MREMBO RAY C AMLILIA MSANII WA WCB REYVANNY
Msanii mkongwe wa Bongo Fleva mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni, Ray C amedai kuwa anamkubali zaidi Rayvanny kutoka lebo ya WCB. Ray C amesema kuwa amesikia msanii huyo amewaandikia wasanii wengi nyimbo hivyo na yeye anatamani siku moja aje kufanya naye kazi. “Nampenda sana yule mtoto Rayvanny. Anaandika sana mashairi, nasikia anaandikia wasanii wengi nyimbo hata mimi natamani kufanya naye kazi,” Ray C amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio. Mbali na hilo msanii huyo ameongeza kuwa anamheshimu sana Diamond Platnumz kutokana na kule alipofika kwakuwa muziki wake umefika sehemu ambayo wao hapo mwanzo hawakuwahi kufika.