Posts

Showing posts from October 6, 2013

Mlimani City yaanza KUWASACHI watu wanaoingia ndani baada ya taarifa kuzagaa kwamba lile GAIDI la kike liko Dar limejificha

Image
phars Katika hali tofauti waliyokutana nayo wanunuzi wa bidhaa kutoka kwenye maduka mbalimbali yaliyopo kwenye mall ya Mlimani city, wengi wameona ni hatua nzuri baada ya kuongeza usalama wa watu wanaotumia jengo hilo hasa kutokana na mambo yaliyotokea huko Kenya. Tofauti na jana, leo hii jumapili 6/10, wateja wote waliokuwa wanaingia kwenye mall hiyo walikuwa wanasachiwa na mashine maalum pamoja na mabegi yao. Mdau wetu alifika kwenye mall hiyo kwa manunuzi ya kawaida na alikuta askari wanaohusika na ulizi wakiwa wametengenisha njia mbili, moja ya kutoka na nyingine ya kuingia kwenye kila mlango wa kuigia kwenye mall. Askari wawili mmoja wa kike kwa ajili ya wateja wa kike na mwingine wa kiume pamoja na askari wa tatu kwa ajili ya kusachi mabegi. Baadhi ya watu walionekana kufurahia hatua hiyo ambapo siku kadhaa zilizopita, watu wengi walianza kujiuliza maswali juu ya usalama wa watu wanaongia kwenye mall hiyo kwa ajili ya manunuzi yao ya kila siku.

Msanii Diamond azungumzia kuhusu kifo chake katika ngoma yake mpya...Wadau wake watabiri Siku zake za mwisho

Image
Diamond ametumia melody inayofanana kidogo na wimbo wake “Kesho” kutengeneza wimbo huu. Ni wimbo ambao umevuta hisia tofauti miongoni mwa mashabiki wake hasa wale wanaoamini kwamba mafanikio yake yanatokana na nguvu za pembeni ( freemason ) .. Wapo wanaojaribu kutabiri siku za mwisho za msanii huyu kwa kulinganisha na kifa cha utata cha msanii Kanumba ambaye naye alitoa wimbo kama huu pamoja na filamu ya kifo chake siku chache kabla ya mauti kumkuta... Haya ni baadhi ya mashairi ya wimbo huo: Vipi Maneke atanililia...?? Je wasanii wenzangu wataniimbia..?? Ama litafutika jina langu...?? Na nyimbo zangu hawatasikia..?? Vipi wasafi watanililia....?? Je ndugu rafiki watahudhuria..?? Ama nitakapokufa Sina changu..?? Hata mama yangu watamkimbia...??

wanafunzi takriban 50 wanusurika katika ajali jijini dar es salaam jana jioni

Image
Askari wa usalama barabarani wakijipanga kutoa huduma baada ya basi la daladala lililokuwa limebeba wanafunzi takriban 50 wa shule ya msingi ya Mgulani kugongana na gari dogo aina ya RAV 4 na kupinduka katika makutano ya Kenyatta Avenue na Barabara ya Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es salaam jana jioni. Dereva wa gari dogo akiwa na mtoto wa umri wa takriban miaka mitatu walijeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitali. Wanafunzi wote walinusurika. Uharibifu wa miundumbinu baada ya ajali hiyo Askari wa usalama barabarani wakiondoa mabegi ya wanafunzi hao ambao walitafutiwa basi lingine kuwapeleka hospitali kwa uchunguzi zaidi Wanafunzi wakiwa katika gari walilotafutiwa baada ya ajali hiyo Magari ya break-down yakifanya juhudi ya kunyanyua basi hilo Baadhi ya wanafunzi hao baada ya ajali. Ishukuriwe hakuna aliyeumia   KAMA UMEGUSWA TOA POLE KWA KUSEMA "AMEN " KISHA LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK

Irene Uwoya apewa matusi ya nguoni baada ya kuweka picha ya mtoto wake AKINYWA BIA

Image
Picha aliyoipost mtandaoni Staa wa filamu za Kibongo,Irene Uwoya ikimuonyesha mtoto wake Krish Ndikumana akiwa ameshika glasi ya pombe imemfanya msanii huyo atukanwe baada ya mashabiki wake kutoa maoni kwamba hapaswi kufanya hivyo kama mzazi na kioo cha jamii kwani anamfundisha tabia mbaya mtoto wake . Irene amepost picha hiyo akiwa Jijini Arusha katika hoteli ya Mount Meru na msanii mwenzake Blandina Chagula‘Johari’wakila bata . Watu hao walimwambia Uwoya kuwa siyo malezi mazuri hata kama ameshika au kunywa kabisa .....anatakiwa kuwa mama wa mfano kwa tabia njema kwa mtoto. …cio malezi ata kama ameshika au kunywa kabisa. b a good mother. Alicomment shabiki mmoja

Rais Kikwete na Tundu Lissu wavaana...Tundu Lissu aiponda hotuba yake ya "NIMEAMBIWA"...Kikwete adai Lissu ni MNAFIKI

