Posts

Showing posts from September 9, 2014

MTOTO APIGWA KIKATILI NA BABA'AKE..AFANYIWA UPASUAJI WA KICHWA!

Image
Mtoto Amani Elisha (10) aliyepigwa vibaya na baba yake mzazi hadi kuzimia kwa siku mbili.   KATIKA   hali ambayo siyo ya kawaida iliyowashangaza wakazi wa eneo la Ukonga Mazizini kwa Makobe, baba  mmoja aliyefahamika kwa jina la Elisha Zakari amedaiwa kumpiga mwanaye wa kumzaa kip i go kama cha ng’ombe machungani na kusababisha azimie na kulazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Mtoto huyo aliyepigwa ni Amani Elisha (10) ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi Maarifa iliyoko Ukonga, Dar es Salaam, baada ya kipigo alizimia siku mbili.  Tukio hilo la kikatili lilitokea usiku wa Ijumaa iliyopita na sababu ya mtoto huyo kupewa kipigo inadaiwa ni kutokana na utoro shuleni na kwamba hata akienda huwa haandiki.Waandishi wetu waliponasa tukio walimtafuta mama mzazi wa mwanafunzi huyo maarufu kama mama Amani na mahojiano yakawa hivi:  Mwandishi: Mama ni kweli kuwa mume wako alimpiga mtoto wenu? Mama Amani: Ni kweli baba yake Amani ndiye aliyempiga. Mwandishi: Kwani

MOTO WATEKETEZA BWENI SHULE YA AFRICAN MUSLIM MJINI MOSHI HIVI SASA

Image
 Bweni la wanafunzi katika shule ya sekondari ya African Muslim iliyopo Laloleni manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro linateketea kwa moto hivi sasa. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema moto huo umeanza majira ya saa 2 za usiku huku chanzo chake bado hakijajulikana na ripota wetu Dixon Busagaga aliye eneo la tukio anafuatilia ajali hii na atatujulisha kila kitachojiri na kupatikana. Kikosi cha zimamoto kimefanya jitihada za kuzima moto huo licha ya kukabiliwa na changamoto ya maji.

TAHADHARI...HUU NDIO UGONJWA UTOKANAO NA KUNYONYANA SEHEMU ZA SIRI

Image
MAPENZI KWA NJIA YA MDOMO, NI CHANZO KIKUU CHA  SARATANI YA KOO? Saratani imeendelea kuwa tishio hapa nchini huku hofu ikiendelea kuikumba jamii kutokana na wataalamu wa afya kushindwa kufahamu tiba halisi ya maradhi hayo hatari. Takwimu kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road zinaonyesha ongezeko la saratani ya mdomo na koo kwa kiasi kikubwa kutoka kesi 167 mwaka 2006 hadi 277 mwaka 2012. Mkurugenzi wa Idara ya Kinga  Ocean road, Julius Mwaiselage anaeleza kuwa watanzania wasipende kuiga mambo ambayo si sahihi bila kujua madhara yake kama kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo. “Saratani ya mdomo ipo, na nyingine zinasababishwa na zinaa “ anasema Dk Mwaiselage Tafiti za saratani Tafiti mbalimbali zimewahi kufanyika nchini na kubaini kuwepo kwa ongezeko la saratani ya mdomo.Utafiti uliofanywa na Dk Innocent Mosha wa Kitengo cha Patholojia cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), umebaini aina za saratani 1,594, kati ya hizo 509 zikiwa ni za midomo kwa mwaka 2003 pekee.

VYAMA VYA SIASA VINAVYOUNDA TCD VYATOA TAMKO KUHUSU MCHAKATO WA KATIBA NA UCHAGUZI MKUU WA 2015.

