisha kwa jina moja la Manase amekiona cha moto baada ya kunaswa na kufungwa kamba mwilini na mtu aliyesema ni daktari wa Kliniki ya Head 2 ya jijini Dar, Fortdas Fidell. Tukio hilo la aina yake lilitokea Jumatano ya Februari 10, mwaka huu katika kliniki hiyo inayojishughulisha na tiba ya mifupa na mazoezi iliyopo Mtaa wa Ununio, Kata ya Kunduchi wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo risasi sita zilipigwa hewani na mtu aitwaye Mashaka Ndonde ili kumdhibiti mtuhumiwa huyo. UWAZI LAFIKA ENEO LA TUKIO Baada ya kusikika kwa milio ya risasi, baadhi ya watu walilipigia simu Uwazi na kuhabarisha tukio hilo ambapo waandishi wetu walifika mara moja eneo hilo na kuweza kukutana na Dk. Fidell ambaye alisimulia kisa cha kufyatuliwa kwa risasi na kushikiliwa kwa ‘afisa usalama’ huyo

MAJALIWA AKABIDHIWA NAKALA YAKE YA FOMU YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea nakala yake ya  fomu ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma kutoka kwa Kamishina wa Maadili, Jaji Mstaafu Salome  Kaganda ambayo aliitia saini na kuipeleka kwenye Secretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambako ilitiwa saini na kamishina huyo. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Februari 15, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Secretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambao walikwenda ofisini kwake jijini Dar es salaam Februari 15, 2016 kumpatia nakala yake  ya fomu ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma  ambayo aliitia saini  na kuipeleka kwenye Secretarieti  hiyo ambako ilitiwa saini na Kamishina wa Maadili, Jaji Mstaafu Salome Kaganda (wapili kulia).Kushoto ni Katibu wa Idara ya Viongozi Watumishi wa Umma, Secretarieti ya Maadili , John Kaole na kulia ni Katibu wa Idara ya Viongozi wa Siasa, Secret