Posts

Showing posts from May 27, 2016

HUYU NDO MTOTO WA MAREHEMU KEBWE ALIYEGOMA KUMPA MKONO RC MAKONDA

Image

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA JK IKULU JIJINI DAR LEO

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete wakifurahia jambo mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU

Shilingi Bilioni 3 na Mali za Bilioni 10 zataifishwa na TRA Kutoka kwa Wakwepa Kodi Bandari Kavu ya Azam

Image
Mamlaka ya kukusanya kodi TRA kupitia madalali wa Yono Auction Mart wamekusanya mali za bilioni 3 pamoja na kutaifisha mali za bilioni 10 kutoka kwa wafanyabiashara waliopitisha makontena 329 kupitia bandari kavu ya Azam bila kulipa kodi na bado wanaendelea na msako bara na visiwani. Madalali hao wamesema watu walipe kodi na watoe risiti za elekroniki la sivyo mali zitakamatwa.

WAZIRI MKUU MH. KASSIM MAJALIWA AKAGUA MRADI WA MABASI YA MWENDOKASI DART LEO

Image
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza na mwanafunzi Amina Abdallah wa darasa la sita katika shule ya msingi ya Ukombozi jijini Dar es salaam ambaye amepanda basi la Mwendo Kasi Ajentina na kushuka Manzese, Waziri Mkuu Majaliwa ametumia usafiri wa DART leo kutoka Feri kwenda Kimara Mwisho wakati alipokagua miundombinu ya usafiri huo ili kujionea mafanikio na changamoto mbalimbali zinazojitokeza mara baada ya mradi huo kuanza mwezi mmoja sasa ili ziweze kurekebishwa na kuuboresha zaidi.  Usafiri DART umekuwa mkombozi kwa wasafiri wengi wa jiji la Dar es salaam wakati wanapotoka majumbani mwao na kuelekea kazini na kurejea majumbani mwao,Katikati ni Bw. David Mwaibula aliyekuwa Mwenyekiti Mamlaka ya Usafiri wa Daladala Dar es salaam (DRTLA) zamani aliyeambatana na Waziri Mkuu kukagua mradi huo leo.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akifurah...

STORI YA KIFO CHA ANETH MDOGO WA BILIONEA ALIYECHINJWA

Image
May 26 kulitokea mauaji ya kutisha ya kukatwa mapanga kwa mwanadada Aneth ambaye ni ndugu wa Tajiri mmoja ambaye naye aliuliwa kwa kupigwa risasi. Aneth amepigwa mapaga na watu wasiojulika na kukimbia. Jirani wa Anetha pia mfanyakazi mwenzake anafafanua vizuri "Yaani Aneth hata siamini, jana tulikua nae kazini, kaondoka kufika nyumbani akakuta housgal katoroka, akapiga simu kwa mwenzetu akamueleza kwamba leo hatokuja ili angalie logistics. Mtoto wake ana miaka minne ndio alpo hojiwa alisema hivi jana walikuja watu watano weusi, wakavunja mlango ni majira ya mama saa tatu usiku, akakimbia chumbani, walipoingia wakamkuta mtoto wakauliza mama huko wapi akasema chumbani, wakamfuata huko mtoto hajui kilichoendelea. hadi asubuhi school bus ilipokuja alijaribu kutoka akashindwa na mwishowe iliondoka. Anafafanua: Baada ya kuona mama yake haamki ndipo alipotoka kwa jirani na kuwaita. Majirani walikwenda na kukuta Aneth akiwa amechinjwa na akiwa uchi (seem...

BUNGE LAENDELEA NA KIKAO CHAKE MJINI DODOMA LEO

Image
Baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza cha maswali na majibu na uchangiaji wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi leo mjini Dodoma. Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Anthony Peter Mavunde ambaye akiwasalimia kwa furaha wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Dodoma leo kwenye viwanja vya Bunge. Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Anthony Peter Mavunde akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ufundi -VETA mkoa wa Dodoma nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma. Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) George Masaju (katikati) akizungumza na viongozi wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) waliolitembelea Bunge mjini Dodoma. akiwasisitiza jambo viongozi wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) alipokutana nao nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma ...

Tanzia: Hussein Macheni afariki dunia

Image
\ Hussein Macheni enzi za uhai wake. Aliyekuwa mmiliki wa baa maarufu ya Macheni iliyopo Magomeni jijini Dar es Salaam, Hussein Macheni amefariki dunia leo baada ya kuanguka ghafla akiwa nyumbani kwake Magomeni. Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu ni kwamba Macheni alianguka ghafla majira ya saa 9 asubuhi na kukimbizwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo iligundulika kuwa tayari amefariki. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Muhimbili kusubiri taratibu nyingine. Mwenyeji Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi. AMEN.

ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUJIRUSHA KUTOKA KWENYE MNARA WA SIMU JIJINI MWANZA.

Image
Kijana Mmoja (picha) Jijini Mwanza amenusurika kifo baada ya kujirusha kutoka katikati ya mnara wa simu. Na BMG Tukio hilo limetokea hii leo na kuvuta watu wengi waliofika kumshuhudia kijana huo ambae amepanda katika mnara huo tangu majira ya asubuhi na kukatalia mnarani hadi majira ya saa sita mchana. Mashuhuda wa tukio hilo ambao pia ni marafiki wa karibu na kijana huyo, wamesema huenda kijana huyo amefikia maamuzi hayo kutokana na ugumu wa maisha ambao amekuwa akiulalamikia huku wengine wakisema ni kutokana na kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo gundi ambayo amekuwa akiyatumia. Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa jeshi la uokoaji na zima moto mkoani Mwanza, mmoja wa maafisa wa uokoaji Mussa Kaboni, amsetoa rai kwa makampuni yenye minara ya simu kuimarisha ulinzi katika minara hiyo ili kuondoa hatari inayoweza kujitokeza kutoka kwa raia wasio wema. Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walionekana kuchukizwa na kitendo cha kijana huyo na kusiki...