Posts

Showing posts from June 2, 2016

Rich Mavoko Asajiliwa Rasmi Lebo ya WCB

Image
Msanii wa Bongo fleva, Rich Mavoko (kushoto)  akisaini Mkataba wa kujiunga na lebo ya muziki ya Wasafi Classic Baby (WCB) iliyopo chini ya staa wa tasnia hiyo, Diamond Platnumz (kulia). Diamond (kushoto) akipongezana na Rich Mavoko mara baada ya kusaini mkataba huo. Habari ikufikie popote ulipo wewe mpenda burudani na mdau wa muziki wa bongo fleva kuwa, leo June 2, 2016 lebo ya muziki ya Wasafi Classic Baby (WCB) inayomilikiwa na staa wa tasnia hiyo Diamond Platnumz inaingia kwenye headlines za Bongo Fleva baada ya kumtambulisha rasmi  msanii  wao mpya  Rich Mavoko ambaye anakuwa ni msanii wa nne atakayesimamiwa kazi zake katika lebo ya WCB. Kwa mujibu wa CEO wa lebo ya WCB, Diamond Platnumz amesema… ’ Kwasasa Label yangu inakuwa na jumla ya wasanii nne ukiachana na Rich Mavoko kuna Dada yangu Queen Darling ambaye sijawahi kumtambulisha lakini anakuwa ni msichana wa kwanza katika label yangu kwahiyo tutakuwa na jumla ya wasanii nne Raymond, H...

AHADI YA RAIS MAGUFULI KWA WAFANYABIASHARA WAKUBWA YAANZA KUTIMIA

Image
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (kushoto) akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi, Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi wakati wa hafla ya utoaji Tuzo za Rais kwa Wazalishaji Bora wa Viwanda  (PMAYA) iliyoandaliwa na Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) jijini Dar es Salaam jana. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya wageni waalikwa wakati wa hafla ya utoaji Tuzo za Rais kwa Wazalishaji Bora wa Viwanda 2015 (PMAYA) iliyoandaliwa na Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) jijini Dar es Salaam jana. Na Mwandishi wetu Nia serikali ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kuanza kushirikiana na wafanyabiashara wakubwa nchini ili kuweza kufanya kazi kwa pamoja na kusaidia kuinua uchumi wa nchi lakini pia kutoa ajira kwa watanzania katika viwanda vinavyoilikiwa na matajiri hao. Hilo limenza kuonekana siku moja baada ya Rais Magufuli kuweka wazi nia yake hiyo am...

NAIBU WAZIRI MASAUNI ATEMBELEA MSITU WA MAPANGOPORI YA AMBONI

Image
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiwa na vikosi vya ulinzi na usalama vinavyotoa ulinzi katika msitu wa Mapangopori ya Amboni mkoani Tanga. Naibu Waziri alifanya ziara ya kutembelea mapango hayo ambayo yalikuwa makazi ya watu wanaohofiwa majambazi waliofanya mauaji katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, Tarafa ya Chumbageni, jijini Tanga. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi Maalum kutoka Kikosi cha Kutuliza Ghasia Makao Makuu Dar es Salaam, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, William Mwampagale.   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akichungulia pango lililopo katika msitu wa Mapangopori ya Amboni linalodaiwa kuwa ni njia kuu ya watu wanaohofiwa majambazi waliofanya mauaji katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, Tarafa ya Chumbageni, jijini Tanga.   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akitoa maelekezo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard...