Posts

Showing posts from December 13, 2014

Faida za kiafya za kunywa maji ya moto

Image
NJIA SITA ZA KUNYWA MAJI YA MOTO ZINAZOTIBU MWILI WAKO. Kunywa kikombe kimoja cha maji ya moto kila asubuhi inaweza kukutibu mwili wako kwa kusaidia umeng’enywaji wa chakula na kuzuia kuzeeka mapema kabla ya wakati. Wengi wetu huianza asubuhi vyema kwa kikombe safi cha kawaha ya moto au chai ya moto kwa lengo la kuuchangamsha miili yetu baada ya kutoka kitandani. Pale tunakunywa maji, basi wengi wetu hupendelea kunywa ya baridi, lakini kutokana na watalaam wa afya wanavyosema,  tunafanya makosa kufanya hivyo. Mara nyingi unywaji wa maji moto au uvuguvugu, hususani majira ya asubuhi, inasaidia kuiponya miili yetu na kuitibu, kwa kusaidia kuongeza nguvu katika mmeng’enyo wa chakula ma kupunguza taka mwili ambazo zinaweza kuzuia kinga zetu kuwa katika hali yake nzuri ya mfumo sahihi. “matabibu wanasema na kushauri kunywa maji moto ama uvuguvugu nyakati za asubuhi, kila siku, sambamba na mchanyanyo wa maji ya limao, au chai ambayo haina madhara kwa mwili” a...

Vyakula 10 vinavyoongeza uwezo katika tendo la ndoa

Image
Tatizo la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa wanandoa na wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu ndoa 4 kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliana na tatizo hili. Aidha wanaume 6 kati ya 10 wanatajwa kulalamikia upungufu wa nguvu za kiume na kuacha idadi ya wanawake wanaokabiliwa na tatizo hilo kwa mujibu wa uchunguzi kubaki na asilimia 13. Pamoja na matatizo mengine kutajwa kuchangia upungufu wa nguvu za kiume na kushuka kwa msisimko wa tendo miongoni mwa wanandoa, uchunguzi umeonesha kuwa utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye mafuta ni moja kati ya sababu zinazochangia kwa kasi tatizo hili. Kwa kuzingatia hilo, watafiti wa masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini aina kumi ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya kufanya tendo la ndoa. Vyakula hivyo ni hivi vifuatavyo: PILIPILI Pilipili zilizocheshwa zimetajwa kuwa na uwezo wa kusaidia msukumo wa usambazaji damu mwilini, ambao kwa kiasi kikub...

Jinsi ya kudumisha uzito wa kawaida wenye afya

Image
Kudumisha uzito wa mwili bora unakusaidia wewe kutokana na hatari Unapaswa kufahamu ya kwamba unakula zaidi kama unazindisha kulingana na vile mwili wako unavyohitaji. • Unapokula zaidi na haufanyi aina yeyote ya mazoezi ya kujenga mwili, unaweza kupata uzito au unene mwingi kupita kiasi. • Kuishi kwa ile hali ya kuwa na uzito wa mwili vyema, ni muhimu kwako kula chakula bora na kwa kiasi. • Kuna njia muafaka ambazo unaweza kufanya ili kudumisha ule uzito wa mwili ambao unaofaa, kama vile:- - kupunguza jinsi unavyokula mafuta na sukari - kupunguza kiasi cha chakula - kuacha kula tu mradi umeshiba - kuongeza kufanya mazoezi ya mwili • Kudumisha uzito wa mwili bora unakusaidia wewe kutokana na hatari kama vile:- - kuumwa na viungo vya mwili - kupandwa na damu - ugojwa wa sukari - ugojwa wa moyo - ugojwa wa saratani manyandahealthy

madhara ya sabuni za kurudisha ubikra!!

Image
  WANAWAKE wameshauriwa kuacha kutumia sabuni za kunawia sehemu za siri ambazo hudaiwa kurejesha ubikira kwani zina madhara makubwa ikiwemo kusababisha kansa ya shingo ya kizazi. Mkaguzi wa Dawa na Mfamasia wa Manispaa ya Dodoma Daria Mwanuka alisema hayo mwishoni mwa wiki katika mahojiano na mwandishi wa habari hizi wakati wa uteketezaji dawa, vipodozi na vyakula visivyofaa kwa matumizi ya binadamu.   Kazi hiyo ilifanywa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Kati. Alisema kumekuwa na sabuni mbalimbali ikiwamo Kaisiki ambapo wanaoziuza wanadai zimekuwa zikisababisha bikira iliyopotea kurudi kitu ambacho si kweli. "Sabuni hizo zinapunguza tu majimaji yaliyo sehemu za siri za mwanamke jambo ambalo husababisha wakati wa kufanya mapenzi mwanaume kupata ugumu kwenye muingiliano kwa vile mwili unakuwa umekataliwa kutoa maji na hivyo kuleta michubuko kitu ambacho ni hatari hasa wenye maambukizi ya magonjwa," alisema.   Alisema ...