Posts

Showing posts from March 17, 2015

YEMI ATANGAZA SIKU YA KUZIKWA BABA YAKE.

Image
Baba yake Yemi Alade aliyekuwa Kamishna Mstaafu wa Polisi, J.A. Alade enzi za uhai wake. MWANAMUZIKI wa kike wa Nigeria, Yemi Alade,  na familia yake watafanya  maziko ya marehemu baba yake tarehe 7 na 8 Mei mwaka huu. Baba yake Alade aliuyekuwa Kamishna Mstaafu wa Polisi, J.A. Alade, alifariki  Januari 16 mwaka huu na binti yake huyo ambaye ni mtunzi wa wimbo maarufu wa ‘Johnny’, hajasema mengi kuhusiana na kifo hicho tangu kitokee. Mwanamziki wa kike wa Nigeria anayetamba kwa wimbo wa Jonny, Yemi Aladeakiwa katika pozi. Ni katika mahojiano ya gazeti la Tribune yaliyofanyika Machi 13, mwaka huu (siku ya kuzaliwa kwake) ndipo  aliposema maziko ya baba yake yatafanyika Mei 7 na 8. Yemi Alade ni mtoto wa mwisho kwa baba yake huyo kutoka kabila la Wayoruba na mama kutoka kabila la Waigbo.

MWANAFUNZI ATEKWA, AUAWA

Image
Na Waandishi Wetu DUNIA imekwisha jamani! Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Mabibo, Dar, Irene Said (15) ametekwa, amebakwa na kuuawa kikatili kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili huku ikidaiwa kuwa, kijana mmoja asiyejulikana alifika nyumbani kwao, Kigogo Luhanga na kutaka kiroba na mtu mmoja waongozane akabebe ndizi. Polisi wakiwa wamebeba mwili wa marehemu. Akizungumzia tukio hilo la kusikitisha sana, mama mdogo wa marehemu, Doto Lucas alisema:  “Siku ya tukio ambayo ni Alhamisi iliyopita (Machi 12), kijana mmoja ambaye hakuna aliyemfahamu alikuja hapa nyumbani na kumtaka mtu mmoja na kiroba ili akachukue ndizi ambazo kuna mtu aliagiza ziletwe. “Marehemu ndiye aliyekuwa karibu akijisomea baada ya kutoka shuleni. Mtu mkubwa aliyekuwa nyumbani muda huo ni bibi wa marehemu ambaye ni mtu mzima hivyo alimwambia Irene aongozane na mtu huyo akachukue mzigo akiju...

MADAI: AK47 ALIPIGWA KABLA YA KIFO CHAKE

Image
Mwili wa AK47 ukitolewa katika mochwari ya Hospitali ya Nsambya. WAKATI wapenzi wa muziki nchini Uganda wakiwa bado wamegubikwa na simanzi kwa kuondokewa na mwanamuziki wa miondoko ya dancehall, Emmanuel Mayanja maarufu kwa jina la AK47, taarifa mpya zimeibuka kuwa kuna uwezekano kuwa alipigwa kabla ya kifo chake. Jose Chameleon (katikati) akiwa na simanzi baada ya kuondokewa na mdogo wake. AK47 amefariki dunia   usiku wa kuamkia leo akiwa hospitali baada ya kuanguka akiwa bafuni. Taarifa hizo zinadai kuwa atakuwa alipigwa katika baa aliyokuwemo iitwayo Dejavu, iliyopo eneo la Kabalagala kabla ya kupelekwa Hospitali ya Nsambya, Kampala ambapo mauti yalimkuta. Baa hiyo inamilikiwa na Jeff Kiwanuka, aliyekuwa meneja wa wasanii wawili Radio na Weasel. Pallaso (mwenye tisheti ya bluu) ambaye naye ni kaka wa marehemu akifarijiwa na mwanamuziki Bebe Cool. Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kabalagala, Nusulah Kemig...

MWANAFUNZI ATEKWA, AUAWA

Image
Polisi wakiwa wamebeba mwili wa marehemu. DUNIA imekwisha jamani! Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Mabibo, Dar, Irene Said (15) ametekwa, amebakwa na kuuawa kikatili kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili huku ikidaiwa kuwa, kijana mmoja asiyejulikana alifika nyumbani kwao, Kigogo Luhanga na kutaka kiroba na mtu mmoja waongozane akabebe ndizi. Akizungumzia tukio hilo la kusikitisha sana, mama mdogo wa marehemu, Doto Lucas alisema: “Siku ya tukio ambayo ni Alhamisi iliyopita (Machi 12), kijana mmoja ambaye hakuna aliyemfahamu alikuja hapa nyumbani na kumtaka mtu mmoja na kiroba ili akachukue ndizi ambazo kuna mtu aliagiza ziletwe. “Marehemu ndiye aliyekuwa karibu akijisomea baada ya kutoka shuleni. Mtu mkubwa aliyekuwa nyumbani muda huo ni bibi wa marehemu ambaye ni mtu mzima hivyo alimwambia Irene aongozane na mtu huyo akachukue mzigo akijua uko jirani kwa mujibu wa mtu huyo. “Baada ya muda, yule kijana alirud...

MAAJABU MAKUBWA DAR! MTOTO AZALIWA BILA UBONGO WA NYUMA!

Image
Mtoto anayedaiwa kuzaliwa bila ya ubongo wa nyuma(medulla oblongata).Na Haruni Sachawa NI maajabu! Mwanamke mmoja, Diana Dioniz mkazi wa Magomeni Makuti jijini Dar es Salaam, ameangua kilio cha kuomba msaada baada ya mtoto wake aliyezaliwa mwaka mmoja uliopita kugundulika kuwa hana ubongo wa nyuma (medulla oblongata), hali inayosababisha shingo kulegea na macho kutoona. Akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake, Diana alisema alipata ujauzito wa mtoto huyo na kujikuta akiwa na furaha kubwa, lakini baada ya kuzaliwa na kumpa jina la John, amejikuta akipata mateso makubwa, kwani kwa muda wote, shingo yake inakuwa imelegea na macho yake hayaoni. “Majirani walinishauri nimpeleke hospitali kwa uangalizi zaidi, nilipomfikisha Muhimbili nikaambiwa suala la mwanangu linapaswa kushughulikiwa na daktari bingwa wa magonjwa ya watoto wa Kitengo cha Moi,” alisema mwanamke huyo. Aliongeza kuwa, baada ya kupelekwa huko na kuchunguzwa ndipo ilipojulikana kuwa na matatizo hayo, ambay...