Posts

Showing posts from December 12, 2016

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM JIJINI DAR ES SALAAM

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) ambaye ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kabla ya kuanza kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Alichokisema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kwenye Sherehe za Maulid, Singida

Image
Katika kusherekea siku ya Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammed (S.A.W), Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali itaendelea kuwatumikia Watanzania wote bila kujali imani zao za kidini. Majaliwa ameyasema hayo katika sherehe za kitaifa za Maulid ambazo zimefanyika mkoani Singida na kusema kuwa kuna matukio ambayo yamekuwa yakijitokeza katika jamii na katika kuyachukulia hatua za kisheria vitendo hivyo Serikali haitakuwa ikibagua mtu kutokana na imani yake ya kidini kama jinsi inavyofanya kwa shughuli za maendeleo. “Serikali inawashukuru sana kwa kuendelea kuunga mkono jitihada ya Serikali ya Rais Magufuli, tunaamini juhudi tunazofanya za kuweka nidhamu kwa watumishi wa umma na taasisi binafsi mtaendelea kutuunga mkono, tutaendelea kuruhusu uhuru wa kuabudu na kushirikiana na viongozi wa dini lakini tu mafundisho yanayotolewa yasikiuke sheria na kanuni za nchi, “Serikali ipo macho kupambana na tukio lolote lenye nia ya kupoteza amani ya ...

Mzee wa Upako: Wote Walionichafua Watakufa Mwakani, Wasipokufa Nitaanza Kuuza Gongo

Image
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo, maarufu kwa jina la Mzee wa Upako jana amesema waandishi wote wa habari wanaoandika habari za kumchafua, watakufa kabla ya kufika Machi 2017. Kauli hiyo ameitoa ikiwa ni mwendelezo wa mahubiri yake ya nne katika wiki ya tatu mfululizo, akijibu yale yaliyoandikwa katika vyombo vya habari kuhusu kumfanyia fujo jirani yake na kulewa. “Kila mwandishi aliyeniandika vibaya, ikifika mwezi wa tatu akiwa hai, mimi naacha kuhubiri, nafunga virago nakwenda kuuza gongo, sasa Mungu ndiye ataamua kwamba ama niache kuhubiri mimi au wewe ufe …najua hata leo mko humu mmekuja na mnasikiliza tu,” alisema. “Akisema Mungu uishi wewe basi, nakuwa sina namna, lakini sijawahi kumtumikia Mungu ambaye ananyamaza. Nilishakubaliana mimi na Mungu, mpango wa Mungu ndiyo mpango wangu, sasa wajiandae, mimi siyo Sheikh Yahaya, mmeingia choo cha kike, nasema ‘Mama yangu mzazi’ nitaacha kuhubiri, nitaacha kuhubiri ….mimi ...