Posts

Showing posts from August 23, 2018

Mabasi Mawili ya Wanafunzi Yagongana, Dereva Afariki

Image
Muonekano wa basi la shule ya Kivulini baada ya ajali. Basi la shule ya Nyamunge likionekana baada ya ajali. Mabasi mawili ya wanafunzi ya Shule za Kivulini na  Nyamunge yamengana uso kwa uso katika Barabara ya Mwanza–Simiyu katika eneo la Nane Nane mkoani Mwanza na kusababisha kifo cha dereva na wanafunzi wanane wa shule hizo kujeruhiwa.

Wakili wa kesi ya Mbowe na wenzake ajitoa

Image
WAKILI Jeremiah Mtobesya aliyekuwa akiwawakilisha Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na viongozi wenzake nane wa chama hicho, amejitoa kwenye kesi hiyo leo Agosti 23 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri. Mtobesya amejitoa katika kesi hiyo baada ya Mahakama ya Hakimu Kisutu kutupilia mbali maombi yao ya kutaka kesi hiyo ya jinai namba 112 ya mwaka 2018 iahirishwe katika Mahakama ya Kisutu ili kusubiri  maombi yao na rufaa yaliyowasilishwa kwenye Mahakama ya Rufani yasikilizwe kwanza na kutolewa maamuzi. Kwa upande wake, hakimu Mashauri alitupilia mbali maombi hayo kwa maelezo kwamba, kifungu cha sheria walichotumia cha 225 (1) (2) cha Mwenendo wa Mashauri ya Jinai Sura ya 20 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 hakiipi mamlaka hayo. Ikumbukwe kwamba, Mbowe na wenzake wanakabiliwa na mashtaka 13 ikiwamo  kuhamasisha maandamano Februari 16 mwaka huu siku moja ya uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Kinondoni yaliyo...

NAFASI ZA KAZI 45 HOSPITALI YA BUGANDO

Image
OFISI ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imetangaza nafasi 45 za kazi Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza za Medical Attendant daraja la II, mwisho wa kutuma maombi ni 2018-08-29 MEDICAL ATTENDANT II.. – 45 POST Employer: Bugando Medical Centre Date Published: 2018-08-15 Application Deadline: FASI DUTIES AND RESPONSIBILITIES: i. Providing basic health education to in patients and relative ii. Ensuring that all utensils are clean. iii. Inspecting the Institute clinical areas. iv. Advising matron on all matters relating to cleaning duties. QUALIFICATION AND EXPERIENCE: Holder of an Ordinary Secondary School Certificate. Must have a Pre-Nursing Certificate OR Certificate in Community Health from recognized institution REMUNERATION: Salary Scale PMOSS.2.1. Login to Apply

Irene Uwoya ampa za uso shabiki Instagram

Image
 Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na akanti nyingi ‘fake’ za Instagram ambazo zinatumia majina ya mastaa na viongozi wa serikali na usipokuwa makini unaweza kugombana na kila mtu mtandaoni. Kwani akaunti hizo zimekuwa zikitumiwa na watu hao kwaajili ya kuwachonganisha mastaa kwa mastaa ili wapate followers. Hayo yamemkuta malkia wa filamu, Irene Uwoya baada ya kuingia kwenye majibizano na akaunti ‘fake’ ambayo inatumia jina la Jokatemwegeelo akidhani anabishana na Mhe DC Jokate, ambae kupitia mtandao huo anatumia jana Jokate Mwegelo. Kaunti hiyo ‘fake’ ilionekana ikidai muigizaji huyo wa filamu amekuwa akitumia muda mwingi kwenye kujiremba na sio kufanya kazi.

RC Mongella ashiriki mazishi ya Bibi yake Paul Makonda

Image
Na James Timber, Mwanza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella leo Agosti 23, ameungana na waombolezaji mbalimbali kushiriki mazishi ya Bi. Anna Makwega Manasse (81) ambaye ni Bibi wa Mkuu wa Mkoa Dar es salaam Paul Makonda. Mazishi ya Bi. Manasse ambaye alifariki dunia juzi Agosti 21, Mwaka huu akiwa katika hospitali ya Rufaa Bugando Jijini Mwanza alikokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu, yamefanyika katika makaburi ya nyumbani yaliyopo Kahangala wilayani Magu. Akizungumza kwa niaba ya viongozi wa serikali mkoani Mwanza, Mkuu wa Mkoa Mongella amewaombea kuwa na uvumilivu kwa  ndugu, jamaa na marafiki kutokana na msiba huo na kuwahimiza kumuombea kwa Mola ili apumzike kwa Amani.

Haji Manara Awapa Makavu Mashabiki wa Simba

Image
Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara. Msemaji wa klabu ya Simba mwenye mbwembwe nyingi miongoni mwa klabu za soka nchini, Haji Manara, ameibuka kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuwapa makavu mashabiki wa Simba wanaoponda ushindi wao bao 1-0 dhidi ya Prisons walioupata jana uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar katika mchezo uliofungua pazia la Ligi Kuu mwaka huu. Alichokisema:- Wakati mwingine najiuliza nn wanadaamu wanataka?hasa washabiki wa Mpira!! Nimetalii kdogo kwenye magroup machache ya Wanasimba kwenye WhatsApp nimeshangaa baadhi yetu kutokuridhika na ushindi wa leo wa goli moja dhidi ya Prisons Wengine kwenye Instagram wanafika mbali zaidi eti mfumo wa kocha haufai!! Guys mpira ni sayansi kubwa kuliko kwenda mwezini au daktari kumfanyia upasuaji wa kichwa mtu,ukubwa wa Sayansi hii ni kwamba hujui mpinzani wako kajipangaje..hujui kama siku hyo wachezaji wako watacheza kwa kiwango gani lakini kubwa Sayansi hii haina jawabu la moja kwa moja kam...

Diamond uso kwa uso na Rich Mavoko

Image
Msanii wa muziki wa kizazi kipya na C.E.O wa lebo ya WCB Wasafi Diamond Platinumz leo amekutana uso kwa uso na aliyekuwa msanii wake Rich Mavoko katika ofisi za baraza la sanaa Tanzania Basata. Diamond wamekutana na Mavoko katika ofisi hizo kwa lengo la kuongelea tofauti zao ambazo zimejitokeza kwa kile kinachodaiwa kuwa Rich Mavoko amejitoa katika lebo hiyo. Mavoko alijiunga na WCB mwaka 2016 akisaini chini ya lebo hiyo na kuanza kufanya kazi akiwa chini ya lebo hiyo ambayo boss wake ni Diamond Platinumz. Baada ya kujiunga na lebo hiyo Mavoko alianza malalamiko mapema mwaka huu kuwa anataka kujitoa katika lebo hiyo ya WCB wasafi kwa madai kwamba ananyonywa kimaslahi. Mbali na kunyonywa kimaslahi lakini pia ilidaiwa kuwa kuna vitu ndani ya makataba huo msanii huyo hakutimiziwa na boss wake kama mkataba ulikuwa unaelekeza. Malalamiko ya Mavoko yalionekana kuwagusa wengi na ikachangia Mavoko kukaa kimya kwa muda ingawa siku za hivi karibuni aliachia ngama yake...