MKE AMFUMANIA MUMEWE GUEST BUBU JIONEE MWENYEWE.
USIOMBE yakukute! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya kusikia kisa cha aliyewahi kuwa mpenzi wa mwanamuziki wa TAKEU, Nice Lucas Mkenda , Lulu John (mwenye blauzi nyekundu) anayedai kumfumania mumewe , Lulu alidai kumfumania bwana’ke Abdulatif Salum na mwanamke ambaye jina halikupatika kwenye gesti moja iliyopo Kinondoni B jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita. SINEMA ILIKUWA HIVI Kwa mujibu wa Lulu, akiwa kwenye mihangahiko ya kusaka bingo, alitonywa na mtu wake wa karibu kuwa mumewe Abdulatif yupo kwenye nyumba hiyo ya wageni akiigagadua amri ya sita nje ya mkataba. Lulu, baada ya kuthibitishiwa kuwa mumewe anacheza ‘nje kapu’ ndipo akakodi bodaboda fasta na kuwahi eneo la tukio kwani naye siyo mgeni wa uwanja huo wa mechi za kitandani. Alidai kuwa ilimchukua dakika 12 tu kutoka Kijitonyama, Dar anakoishi na mumewe hadi eneo la tukio. MPAKA CHUMBANI Aliendelea kusema kuwa baada ya kutimba mahali hapo alikwenda moja kwa zote hadi ...