Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Matawi ya Yanga Dar es Salaam, Boas Ikupilika, Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji amewaahidi kuisuka Yanga mpya kwenye dirisha dogo la Novemba. Manji pia ameahidi kumpa sapoti kubwa Kocha Mwinyi ZaĀhera kuhakikisha sifa ya Yanga inarejea kwani amewakubali wachezaji baada ya kuwaona kwenye Uwanja wa Taifa hivi kaĀribuni alipokwenda kuwaangalia. Usajili wa dirisha dogo umepangwa kuanzia Novemba 15 hadi Desemba 15, mwaka huu ambapo timu hupata nafasi ya kuongeza wachezaji wachĀache kulingana na upungufu wao. Ikupilika amethibitisha kuwa Manji amekuwa akihusika katika mambo mbalimbali ndani ya klabu, amemuahidi Zahera kuwa, atamsaidia kutimiza maĀhitaji yake kwa kufanya usajili wa wachezaji ambao atahitaji kwenye dirisha dogo. āManji aliomba muda kidogo kabla ya kurejea rasmi wakati wowote, lakini kuna baadhi ya majukumu ambayo amekuwa akĀitekeleza kama kiongozi wetu. Amekuwa akishauri mambo mengi kuhusu timu yetu,ā alidokeza kionĀgo...