Posts

Showing posts from August 9, 2018

WASANII WAJITOKEZA KUMUAGA MZEE MAJUTO

Image
Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul maarufu kama Diamond Platnumz (mwenye kanzu nyeupe) akibeba jeneza la mwili wa aliyekuwa nguli wa filamu za uchekeshaji nchini, Amri Athumani ‘King Majuto’ baada ya kumalizika kwa shughuli ya kuuaga mwili wake iliyofanyika leo tarehe 9 Agosti, 2018 kwenye viwanja vya Karim Jee vilivyoko jijini Dar es Salaam. Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul maarufu kama Diamond Platnumz akibeba jeneza la mwili wa aliyekuwa nguli wa filamu za uchekeshaji nchini, Amri Athumani ‘King Majuto’. Msanii wa Bongo Movie, Jacob Steven ‘JB’ akizungumza na wanahabari wakati wa shughuli ya kuuaga mwili wa marehemu Mzee Majuto.  Msanii wa Bongo Movie, Single Mtambalike (wa kulia) akizungumza na msanii mwenzake, Mzee Hashim Kambi (wa kushoto).

Rich Mavoko Ashinda Kesi Dhidi ya WCB

Image
EXCLUSIVE: Msanii Rich Mavoko ameshinda kesi ya kujiengua katika Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB). Kesi hiyo ilikuwa ikisikilizwa katika Ofisi za Baraza la Sanaa Tanzania ( Basata). Takribani miezi miwili iliyopita taarifa zilianza kusambaa kuwa Mavoko ametimuliwa WCB huku nyingine zikieleza kuwa amejiengua mwenyewe. Aidha, viongozi wa lebo hiyo hawajataka kuweka bayana kinachoendelea dhidi ya Mavoko ambapo hivi karibuni, Mmoja wa viongozi hao, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ hivi karibuni alikaririwa akisema wakati wa kuzungumzia jambo hilo haujawadia.