Messi ataweza Kujibu mabao HAT-TRICK za Ronaldo leo dimbani?
Cristiano Ronaldo jana alifanikiwa kufunga mabao matatu pekee 'Hat-trick' katika mchezo wake wa kwanza wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu dhidi ya Spain nchini Urusi. Mabao hayo yaliisaidia Ureno kwenda sare ya 3-3 dhidi ya mabingwa hao wa Kombe la Dunia kwa mwaka 2010 huko Afrika Kusini. Hattrick hiyo imekuwa ya 51 kwa Ronaldo katika soka la ushindani huku akiifunga akiwa na umri wa miaka 33, moja ya wachezaji wenye umri mkubwa katika mashindano hayo. Rekodi hizo kadhaa za Ronaldo zinamfanya Messi ambaye hajawahi kutwaa ubingwa wa taji hilo kujipanga kwa ajili ya kulipiza mapigo. Mara nyingi wawili hawa wakiwa viwanjani wamekuwa ni watu wa kuvunja na kuandika rekodi za aina yake na kipekee. Messi atakuwa anashuka dimbani kuingoza Argentina kucheza kibarua chake cha kwanza leo dhidi ya Iceland. Pengine anaweza akajibu kwa kufunga pia mabao kama aliyofunga mpinzani wake ingawa huu ni mchezo wa soka mambo yanaweza kuwa tofauti. Tusubiri tuone n...