TAMISEMI Yaagiza Shule Ichunguzwe Baada ya Wanafunzi Wote Kupata 0
WIZARA ya Ofisi ya Rais –Tamisemi kupitia kwa Naibu Wairi wake, Joseph Kakunda imemuagiza mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Njombe kuchunguza matokeo mabaya ya mtihani wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Viziwi Njombe. Akiji alipojibu swali la mbunge wa Buyungu (Chadema), Samson Bilago, bungeni leo Jumatano Januari 31,2018, Kakunda amesema katika matokeo yaliyotangazwa jana na Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), shule hiyo katika matokeo ya mtihani uliofanyika Oktoba na Novemba mwaka jana watahiniwa wote 21 wamepata daraja sifuri (0) yaani wamefeli. Bilago alitaka kujua ni kwa nini shule za wanafunzi wenye mahitaji maalumu zinafanya vibaya kwenye mitihani, ambapo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika amesema walimu waliosoma elimu maalumu watapata ajira bila kikwazo cha kusubiri huku akieleza kuwa anasubiri kupelekewa orodha ya walimu hao.