Posts

Showing posts from February 21, 2016

Mbinu mpya ya Mastaa kujiuza

Image
Masogange Na Mwandishi wetu, Risasi Jumamosi DAR ES SALAAM: Imevuja! Siri ya maisha mazuri ya baadhi ya mastaa wa kike Bongo ambao hawafanyi filamu, Bongo Fleva wala kazi yoyote imejulikana huku aibu kubwa ikiwafuata nyuma ya siri hiyo, Risasi Jumamosi limefungasha mzigo wa kutosha! Kwa mujibu wa chanzo chetu kikuu kikizungumza na Risasi Jumamosi, mastaa hao wamekuwa wakitumia njia ya kisasa ambayo ni Mtandao wa Kijamii wa Instagram kupata wanaume wenye fedha ambao hujitokeza na kuwataka kimapenzi, wengi wao wakiwa nje ya nchi. Giggy Money NCHI ZENYE WATEJA WENGI Chanzo hicho ambacho na chenyewe ni staa, kiliendelea kusema kuwa, nchi ambazo mastaa hao wana soko kubwa ni China, Dubai na Afrika Kusini. India ni kwa mbali sana! INAVYOKUWA SASA Chanzo: “Ili tuweze kuonwa na wateja wetu hao, huwa tunatupia kwenye mtandao huo, picha zetu zenye mvuto tukiwa kwenye mapozi ya ‘ki-hasarahasara’, wengine hutupia mpaka picha za nusu utupu ili wanaume wakiwaona wavutike

Talaka ya Jide Mazito Yaibuka!

Image
Mkongwe wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ na mumewe Gardner G. Habash ‘Captain’. Na Musa Mateja Risasi Jumamosi DAR ES SALAAM: Siku chache baada ya staa mwanadada mkongwe wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ kupewa talaka mahakamani na mumewe Gardner G. Habash ‘Captain’ mazito yameibuka baada ya kubainika uwepo wa hati nyingine ya talaka aliyoitoa Gardner kwa mwanamke mwingine, Risasi limeinasa. Jide Chanzo makini kimepenyeza habari kuwa mbali ya Jide anayetarajia kuibuka na kishindo kikubwa cha mabadiliko ya muziki wake hivi karibuni, Gardner alimpa talaka mahakamani mkewe wa awali aliyefahamika kwa jina la Idda Pius Mkunja, mwaka 2003. “Mwenzangu Gardner anaonekana ndiyo kamchezo kake kumalizia ndoa mahakamani, ukiachana na Jide nimeona hati ya talaka nyingine aliyoitoa kwa Idda ambaye alimuona mwaka 1997,” kilisema chanzo hicho huku kikimpenyezea hati hiyo ya talaka (tazama pichani) mwanahabari wetu. Siku ya ndoa yao Kama hiyo haitoshi, c

WAZIRI NAPE AONGEZA HAMASA MECHI YA WATANI WA JADI SIMBA NA YANGA

Image
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (kushoto)walipokutana katika mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga Afrika na Simba Sports Club katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam.( Picha na: Frank Shija,WHUSM) Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na mashabiki wa mpira wa miguu wakati wa mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga Afrika na Simba Sports Club katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na mashabiki wa mpira wa miguu wakati wa mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga Afrika na Simba Sports Club katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam. Mabeki wa Timu ya Simba wakiokoa mpira wa hatari katika lango lao wakati wa mechi dhidi ya Yanga iliyochezwa katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam.Mechi hiy