Image
Na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma. VIONGOZI Wakuu wa Vyama vya siasa vyenye Wabunge vinavyounda Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) wameku wa katika mashauriano ya zaidi ya mwezi mmoja tangu tarehe 2 Agosti mwaka huu huku wakishauriana juu ya mwenendo wa mchakato wa Katiba Mpya na jinsi ya kuwa na uchaguzi ulio huru na wa haki hapo mwakani Akiongea kwa niaba ya viongozi wengine wa kituo hicho, Mwenyekiti wa TCD, Mhe. John Cheyo amesema kuwa Katika mashauriano hayo yaliyochukua sura ya Kamati ya Makatibu Wakuu, Kamati ya Wenyeviti wa Vyama vya CCM, CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi katika hatua tofauti. Mhe. Cheyo ameeleza kuwa kamati zote zilitoa taarifa zao kwenye vikao vya Viongozi Wakuu wa Vyama (Summit) ya TCD ambayo wajumbe wake ni Wenyeviti, Makamu Wenyeviti na Makatibu Wakuu wa Vyama wanachama. Mhe. Cheyo aliongeza kuwa katika kutafuta maridhiano, Wenyeviti na Makatibu Wakuu wa Vyama walifanya mashauriano na Mhe. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete siku ya tarehe

BREAKING NEWZ.MTOTO WA RAIS APIGWA RISASI

Image
Mtoto wa aliyekuwa Rais wa Nigeria, Olesugun Obasanjo amejeruhiwa kwa risasi wakati wa mapambano na wanamgambo wa kiislamu Boko Haram. Luteni Kanali Adeboye Obasanjo alijeruhiwa siku ya jumatatu wakati jeshi la Nigeria lilipokuwa likipambana kuudhibiti mji wa Michika karibu na mji wa Mubi mji uliokuwa ukidhibitiwa na wanamgambo katika jimbo la Adamawa. Msemaji wa zamani wa Olusegun Obasanjo ameiambia BBC kuwa kanali Adeboye anaendela vizuri. Wakazi wa eneo hilo wanasema kuwa maelfu ya watu wameyakimbia makazi yao, wanajeshi wameondoka kwenye kambi za kijeshi na chuo katika jimbo hilo kufungwa. Wanamgambo wa Boko haram wamedhibiti miji mingi kaskazini mashariki na kutangaza kuwa himaya za kiislamu

AJALI NYINGINE TENA LEO YAUA DEREVA SEKENKE, SINGIDA

Image
Wananchi wakishuhudia lori la saruji lililopinduka na kuua dereva wake leo eneo la Milima ya Sekenke mkoani Singida. Pichani juu na chini malori mengine ya mizigo yakipita karibu na eneo la tukio. Moja ya lori likitoa msaada wa kulivuta lori lililopata ajali kutoka bondeni. DEREVA wa lori lililokuwa limebeba saruji kutoka jijini Dar es Salaam kuelekea Mwanza leo amefariki dunia baada ya lori hilo kupinduka eneo la Sekenke mkoani Singida. Watu wengine wanne waliokuwa kwenye lori hilo wamejeruhiwa. Mmoja wa mashuhuda wa ajai hiyo ameiambia tovuti hii kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kufeli breki kwa lori hilo lililokuwa likishuka Milima ya Sekenke na mpaka anaondoka eneo la ajali hiyo bado dereva (marehemu) na mmoja wa watu waliokuwemo aliyekuwa hai walikuwa bado wamenasa kwenye lori hilo.

KABURI LA MMOJA KATI YA WALIOPATA AJALI YA BUS MUSOMA LAFUKULIWA NA WATU WASIOJULIKANA

Image
Kaburi la mmoja kati ya watu waliopoteza maisha katika ajali mbaya iliyohusisha mabasi ya Mwanza Coach na J4 katika eneo la Sabasaba, Musoma, Mara limekutwa likiwa limefukuliwa na watu wasiojulikana leo asubuhi.A Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichofika katika eneo la makaburi ya Musoma Basi, ndugu wa marehemu aliyetajwa kwa jina la Juma Sai walienda asubuhi kuangalia kaburi ikiwa ni siku ya tatu tangu wafanye mazishi, ndipo walipokuta kaburi limefukuliwa na mbao zilizotumika kuhifadhi mwili kwa imani ya dini ya kiislamu zikiwa zimewekwa pembeni. “Mwili wa marehemu bado uko ndani, watu wengi wako hapa na polisi wameimarisha hali ya usalama. Madaktari wameshafika hapa na wanafanya uchunguzi kuona kama kuna kiungo chochote kilichotolewa kwenye mwili wa marehemu. Inasikitisha sana.” Kimeeleza chanzo chetu cha kuaminika. Ijumaa iliyopita, kulitokea ajali mbaya iliyohusisha magari matatu, mabasi ya kampuni ya Mwanza Coasch na J4 pamoja na gari dogo aina ya Landcr