TAREHE 13.06.2017 MAJIRA YA SAA 01:00HRS USIKU KATIKA KIJIJI CHA KISABO KATA YA BUJASHI TARAFA YA SANJO WILAYA YA MAGU MKOA WA MWANZA, NUNGHU MGETA, MIAKA 35, MSUKUMA, MKAZI WA KIJIJI CHA KISABO, ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA MAUAJI DHIDI YA MTOTO WAKE AITWAYE MISUNGWI NUNGHU MIAKA 06, MTOTO WA KIUME, AMBAPO INADAIWA KUWA ALIMUUA KWA KUMZIBA MDOMO NA PUA KWA MUDA MREFU HALI ILIYOPELEKEA MTOTO KUSHINDWA KUPUMUA NA BADAE KKUPOTEZA MAISHA, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI. INADAIWA KUWA MTUHUMIWA ALIKUWA AKIISHI NA WATOTO WAKE MWENYEWE HAPO NYUMBANI KWAKE, KWANI TAYARI ALIKUWA AMETENGANA NA MKEWE KWA MUDA MREFU. INADAIWA KUWA BAADA YA MTUHUMIWA KUTELEKEZA MAUAJI HAYO ALIMCHUKUA MAREHEMU KISHA KWENDA KUMTUPA KWENYE DIMBWI LA MAJI LILILOPO MBALI NA NYUMBA YAKE ILI IONEKANE AMEKUFA MAJI. ASUBUHI WAKATI WANANCHI WANAPITA MAENEO HAYO NA KUONA MWILI WA MTOTO ALIYEPOTEZA MAISHA UKIELEA KWENYE MAJI WALIPATA MASHAKA KISHA WALITOA TAARIFA KWENYE KI...