WEWE MWANAUME UNAYESOMA HAPA, JIULIZE; HUWA UNADUMU NA MWENZI WAKO? UNAACHWA AU KUKIMBIWA BAADA YA MUDA MFUPI? KAMA JIBU NI NDIYO, HAPA UTAPATA TIBA. SIKIA NIKUAMBIE, WAPO WENGI AMBAO KILA WAKIANZISHA UHUSIANO, SIKU MBILI TATU, MWANAMKE ANAMKIMBIA. Anampenda sana, anamfanyia kila kitu ambacho yeye anaamini kinakidhi kwa mwanamke wake, lakini baada ya muda mfupi sana, anaachwa! Anabaki kujiuliza maswali yasiyo na majibu. Rafiki yangu, lazima ujue kwamba pamoja na kuwa mapenzi hayana kanuni za moja kwa moja, zipo ndogo ndogo ambazo zikifuatwa, mateso kwako yatakuwa ni kitendawili. Huwezi kukimbiwa na wanawake bila sababu za msingi, lazima kuna kitu kinachosababisha uachwe. Hapo sasa hakuna sababu moja, wewe ukiachwa kwa sababu hii, mwingine atakimbiwa kwa sababu ile. Katika darasa hili, ukijifunza kwa umakini utaweza kujua kasoro yako ilipokuwa na kufanya mabadiliko ili ‘usiachike’ tena! Wanaume huwa wanawalaumu zaidi wanawake kutokana na sababu za hapa...