Fahamu aina saba za uvimbe kwenye mayai ya mwanamke
Kuna aina nyingi za uvimbe kwenye mayai ya mwanamke na kusababisha maumivu kwao lakini aina hizi saba ndiyo huonekana sana kwa wanawake wengi ambazo ni kama ifuatavyo: I. Follicular cyst : Ni uvimbe ambao hutokea wakati Ovulation isipotokea au baada ya Corpus Luteum kuanza kusinyaa na kupotea yenyewe baada ya kutopachikwa kwa yai kwenye kuta za mfuko wa kizazi. Uvimbe huu unakuwa na wastani wa inchi 2.3 kwa upana. Upasukaji wa uvimbe huu husababisha maumivu makali sana katikati ya mzunguko wa hedhi yaani siku ya Ovulation. Maumivu haya huonekana kwa robo ya wanawake wenye aina hii ya uvimbe. Kwa kawaida, uvimbe huu hauna dalili zozote na hupotea wenyewe baada ya miezi kadhaa. 2.Corpus Luteum cyst ; Ni uvimbe unaotokana na kutopachikwa kwa yai la uzazi lililorutubishwa na mbegu ya kiume kwenye mfuko wa kizazi. Kwa kawaida Corpus Luteum husinyaa na kupotea yenyewe, au wakati mwingine inaweza ikajaa maji na hivyo kusababisha uvimbe wa aina hii. Uvimbe huu huonekana kwen