MAKUBWA YAFUCHUKA HOUSIGELI ALIYETESWA KWA MIAKA 3 KWA KUCHOMWA NA PASI NA BOSI WAKE
NYUMAya pazia! Yule msichana Yusta Lucas (20) mwenyeji wa Mkoa wa Tabora ambaye alifika jijini Dar kufanya kazi ya u-hausigeli na kufanyiwa ukatili wa kutisha na bosi wake kisha habari zake kuandikwa, ametoa siri nzito, Uwazi limemegewa.Yusta Lucas akionyesha majeraha ya meno aliyong'atwa na bosi yake . Akizungumza kwa uchungu na gazeti hili akiwa wodini kwenye Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu Kino ndoni, Mwananyamala jijini Dar, Yusta ambaye amefanya kazi kwa tajiri yake huyo kwa miaka mitatu alisema: “Kwanza nataka watu wajue kuwa mwajiri wangu ni binamu yangu, alinileta hapa Dar kwa ajili ya kumsaidia kazi za ndani pamoja na kumlelea mwanaye. “Kipigo hasa kilianza mwanzoni mwa mwaka huu ikiwa ni pamoja na kuning’ata kwa meno mwili mzima, ndiyo maana mwili wangu wote unaonekana una mabakamabaka. “Mateso yangu majirani walikuwa wakiyajua kutokana na kilio changu lakini walikuwa wanashindwa kunisaidia kwa sababu ya ushirikiano mdogo. “Kwanza nashangaa ...