Gadner alitongoza na kuwashika makalio wanawake mbele yangu – Lady Jaydee
Wiki hii Lady Jaydee amewapa nafasi mashabiki wake kumuuliza maswali naye kuyajibu kupitia akaunti yake ya Instagram. Ameulizwa maswali mengi, na miongoni mwa maswali hayo ni la kuhusu ndoa yake na mtangazaji wa Radio E-FM Gadner G. Habash. Haya ni maswali na majibu kama alivyopost Instagram. Tunasikia umeachana na mume ni kweli au uzushi? JIBU : Hatuja achana niliamua kumuacha Kwanini umeachana/umemuacha mume? JIBU : Nimemuacha kutokana na kuwa Ndoa inatakiwa iwe na maelewano, furaha, amani na upendo. .. ila kwa bahati mbaya vyote hivyo havikuwepo , sikuwa tayari kuendelea kuishi kwa maumivu huku niki pretend ili kuiridhisha jamii. Huoni kama umejishushia heshma kuachana na mume? JIBU : Sioni hivyo, ila naona nilikuwa najishushia heshma zaidi kuishi na mume asie na heshma, anaeweza kutongoza na kushika wanawake makalio wakati mi niko jukwaani naimba. Kuwapa mademu magari yangu waendeshe na kuyagonga wakati niko safarini...