NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA GEREZA LA BANGWE AFANYA MAZUNGUMZO NA WATUMISHI WA WIZARA MKOANI KIGOMA
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(katikati), akiongozana na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kigoma, SACP Sabas Matolo(kushoto) na Mkuu wa Gereza la Bangwe,SSP Raphael Mwanyingile(kulia), alipofika kutembelea gereza hilo katika ziara ya kikazi mkoani Kigoma tarehe 31/3/2016. Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akisaini kitabu cha wageni katika Gereza la Bangwe mkoani Kigoma, ambapo baadae alisikiliza risala iliyohusu mambo mbalimbali, iliyoandaliwa na wafungwa na mahabusu walioko katika gereza hilo na kuahidi kushughulika changamoto zao. Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kigoma, SACP Sabas Matolo, akisoma taarifa ya hali ya magereza mkoani Kigoma mbele ya Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni.Naibu Waziri yuko mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi. Mmoja wa Askari Magereza mkoa wa Kigoma, akizungumza wakati wa kipindi cha maswali kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nda...