Posts

Showing posts from April 29, 2018

RAIS MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA IRINGA-DODOMA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwakilishi wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Jeremy Aguma wa pili kutoka kulia wakivuta utepe kwenye jiwe la msingi kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Iringa-Dodoma katika sehemu ya Iringa-Migori-Fufu Km 189 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami. Sherehe hizo za ufunguzi zilifanyika katika kijiji cha Ndolela kilichopo Isimani nje kidogo ya mji wa Iringa. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwakilishi wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Jeremy Aguma, Balozi wa Japan Masaharu Yoshida wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Iringa-Dodoma katika sehemu ya Iringa-Migori-Fufu Km 189 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami. Wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Ujenzi Profesa Makame Mbarawa , Spika wa Bunge Job Ndugai pamoja na viongozi wengine wa Serikali na wageni k

Serengeti Boys wanyakua ubingwa wa CECAFA U- 17

Image
Timu ya taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) imeibuka na ubingwa wa CECAFA U-17 baada ya kuifunga timu ya vijana ya Somalia mabao 2-0 katika fainali iliyopigwa huko Burundi. Serengeti Boys imecheza vizuri mchezo huo wa fainali na kufanikiwa kuongoza kwa bao moja hadi mapumziko kabla ya kuongeza bao la pili kipindi cha pili na kujihakikishia ubingwa huo. Mabingwa hao wapya wa Afrika Mashariki na Kati, wamekabidhiwa kombe hilo na mgeni rasmi wa fainali hiyo ambaye ni Rais wa shirikisho la soka barani Africa Ahmed Ahmed. Vijana hao wametinga fainali hiyo baada ya kuwatoa timu ya Taifa ya Kenya U17 kwa jumla ya mabao 2-1 katika mchezo wa nusu fainali uliopigwa Alhamisi. Wakati Somalia imeingia fainali kwa kuifunga Uganda 1-0. Moja ya timu zilizofungwa na vijana hao katika hatua ya makundi ni pamoja na Sudan na Uganda. Katika michuano hii timu ya taifa ya vijana ya Zanzibar (Karume Boys) iliondolewa kutoka na kuwa na wachezaji we

ALIKIBA NA MKEWE AMINA WALIVYOINGIA UKUMBINI

Image
STAA wa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘Alikiba’ na mkewe, Amina raia wa Kenya wameingia katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena uliyopo Posta jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusherehekea harusi yao usiku huu wa Aprili 29, 2018. Katika sherehe hizo ambazo pia zinahusisha harusi ya mdogo wake Alikiba, Abdu Kiba na mkewe, Ruwayda imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo mke wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na Naibu Waziri wa Kazi, Anthony Mavunde. Tazama picha hizi. Picha na Azam TV.

ABDU KIBA NA MKEWE WALIVYOINGIA UKUMBINI

Image
MKALI wa Bongo Fleva, Abdu Kiba na mkewe, Ruwayda tayari wameshaingia katika Ukumbi wa Serena Hotel uliyopo Posta jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusherehekea harusi yao usiku huu. Katika sherehe hizo ambazo pia zinahusisha harusi ya Alikiba na mkewe, Amina imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo mke wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na Naibu Waziri wa Kazi, Anthony Mavunde. Tazama picha hizi. Picha na Azam TV.

MAMA KIKWETE, UMMY MWALIMU WATINGA HARUSI YA KIBA

Image
MKE wa Rais wa Awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amepata fursa ya kuhudhuria katika harusi ya staa wa Bongo Fleva, Alikiba na mkewe, Amina katika ukumbi wa Serena Hotel uliyopo Posta jijini Dar es Salaam usiku huu wa Aprili 29, 2018. Mama Salma ambaye pia ni mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameambatana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Watoto, Wanawake, Jinsia na Wazee, Dkt. Ummy Mwalimu katika seherehe hiyo. Katika sherehe hiyo pia inahusisha harusi ya mdogo wa Alikiba, Abdu Kiba na mkewe, Ruwayda ambao walifunga ndoa Jumapili iliyopita. Viongozi wengine waliopata fursa ya kuhudhuria sherehe hiyo ni Naibu Waziri wa Kazi ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde (kulia), na Mwenyekiti wa UVCCM, Khery James (kushoto). Picha na Azama TV.

WAMILIKI SOBA HOUSE WAWAJIBU WABUNGE TUHUMA ZA KUWACHOMA SINDANO WAATHIRIKA DAWA ZA KULEVYA

Image
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wamiliki wa Sober House Tanzania, Pili Missanah (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani). Baadhi ya viongozi wa  Sober House Tanzania walioshiriki mkutano huo na waandishi wa habari. WAMILIKI wa nyumba zinazosaidia waathirika kujinusuru na dawa za kulevya nchini maarufu kama Soba house wamejibu tuhuma za kuwachoma vijana sindano pindi wapatapo nafuu. Akiongea na waandishi wa habari leo Jiji Dar es Salaam Katibu wa Umoja wa Soba house nchini, Pili Missanah ambaye ni mmoja wa wamiliki wa vituo hivyo ameeleza kuwa, April 25 mwaka huu katika mjadala wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baadhi ya wabunge walieleza kuhusu tabia chafu  za baadhi ya wamiliki wa nyumba hizo kuwachoma sindano za dawa za kulevya baadhi ya waathirika pindi wanapokaribia kupona ili wazazi au walezi waendelee kuchangia fedha kwenye nyumba hizo. Pili ameeleza kuwa lengo la nyumba hizo sio baya bali ni kuwasaidia waathirika wa dawa za k

FT: SIMBA 1-0 YANGA, KUTOKA UWANJA WA TAIFA (KADI NYEKUNDU KESSY)

Image
MPIRA UMEKWISHA DAKIKA 4 ZA NYONGEZA Dk 90 Yanga wanaingia lakini Simba wamejaa nyum SUB Dk 83, Simba wanamtoa Gyan nafasi yake inachukuliwa na Paul  Bukaba Dk 82, Mahadhi anaingia na kujaribu kupiga krosi, Mkude ameunawa ni faulo si mbali na lango la Simba Dk 76, krosi maridadi katika lango la Simba, Chirwa anaruka na kupiga kichwa lakini ni goal kick Dk 70 Kichuya anapangua watu wawili, anatoa pasi kwa Bocco, naye anampa Kapombe kona ya saba ya Simba, Yanga hawana kona hata moja Dk 70 sasa, bado inaonekana Yanga wanafanya mashambulizi ya kufunga, lakini Simba wanapoteza nafasi nyingi na lazima wazitumie mapema maana Yanga bado nao wana uwezo wa kufunga Dk 67, Kichuya anamtoka Makapu, anaingia na kupiga krosi safi kabisa, Dante anapiga kichwa na kuokoa Dk 65 Yanga wanaonekana wanaanza kufunguka lakini Mlipili yuko makini, anaokoa unakuwa wa kurushwa Dk 63 mpira wa Okwi unaokolewa na kuwa kona ya sita ya SImba, inachongwa na kuokolewa SUB Dk 62, Yanga inafanya sub