Posts

Showing posts from March 13, 2020

Breaking: Halima Mdee Akamatwa Tena Segerea

Image
MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kada wa hicho, Kilewo Mwanga,  wamekamatwa leo Ijumaa, Machi 13, 2020, katika Gereza Kuu la Segerea jijini Dar es Salaam, walipokwenda kumpokea Mwenyekiti wa chama hicho wa taifa, Freeman Mbowe, ambaye ameachiwa leo baada ya kulipa faini aliyohukumiwa yeye na wenzake tisa na Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, Jumanne wiki hii. Askari Magereza wametumia silaha za moto na kufyatua risasi hewani kuwatawanya wafuasi wa chama hicho waliokuwa nje ya gereza hilo kumsubiri Mbowe akiachiwa. Baadhi ya viongozi na wananchi kadhaa wamejeruhiwa, akiwemo dereva mmoja wa bodaboda ambaye inadaiwa amevunjika mguu.

Mmiliki Mabasi ya J4 Ahukumiwa Kifo kwa Kuwaua Wenzake

Image
MAHAKAMA Kuu Mwanza imemhukumu adhabu ya kifo mfanyabiashara wa kampuni ya mabasi ya J4, Jumanne Mahende (45) baada ya kumtia hatiani kwa makosa ya kuwaua watu wawili kwa kukusudia. Jumanne alikuwa akikabiliwa na kesi ya mauaji namba 131 ya mwaka 2015. Anadaiwa kuwa Julai 13, mwaka 2015, saa 4 usiku, aliwaua kwa risasi, Ali Mohamed, fundi ujenzi wa Igoma wilayani Nyamagana na Claude Sikalwanda wa Nyasaka, Ilemela, Mwanza. Kwa mujibu wa RPC Mwanza, Mkumbo alisema Saa 4 usiku Julai 13 mwaka 2015, mkurugenzi wa kampuni ya mabasi J4 Express akiwa anajiandaa kufunga ofisi yake, alikutana na watu wawili Ally Mohamed (35) na Claude Sikalwanda (35), ghafla ukaanza mzozo uliopelekea Mahende kuwapiga risasi na kufariki papo hapo. Kwa upande wa ushahidi, mke wa marehemu Ally Mohamed, Donatha Gabriel na Aziza Sikalwanda ambae ni dada wa marehemu Claude Sikalwanda waliiambia mahakama hiyo kuwa mnamo tarehe 13 Julai, 2015,  siku ya tukio la mauaji lilipotokea marehemu waliwaaga k...

Breaking News: Corona Yatua Kenya, Mmoja Athibitika

Image
TUKIO la kwanza la virusi vya Corona limethibitishwa nchini Kenya. Wizara ya afya imethibitisha tukio hilo kulingana na waziri wa afya Mutahi Kagwe. Akizungumza na vyombo vya habari waziri huyo amesema kwamba kisa hicho kilithibitishwa Alhamisi usiku. Amesema tukio hilo ni la kwanza kuripotiwa nchini Kenya tangu kuzuka kwa mlipuko huo mjini Wuhan nchini China. Kisa hicho ni cha raia wa Kenya aliyewasli humu nchini kutoka Marekani kupitia mji London nchini Uingereza tarehe 5 mwezi Machi 2020. Aligunduliwa kuwa na virusi hivyo katika maabara ya wizara ya afya nchini Kenya. Hata hivyo, waziri huyo amesema kwamba mgonjwa huyo ambaye ni mwanamke yuko katika hali njema na kwamba viwango vyake vya joto vimeshuka na kuwa vya kawaida. ”Tarahe 5 mwezi Machi, 2020,  aligunduliwa kuwa na virusi hivyo katika maabara ya serikali lakini sasa viwango vyake vya joto vimeshuka na kuwa vya kawaida ambapo anakula vizuri lakini hawezi kutolewa hadi virusi hivyo vitakapokwisha mwil...