Posts

Showing posts from January 27, 2018

Man U Waitwanga Yeovil 4-0, Sanchez Aibuka Man Of The Match

Image
KLABU ya Soka ya Manchester United imeenedeleza ushindi kwa michezo mitatu mfurulizo tangu itoke mapumzikoni, Dubai ambpo usiku wa kuamkia leo imeitwanga timu ya Yeovil bao 4-0 katika michuano ya Kombe la Shirikisho (FA Cup). Katika game hiyo mchezaji mpya wa Man U aliyesajiliwa hivi majuzi akitokea Arsenal, Alex Sanchez ikiwa ni mechi yake ya kwanza alionyesha uwezo mkubwa huku akiisaidia timu yake hiyo kuibuka na ushindi mnono katika Mji wa Yeovil. Wenyeji Yeovil walianza vizuri lakini walifanya makosa yaliyopelekea kuadhibiwa na klabu hiyo tajiri zaidi duniani kwa sasa. Wafungaji ni; Rashford 40, Ander Herrera 61, Lingard 90, Lukaku 90+3. Yeovil: Krysiak, James, Sowunmi, Nathan Smith, Dickson, Green, Wing, Bird, Gray, Zoko, Surridge. Subs:  Connor Smith, Browne, Maddison, Gobern, Whelan, Santos, Fisher. Man Utd:  Romero, Darmian, Lindelof, Rojo, Shaw, Ander Herrera, Carrick, McTominay, Mata, Rashford, Sanchez. Subs: ...

DC aamuru mkandarasi akamatwe

Image
Mkuu wa Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, John Palingo ameamuru kuwekwa mahabusu mkandarasi wa umeme kutoka Kampuni ya Cyber, Benjamin John baada ya kutuhumiwa kuchukua fedha kwa wananchi kwa madai ya kuwaunganishia umeme wa Wakala wa Nishati Vijijini (Rea) katika vijiji ambavyo havipo kwenye mpango huo. Palingo alitoa amri hiyo jana kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mbozi baada ya baadhi ya madiwani kudai kampuni hiyo imekuwa ikiwatoza baadhi ya wananchi Sh20,000 hadi 140,000 kwa ajili ya fomu na usajili wa mteja kuunganishiwa umeme. Kutokana na malalamiko hayo Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Erick Ambakisye alilazimika kuuita uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Songwe na mwakilishi wa Kampuni ya Cyber kutoa ufafanuzi mbele ya baraza hilo. Hata hivyo, Mkandarasi na mwakilishi wa Kampuni ya Cyber, Benjamini John alipotakiwa kutoa ufafanuzi alikanusha madai hayo akieleza kwamba iwapo itathibitika kuwa kampuni yake imehusika, fe...

Trump Uso kwa Uso na Rais Kagame, Atuma Salamu Afrika

Image
Rais Trump (kushoto) akisalimiana na Rais Kagame. RAIS wa Marekani, Donald Trump amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Rwanda Paul Kagame ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na kumuomba afikishe salamu zake za upenzo kwa viongozi wengine wa mataifa wanachama wa AU. Viongozi hao wawili wamekutana mjini Davos, Uswizi baada ya Mkutano wa Viongozi na Watu Mashuhuri Kuhusu Uchumi na Biashara Duniani. Mkutano huo wa Kagame na Trump umekuja wiki chache baada ya kiongozi huyo wa Marekani kutoa kauli iliyotafsiliwa kama ni kuyakashifu mataifa ya Afrika. Kutoka kusoto ni mama Jeannette Nyiramongi Kagame, Rais Kagame, Rais Trump na Melania Trump. Hatua hiyo ilimfanya kushutumiwa vikali na viongozi wa AU na baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika kama vile Botswana na Ghana ambapo  amekanusha kwamba alitumia neno hilo kuyakashifu mataifa ya Afrika huku aki kiri kutumia maneno makali akiyaeleza mataifa ya Afrika, Haiti na El Salvador alipokuwa anazungumz...