RAIS KIKWETE AZINDUA MTAMBO WA KUHAKIKI TAKWIMU ZA MAWASILIANO
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System) leo February 27, 2014 katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pro, Makame Mnyaa Mbarawa, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadick na wadau wengine wa tehama. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibofya kitufe kuzindua rasmi Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System) leo February 27, 2014 katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar es salaam. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System) aliouzindua leo February 27, 2014 katika j...