Posts

Showing posts from April 19, 2018

SHUHUDIA UKUMBI WA HARUSI YA ALIKIBA NA AMINA UNAVYOWAKA

Image
BAADA ya Staa wa Bongo Fleva, Alikiba ‘King Kiba’ kufunga ndoa na mchumba wake, Amina Khaleef Mjini Mombasa nchini Kenya leo, Aprili 19, 2018, sherehe ya harusi ya msanii huyo inatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Mombasa. Kiba na Amina wamefunga ndoa katika msikiti wa Ummul Kulthum, mjini Mombasa leo Asubuhi ambapo tukio hilo limeshuhudiwa pia na ndugu na marafiki zake wa karibu wa msanii huyo. Kiba amesema ameamua kufunga ndoa yake siku ya leo kwani siku kama hii ndiyo wazazi wake walifunga ndoa yao miaka kadhaa iliyopita.  

BABU SEYA, FAMILIA YAKE WATINGA BUNGENI – PICHA

Image
MWANAMUZIKI nguli wa dansi,  Nguza Viking ‘Babu Seya’  na watoto wake ambao ni  Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ na Francis Nguza , leo Alhamisi, Aprili 19, 2018 wametembelea  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma  baada ya kualikwa na  Mbunge wa Viti Maalum CCM, Mariam Ditopile. Babu Seya na familia yake, walishangiliwa na Bunge zima baada ya kutambulishwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai,   baada ya kipindi cha maswali na majibu kumalizika bungeni humo. Wanamuziki hao walikuwa ni miongoni mwa wafungwa 8,157 waliosamehewa na Rais John Magufuli siku ya maadhimisho ya sherehe za uhuru wa Tanganyika, Desemba 9, 2017 zilizofanyika mjini Dodoma.

REKODI 3 NDOA YA KIBA!

Image
DAR ES SALAAM: Wakati mkali wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘AliKiba’ amefunga ndoa leo pande za Mombasa nchini Kenya, nyumbani kwa bibi harusi, Amina Khaleef, imeelezwa kuwa ndoa hiyo inatarajia kuandika rekodi ya mambo makubwa matatu. Akizungumza na Gazeti la Amani, mmoja wa mameneja wa mwanamuziki huyo, Aidan Sefu, alisema tayari wamelipwa mamilioni ya fedha na moja ya luninga ya hapa Tanzania kurekodi na kurusha live harusi hiyo.“Itakuwa kitu kikubwa sana, ni harusi ya aina yake hivyo nisingependa kuongea sana lakini watu wataona,” alisema Aidan. Kama hiyo haitoshi, Amani lilielezwa kuwa miongoni mwa rekodi zinazotarajiwa kuandikwa katika harusi hiyo ni pamoja na kukodiwa ndege maalumu ya kwenda Mombasa na kurudi Bongo. “Kutakuwa na utofauti mkubwa kwani Ali anatarajiwa kukodi ndege kumpeleka kama bwana harusi na ndege ya kumrudisha akiwa tayari na kifaa chake ili kuja kumalizia sherehe huku mwisho wa mwezi,” alisema mnyetishaji wetu. Pia mnyetishaji huyo alisema rekod

SHUGHULI YA NDOA YA ALIKIBA IMEANZA KENYA – Picha

Image
ILE siku iliyokuwa ikisubiliwa kwa hamu kushuhudia ndoa ya Staa wa Bongo Fleva, Alikiba ‘King Kiba’ hatimaye imewadia na leo Aprili 19, 2018 mkali huyo anafunga ndoa yake na mrembo Aminah Rikesh Khaleef mjini Mombasa nchini Kenya. Tayari wapenzi hao wanaofunga ndoa, Mashehe, ndugu na marafaiki wameshafika eneo ambapo ndoa hiyo inafungwa na tayari shughuli imeshaanza kama picha zinavyoonyesha. Watu wa karibu wa msanii huyo wameonekana mjini Mombasa, Kenya kwa ajili ya kuhudhuria ndoa hiyo. Baadhi ya picha tayari zimeanza kusambaa mitandaoni zikiwaonyesha watu hao akiwemo msanii wa filamu Bongo, Esha Buheti na dada yake Alikiba, Zabibu na wengine. Tazama video ushuhudie mwenyewe.

Rais Magufuli afanya uteuzi wa watu 10

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo April 18, 2018 ameteuwa watu kumi kushika nafasi mbalimbali akiwepo Prof. Idris Suleiman Kikula kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini. Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Kikula umeanza April 17, 2018

Jinsi ya Kupika Pilau ya Zabibu Kavu

Image
K WENYE ukurasa huu wa Mapishi ya Amani tutaona jinsi ya kupika pilau ya zabibu kavu ambayo ni tamu sana. MAHITAJI: -Mchele -Viungo vya pilau -Mafuta ya kupikia -Nyama -Vitunguu swaumu -Vitunguu maji JINSI YA KUPIKA: Andaa mchele wako uoshe kisha weka pembeni, baada ya hapo chemsha nyama yako na yenyewe iweke pembeni, ukimaliza weka sufuria kwenye moto na mafuta, anza kukaanga vitunguu. Weka kitunguu swaumu, ukimaliza kaanga weka viungo vikaangike vizuri kisha weka mchele ukaange sana mpaka uive wakati unakaanga weka na nyama ili vikaangike kwa pamoja ukimaliza weka maji na chuvi pika pilau lako taratibu. Wengine hupendelea kuweka viazi pia ambapo huvikaanga na mafuta na viungo lakini sio lazima sana unaweza kupika pilau la nyama tu.  Pilau likishaiva sasa chukua zabibu zako kavu ziweke kwenye chakula, geuzageuza kisha funikia liache kidogo kwanza. Baadaye pakua pilau lako litakuwa tayari kwa kuliwa.

Ijue misingi ya uvumilivu katika ndoa

Image
Ni wazi kuwa migogoro kwenye uhusiano wowote ule ipo, hasa pale wenza hao wasipopeana nafasi ya kusikilizana. Kila siku narejea hii hoja kuwa, hata kwenye uhusiano wa mapenzi lazima kutakuwepo na mikwaruzano ya hapa na pale jambo la msingi ni namna ya kushughulikia misuguano hiyo bila kuibua chuki na hatimaye kuvunja uhusiano. Hata katika uhusiano wa kawaida, mikwaruzano na misuguano ni kama kukanyaga bomu, bila kuchukua tahadhari na kutegua bomu lenyewe, ukiondoa mguu mtu bomu hilo linalipuka na kuharibu kila kitu. Uvumilivu ndio jibu kubwa kwa wenza endapo itatokea kukwaruzana au kutoelewana. Endapo mwenza wako amekuudhi na kukupandisha hasira jambo la msingi kabisa ni kuhakikisha unadhibiti hasira hizo. Jaribu kuelewa kwanza tatizo kabla hasira hazijakuathiri na kukutawala. Kumbuka kuwa hasira hasara na siku zote mtu mwenye hasira huzungumza na kufanya mambo ambayo baadaye hujikuta akijilaumu. Lakini pia watalamu wa masula ya mahusiano wanasema ya kwamba siku zot

Mbegu za Maboga Zinavyoweza Kukupa Ngozi Nzuri

Image
L EO kwenye safu yetu hii tutaona jinsi mbegu za maboga zinavyoweza kukupa ngozi nzuri na ukawa na muonekano wa kuvutia. MAHITAJI: -Kikombe kimoja cha mbegu za maboga. -Kikombe kimoja cha mafuta ya butter. -Yai moja. JINSI YA KUCHANGANYA: Chukua kikombe cha mbegu za maboga zilizosagwa, changanya na mafuta ya butter yaliyoyeyushwa. Baada ya hapo lipige yai lichanganye pia ili kuleta urahisi, tumia blenda kusagia mchanganyiko wako ukae vizuri. Ukimaliza paka mchanganyiko huo usoni acha kwa muda wa dakika kumi mpaka kumi na tano ukauke. Ukimaliza osha na maji masafi. Mchanganyiko huu ni mzuri kwa afya ya ngozi lakini pia husaidia kuondoa uchafu wote pamoja na chunusi ndogondogo

Fatma Karume aiomba radhi Serikali

Image
Rais mpya wa Chama cha wanasheria wa Tanganyika (TLS), Fatma Karume ameiomba radhi serikali kwa kutoa lugha kali ambazo zilizokuwa zinaenda moja kwa moja kugusa muhimili wa Mahakama kuhusiana na mambo ambayo yanayoendelea nchini kupitia Mahakama bila ya kufuata haki za kisheria Fatma Karume ambaye ni mtoto wa Rais mstaafu wa Zanzibar ametoa kauli hiyo leo Aprili 18, 2018 wakati akizungumza katika kipindi cha East Africa Breakfast kinachorushwa na East Africa Radio kwa njia ya simu ambapo amesema zoezi la kuteua Majaji nchini liangalie zaidi taaluma za wanaoteuliwa badala ya kuwateua kwa mlengo wa kisiasa. "Mahakama ni mhimili unaojitegemea hivyo ni vema ukaheshimiwa kwa kuchagua Mahakimu wenye vigezo vya kitaaluma ambao watasimamia vema sheria badala yakuyumbishwa na siasa. Mimi nipo tayari kushirikiana na serikali kwa sababu siwezi kutengeneza bajeti lakini naweza kushirikiana nao katika kuelezea mapungufu yaliyopo", amesema Fatma. Mbali na hilo, Rais

Zitto Kabwe: Nipo tayari kwa lolote

Image
Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia ACT Wazalendo Mhe. Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuwa yupo tayari kukamatwa na polisi lakini pia yupo tayari hata kuuwawa kwa ajili ya kuisemea trilioni 1.5 ambayo CAG amesema haijatolewa maelezo imetumikaje. Zitto Kabwe amesema hayo leo April 18, 2018 baada ya Katibu Mwenezi wa CCM Humphrey Polepole kusema kuwa wapo viongozi wa upinzani wanasema uongo juu ya ripoti Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kutaka watu hao wachukuliwe hatua. Kufuatia kauli hiyo Zitto Kabwe amesema kuwa anauhakika kuwa serikali ya awamu ya tano imeshindwa kuonyesha matumizi ya trilioni moja na bilioni mia tano. "Kuna mtu anasema nikamatwe kwa kupotosha Kuhusu TZS 1.5trn zinazohojiwa na CAG. Mimi Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto, Mwenyeji wa Kigoma, Muislam, naapa kwamba Serikali ya CCM ya awamu ya tano imeshindwa kuonyesha kwa CAG matumizi ya shilingi trilioni moja na bilioni mia tano. Nipo tayari kukamatwa kwa kusema hivyo ( haitafuta