Posts

Showing posts from April 21, 2017

Sakata la Lugumi bado halijachacha

Image
Dar es Salaam. Sakata la mkataba baina ya Kampuni ya Lugumi Enterprises na Jeshi la Polisi, halijafa; ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imeliibua ikionyesha madoa lukuki. Sakata hilo lilikuwa kama limezikwa baada ya kamati iliyoundwa na Bunge kulichunguza na baadaye kukabidhi ripoti ofisi ya Spika ambayo ilisema ingeishauri Serikali cha kufanya. Juni 30 mwaka jana, Naibu Spika Tulia Ackson alilieleza Bunge kuwa ametumia kanuni ya 117(17) kuikabidhi Serikali matokeo ya uhakiki uliofanywa na kamati ndogo iliyoundwa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC). Alisema matokeo ya ripoti hiyo yana maoni, ushauri, mapendekezo ya namna ya kutatua changamoto zilizoainishwa na taarifa ya kamati ya PAC na hivyo kuzuia wabunge kujadili suala hilo. Lakini, ripoti ya CAG iliyotolewa wiki iliyopita imeibua upya sakata hilo, ambalo linahusu utekelezwaji mbovu wa mkataba wa uwekaji mashine za kielektroniki za kuchukua alama za ...

NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA NI MADRID NA MADRID, MONACO NA JUVENTUS

Image
Droo ya Nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa imekamilika na Real Madrid atakutana na Atletico Madrid katika mechi ya kwanza ya hatua hiyo.Nusu fainali ya pili, itakuwa ni AS Monaco dhidi ya Juventus mechi ya kwanza ikipigwa nchini Ufaransa.

STAA OMMY DIMPOZ AFUNGUKA HAYA KUHUSU KUPOTEZWA KWENYE MUZIKI

Image
MWANAMUZIKI Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ ametoa povu kufuatia madai kuwa, hivi sasa  kapotezwa na vijana wadogo wanaolazimisha ‘kuvaa viatu vyake’. Akipiga stori na Showbiz, Dimpoz alisema hajapotea kwenye gemu kama mashabiki wanavyomchana mitandaoni na kwamba ukimya wake wa muda unatokana na yeye kujipanga katika kuandaa kazi mpya ili iweze kufanya vizuri atakapoiachia. “Siyo kweli kuwa nimepotea, kwanza najiandaa kuachia kazi mpya ambayo ina ubora wa hali ya juu, wanaosema nimepotea wasubiri waone maajabu yangu,” alisema Dimpoz.
Image
WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO, DK. HARRISON MWAKYEMBE. WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amesema yuko tayari kuuachia uwaziri ili aweze kulithibitishia Bunge kuwa aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowassa alihusika katika kashfa ya Richmond. Dk. Mwakyembe alitoa kauli hiyo jana bungeni baada ya Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari na Mbunge wa Ubunge Ubungo (Chadema) Said Kubenea kumtuhumu juzi kuwa hakutenda haki mwaka 2008 wakati alipoongoza Kamati Teule ya Bunge kuchunguza kampuni tata ya ufuaji umeme ya Richmond bila kumhoji Lowassa ambaye alituhumiwa. Nassari juzi wakati akichangia bajeti ya Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) alisema Dk. Mwakyembe ameikataa ripoti iliyomchunguza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuvamia kituo cha televisheni cha Clouds kwa madai kuwa haikumhoji mkuu huyo wa mkoa ili hali yeye aliendesha Kamati ya Teule ya Bunge ya Richimond na kum...

RAIS DKT MAGUFULI APOKEA UJUMBE TOKA KWA RAIS KAGAME WA RWANDA IKULU DAR ES SALAAM LEO

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Dkt. Musafiri Papias, Waziri wa Elimu wa Rwanda na Mjumbe maalumu wa Rais Paul Kagame alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Aprili 20, 2017   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Dkt. Musafiri Papias, Waziri wa Elimu wa Rwanda na Mjumbe maalumu wa Rais Paul Kagame alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Aprili 20, 2017   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Dkt. Musafiri Papias, Waziri wa Elimu wa Rwanda na Mjumbe maalumu wa Rais Paul Kagame alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Aprili 20, 2017. Wengine ni Balozi wa Rwanda nchini Mhe. Eugene Kayihura na Afisa Mwandamizi wa Ubalozi Bw. Issa Mugabutsinze.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea ujumbe maalumu kutoka kwa Rais Paul Kagame wa Rwan...

