Amfumania mume, achoma nyumba!
Monika akiwa amezimia. Waandishi wetu, Amani Dar es Salaam: Mapenzi uchizi! Hii ndiyo kauli pekee unayoweza kuitumia baada ya mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Monika, mkazi wa Tabata-Senene jijini Dar, kudaiwa kumfumania mumewe na mchepuko ndani kwake kisha kuchoma moto nyumba kabla ya kuzimia. Nyumba ilivyochomwa moto. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo lililojaza umati, sekeseke hilo lilijiri wiki iliyopita, mishale ya saa 5:00 asubuhi nyumbani kwa wanandoa hao maeneo hayo ambapo mwanamke huyo hakuwepo nyumbani hivyo aliporudi ndipo akaanzisha timbwili, akidai kumkuta mumewe ndani na mchepuko. “Unaambiwa baada ya Monika kurudi nyumbani na kumfuma mumewe ‘akimalizana’ na mchepuko, palikuwa hapatoshi. “Monika aliangusha timbwili la aina yake lakini yule mchepuko alifanikiwa kutoka nduki. “Kutokana na hasira, Monika alijifungia ndani, akamwagia nyumba mafuta ya taa, akawasha moto akitaka kujitoa uhai. “Tunashukuru Mungu, askari wa zima moto walifika na k...