YAMETIMIA CCM KALENGA YAFIKA UKOMO MTOTO WA MGIMWA APEWA KURA ZA RAMBIRAMBI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa mkono wa pole Godfrey Mgimwa, mmoja wa watoto wa Marehemu Dkt William Mgimwa, wakati wa mazishi kijijini Magunga jimbo la Kalenga mkoani Iringa Godfrey Mgimwa, mmoja wa watoto wa Marehemu Dkt William Mgimwa, akiongea kwa niaba ya familia wakati wa mazishi kijijini Magunga jimbo la Kalenga mkoani Iringa Na Francis Godwin Iringa. Mtokeo ya kura za maoni ndani ya CCM yametangazwa usiku wakuamkia leo mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Godfrey Mgimwa akishinda kwa kishindo katika nafasi hiyo huku Jackson Kiswaga akifuatia katika matokeo hayo. Mtoto wa Mgimwa amepata kushinda kwa kura 342 huku Kiswaga akipata kura 170 na mkuu wa wilya ya Pangani Hafsa Mtasiwa akiambulia kura 42 . matokeo hayo yametangazwa katika ukumbi wa shule ya sekondari Mwembetogwa mjini Iringa huku mgombea Peter Mtisi akipata kura...