Banda sasa huru kuitumikia Simba

Image
BEKI WA SIMBA, ABDI BANDA. BEKI wa Simba, Abdi Banda, yuko huru kuendelea kuitumikia timu yake katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara inayoelekea ukiongoni imefahamika. Uamuzi wa Banda kurejea uwanjani umetolewa na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambayo imetangaza kumfungia beki huyo mechi mbili kutokana na kosa lake la kumpiga ngumi, kiungo wa Kagera Sugar, George Kavilla katika mechi iliyowakutanisha iliyofanyika Aprili 2, mwaka huu kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Taarifa kutoka kwenye kikao hicho ambacho Banda aliitwa kuhojiwa kilieleza kuwa adhabu ya beki huyo ni kutocheza mechi mbili. Awali beki huyo wa Timu ya Soka ya Taifa (Taifa Stars) alisimamishwa kwa muda usiojulikana na Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi Tanzania maarufu Kamati ya Saa 72. Hatua hiyo ilimfanya beki huyo ashindwe kuitumikia timu yake katika mechi mbili za Ligi Kuu Bara zilizopita ambazo Simba iliikabili Mbao FC na kupata ushindi wa mabao...

Watumishi 2,000 Elimu wapandishwa vyeo

Image
WAZIRI WA ELIMU, PROFESA JOYCE NDALICHAKO. BUNGE limeelezwa kuwa Jumla ya watumishi 2,272 walipandishwa vyeo katika Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi katika kipindi cha 2015/16 huku miongoni mwao 71 walitoka Chuo cha Ualimu Korogwe. Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Stella Manyanya, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Korogwe Mjini, Mary Chatanda (CCM), aliyetaka kujua serikali ina mpango gani wa kuwapandisha daraja wale waliostahili na kuwa lini itawalipa madai yao ya fedha za likizo ambazo watumishi hawajalipwa kwa muda mrefu na wamekuwa wakishindwa kuzipata kwa wakati. Akijibu swali hilo, Naibu Waziri huyo alibainisha serikali inaendelea kulipa madeni, ikiwamo fedha za likizo kwa walimu au watumishi katika sekta ya Elimu, ambapo katika kipindi cha mwaka wa fedha 2015/16 hadi Juni 2016, jumla ya Sh. Bilioni  22.7 zililipwa kwa walimu 63,814. Aidha, alisema katika kipindi cha mwaka 2016/17 hadi Machi 2...

MCHUNGAJI MREMBO NA MWENYE MVUTO WAKUPAGAWISHA WANAUME HAFANYIWA HILI NA WANAJESHI HAWA

Image
After Nairobi Senator Mike Sonko took to social media and disclosed that he enjoyed sermons from youthful female pastor, Lucy Natasha, she became an instant hit amongst Kenyans. Many adored the youthful pastor for her immense beauty and good sense of fashion that consists of designer clothes and expensive jewellery. And it now seems that Kenyans will keep talking about this s3xy preacher whose beauty is simply irresistible. She recently rocked a red dress during her birth-day and the out-come was just amazing. Check out the photos below.

MAHAKAMA YATOA AMRI YA MSANII AGNES MASOGANGE AKAMATWE

Image
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa hati ya kumkamata msanii, Agnes Gerald maarufu kama Masogange kwa kushindwa kuhudhuria kwenye kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili. Hati hiyo ilitolewa jana mbele ya Hakimu Mkazi mkuu, Wilbroad Mashauri, wakati kesi hiyo ilipotajwa.Wakili wa Serikali, Adolf Mkini alidai mahakamani hapo kwamba upelelezi wa kesi hiyo upo hatua za mwisho, lakini mshtakiwa, wadhamini wake na wakili wake hawakufika hivyo wakili Nkini akaomba mahakama itoe hati ya kumkamata mshtakiwa huyo kwa sababu ni mara ya pili ameshindwa kufika mahakamani hapo.Hakimu Mashauri alikubali maombi ya wakili wa Serikali na kutoa hati ya kumkamata mshtakiwa ambaye ni Masogange.Msanii huyo aliwahi kuonywa akitakiwa aheshimu mahakama kutokana na kutokuwapo kwenye kesi yake ilipotajwa. Katika kesi hiyo namba 77 ya mwaka 2017, Masogange anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14 mwaka huu, katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam, alitumia daw...