Image
SIKU moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kukasirishwa na kauli ya Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) Tundu Lissu, kuwa Rais hakuheshimu mapendekezo ya TEC, CCT na walemavu huku akisema kwamba maneno ya Mbunge huyo niya uzushi na uongo mtupu, nanin ya unafiki, fitina na uzandiki wa hali ya juu. Mbunge huyo ameibuka na kumjibu Rais Kikwete. Nanukuu sehemu fupi ya hotuba ya Rais: "Siyo tu kauli hiyo ya Mheshimiwa Tundu Lissu ni uzushi na uongo mtupu bali pia ni ya unafiki, fitina na uzandiki wa hali ya juu. "Nasema hivyo kwa sababu, sipendi kuamini kuwa Mheshimiwa Mbunge amesema yale kwa kutokufahamu ukweli au kwa bahati mbaya. "Amesema yale kwa makusudi mazima ya kupotosha ukweli ili pengine isaidie kujenga hoja yake ya kutaka Rais asiteue wale Wajumbe 166 wa Bunge Maalum" Rais Kikwete alisema hayo wakati akihutubia Taifa, kama ilivyo kawaida yake kila mwisho wa mwezi.Katika hotuba yake, JK alisema suala la Mchakato wa mabadiliko ya Kati...

Tahadhari: Yule gaidi wa kike aliyevamia Kenya anadaiwa kujificha jijini Dar es Salam

Image
MWANAMKE wa nchini Uingereza, Samantha Lewthwaite, anayetuhumiwa kuhusika katika shambulio la kigaidi nchini Kenya hivi karibuni, anadaiwa kujificha hapa nchini, RAI Jumapili linaripoti. Taarifa za Samantha kujificha nchini zimeripotiwa kwa mara ya kwanza jana na gazeti moja kubwa linaloheshimika nchini Uingereza la Daily Mail. Daily Mail katika taarifa yake hiyo limeandika kuwa Samantha, ambaye kwa sasa anasakwa na vyombo vya ulinzi na usalama duniani kote, huenda akawa amejificha Tanzania au Somalia, baada ya shambulizi la Westgate Mall. Taarifa hiyo ya Daily Mail imekuja ikiwa ni siku chache tu kupita tangu gazeti moja la hapa nchini (Siyo RAI) kuchapisha habari ya uvumi wa mwanamke aliyesadikiwa kuwa ni Samantha kuonekana katika viunga vya Jiji la Dar es Salaam. Katika habari hiyo ambayo ilithibitishwa na polisi, ni kwamba mwanamke huyo, ambaye ni mzungu aliyefananishwa na Samantha, alifika katika benki ya Exim tawi la Tower jijini Dar es Salaam kwa lengo la k...

Shilole ataja sababu zinazomfanya acheze NUSU UCHI jukwaani na kukubali kunyonywa maziwa yake

Image
Msanii wa filamu na muziki nchini, Shilole amefunguka kwa kusema anafanya muziki wa kucheza na wanaume jukwaani ili kukidhi mahitaji ya aina ya burudani wanayoihitaji watu wake. Akizungumza na Bongo5 leo akiwa Moshi, Shilole amesema anafanya muziki kulingana na mahitaji ya mashabiki wake na si kwa kusikiliza mawazo ya mtu mmoja mmoja yasiyokuwa na manufaa kwenye muziki wake. “Nafanya muziki anaofanya Shilole peke yake,na wapenzi wengi wa muziki wangu wanafurahishwa na kitendo cha kuwapandisha vijana na kucheza nao, hii inaleta mzuka kwangu na kwa wapenzi wa burudani,” amesema. “Ninavyowapandisha vijana na kucheza nao huku wamenishika au tumeshikana ndio wanaona hatari? Mbona ni mambo ambayo yanafanyika kwenye show mbalimbali, pia ili kuleta uhalisia wa show ni lazima mshikane kidogo,kwa wale ambao wanaona kama naharibu ni washamba tu.”

Picha za Serengeti fiesta 2013 ndani ya uwanja wa majengo mjini moshi

Image
Msanii mkongwe katika anga ya muziki wa kizazi kipya,Dully Sykes akiwaimbisha mashabiki wake kibao waliofurika vilivyo ndani ya uwanja wa Majengo mjini Moshi Kundi la Weusi likiongozwa na Joe Makini wakilishambulia jukwaa kwenye tamasha la serengeti fiesta uwanja wa Majengo mjini Moshi. Mwanadada aliyewahi kufanya vyema kwenye shindano la BSS,Menina akiimba kwa hisia jukwaani Mkali mwingine wa bongofleva anaefanya vyema kwenye muziki huo,akitambulika kwa jina la kisanii Ney wa Mitego akiwaimbisha mashabiki wake kwenye wakati wa tamasha la serengeti fiesta. Mwanadada Linah akimpagawisha shabiki wake vilivyo jukwaani ndani ya tamasha la serengeti fiesta 2013,kwenye uwanja wa Majengo mjini Moshi. Mkali wa shindano la BSS,Walter Chilambo akiimba kwa hisia jukwaani kwenye tamasha la serengeti fiesta ndani ya uwanja wa Majengo mjini Moshi. Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye amekuwa akifanya vyema tangu aibuliwe na Serenge...