Mwigizaji Aunt Ezekiel akiwa na mke wa Iyobo. DAR ES SALAAM: Yamekwisha! Baada ya kudumu ndani ya bifu kwa muda mrefu huku wakituhumiana uchawi, hatimaye mwigizaji Aunt Ezekiel na mzazi mwenzie na Moses Iyobo, Mwengi Ally wamekutana na kumaliza tofauti zao. Mapema mwaka jana, wawili hao waligombana kufuatia Iyobo ambaye ni dansa wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kummwaga Mwengi kisha kuanzisha uhusiano na Aunt ambapo uhusiano huo ulijibu na wakafanikiwa kupata mtoto. Aunt ndiye aliyeamua kufuta ‘kinyongo chao’ ambapo alisema hakuona sababu ya wao kuendeleza bifu lisilokuwa na msingi wowote na kuwa wao ni wazazi na watoto wao ni ndugu wa damu moja, alimshauri Iyobo awakutanishe, wamalize tofauti zao. Baada ya kukubaliana, Aunt na Mwengi walikutana katika Hoteli ya Girrafe iliyopo Mbezi Beach, jijini Dar wakiwa na Iyobo ambaye alisimamia zoezi zima la mapatano kwa wawili hao kuzungumza, wakaelewana, ‘wakazika’ tofa...