NIMEKUWEKEA VICHEKESHO NILIVYOVISIKIA MTAANI: VUNJA MBAVU!
MWALIMU : Alex, simba akianza kukufukuza utafanya nini? Alex: Nitapanda juu ya mti. Mwalimu: Je, na simba naye akipanda juu ya mti? Alex: Nitakimbilia mtoni niogelee. Mwalimu: Je simba naye akikufuata mtoni? Alex: Mwalimu uko upande wangu au wa simba? Maana sikuelewi kabisa, kila ninavyojaribu kumkwepa simba we unamwelekeza niliko, kama hunipendi sema tu. Kama hukuwahi kupata mia darasani usijali, utapata ukiwa unachaji simu. Ukimpa ‘demu’ hela mzazi wake hata hamuulizi, mpe mimba uone, utatafutwa hadi ‘Google’. Kumbe bangi haina madhara… nimetoka kuvuta pafu moja nipo fresh kabisa bila tatizo..saivi nimekaa juu ya tv naangalia makochi. Dua zenu jamani nipo ugenini nimefumwa naongeza maji ya ugali nijitetee vipi? Nimepika ugali ya watu wawili nikakula ya mtu mmoja nikashiba alafu nikatoka nje nikabisha mlango kama mgeni, nikaingia na nikakula iyo ingine! Mwili haijengwi na mbao. Mnamkumbuka yule Subira aliyekuwa anavuta her...