Posts

Showing posts from August 13, 2017

Gigy azidi kukonda, apima ngoma

Image
Gift Stanford ‘Gigy Money’. VIDEO Queen, Gift Stanford ‘ Gigy Money ’ ambaye mwili wake umepungua sana kiasi cha kuwapa wasiwasi mashabiki wake, amesema licha ya kupungua huko, lakini ni mzima kwani amepima ‘ngoma’ na kujikuta yuko fi ti. Akizungumza na Risasi Jumamosi juzikati, Gigy aliifungukia afya yake na kusema baada ya kujipunguza kwa mazoezi, baadaye aliamua kutumia dawa maalum za kujipunguza kwa makusudi kwani kuna mwili aliokuwa akiutafuta na sasa umekaa mahala pake. Gigy alisema hata hivyo, katika kuwahakikishia mashabiki kuwa kukonda kwake hakuna tatizo, ameamua kupima ngoma na majibu yamerudi yakimuonyesha yuko sawa kabisa. “Nimeamua kupima ngoma ili kuwaondoa wasiwasi mashabiki, kwani mwili huu si wa magonjwa kama watu wanavyodhani, nimejipunguza kwa kutumia dawa maalumu na nimefanikiwa nashukuru Mungu,” alisema Gigy. Katika hali ya kushtua, Gigy pia alifungukia maisha anayotaka kwa sasa ya kutokuwa na mpenzi ‘pamanenti’ wa kupika na kupakua, bada...

BREAKING NEWS: MZEE KILOMONI ASIMAMISHWA UANACHAMA, AFUTWA UONGOZI WA BARAZA

Image
Aliyekuwa mdhamini wa Simba, Hamisi Kilomani. Klabu ya Simba imetangaza kumtoa mzee Hamisi Kilomani kwenye Baraza la Wadhamini kwa kosa la kuvunja katiba ya klabu hiyo. Pia, wanatarajia kumpekelea barua ya kumfuta uanachama na ikiwa hatafuta kesi na kushindwa kujitetea watamfukuza uanachama moja kwa moja. Aidha, profesa Juma Kapuya ameteuliwa kuziba pengo la Ally Sykes ambaye kwa sasa ni marehemu katika baraza hilo, nafasi ya mzee Kilomoni imejazwa na Mkuu wa wilaya ya Kilosa, Alhaj Adam Mgoyi.

IGP Sirro awaaga askari na maofisa wanaokwenda Sudani

Image
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akiwakabidhi bendera ya taifa askari kumi (10) waliopata uteuzi wa kwenda kuiwakilisha nchi ya Tanzania kwenye kazi ya Ulinzi wa Amani nchini Sudani ya Kusini (UNMISS) IGP Sirro, amewataka askari hao kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia misingi ya sheria na taratibu. Picha na Jeshi la Polisi. Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akiwa kwenye picha ya pamoja na askari waliopata uteuzi wa kwenda kuiwakilisha nchi ya Tanzania kwenye kazi ya Ulinzi wa Amani nchini Sudani ya Kusini (UNMISS) IGP Sirro, amewataka askari hao kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia misingi ya sheria na taratibu. Picha na Jeshi la Polisi.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA:SERIKALI KULIPA MADENI YA WATUMISHI

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema serikali italipa madeni yote ya Watumishi ambayo yamehakikiwa na kukutwa kuwa ni halali.  Waziri Majaliwa ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui kwenye mkutano uliyofanyika kata ya Goweko, wilayani Uyui mkoani Tabora na Rais Pombe Magufuli alisitisha malipo kwa sababu ya zoezi la kubaini watumishi hewa, sasa kazi hiyo imeshakamilika na yale yaliyobainika kuwa halali yatalipwa huku akiwataka Watumishi hao wafanye kazi ya kuwadumia wananchi kwa bidii. "Hivi sasa tunadhibiti uzalishaji wa madeni mapya ya watumishi, hakuna madeni ya matibabu, ya likizo au ya masomo. Kila mtumishi anaruhusiwa kujiendeleza, lakini ni lazima kwanza aandike barua kwa Mkurugenzi wa Halmashauri kuelezea nia yake na akikubaliwa, ndipo aanze kutuma maombi kwenye vyuo. Mtumishi akiamua kuomba chuoni moja kwa moja ndipo alete madai yale, hatapewa chochote kwa sababu ni nje ya utaratibu,"  alisema Ma...

Shamba jingine la Sumaye lachukuliwa

Image
WAKATI machungu ya kupoteza shamba lake lenye ukubwa wa ekari 33 lililokuwa Mabwepande yakiwa hayajatuliwa, aliyekuwa Waziri Mkuu Katika serikali ya awamu ya tatu, Frederick Sumaye amepoteza shamba jingine mkoani Morogoro baada ya serikali kulichukua. Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero imelitwaa shamba la Sumaye lenye ukubwa wa ekari 326 baada ya kupata kibali kutoka kwa Rais Magufuli kwa madai kuwa hajaliendeza licha ya kupewa notisi ya kufanya hivyo. Shamba la Sumaye la Mabwepande lilichukuliwa Novemba mwaka jana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi akifikia uamuzi huo baada ya mmiliki wa shamba hilo kutoliendeleza kama notisi ya siku 90 aliyopewa ilivyokuwa ikimtaka. Oktoba 28 Rais Magufuli alibatilisha umiliki wa shamba hilo namba 3,074 lililopo Mabwepande. Shamba hilo lilikuwa na hati namba 53086 na jina la umiliki lilikuwa ni Frankline Sumaye. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, Florent Kyombo jana alisema kuwa Rais Magufuli amekubali ku...

Aliyekuwa mke wa Barnaba afunguka alichokuwa anakikosa

Image
 Aliyekuwa mke na mama mtoto wa mwanamuziki Barnaba Elias, Zuu Namela, ametoa kile kinachoitwa la moyoni, na huenda ndio sababu iliyomtoa kwa mzazi mwenzake na kuanzisha mahusiano mapya. Kwenye ukurasa wake wa instagram Zuu Namela ameandika ujumbe kuwa kwa miaka mitano (ambayo ilikuwa ndani ya mahusiano na Barnaba) alikuwa anakosa furaha ya kweli na amani ya moyo, lakini sasa ameipata furaha hiyo baada ya kuachana. "Ni watu wachache sana wanaojua nikitu gani nilikua nakosa katika maisha yangu! Unaweza ukapata kila kitu kwenye maisha ila ukakosa furaha,amani,heshima......kwa zaidi ya miaka mitano ichi ndo nilicho kuwa nakitafuta #AMANIyaMOYO " aliandika Zuu Namela. Hivi karibuni Zuu Namela ameonekana akimpost mwanaume mwengine kwenye ukurasa wake, huku akiandika jumbe mbali mbali za mapenzi, na kuacha mashabiki wake kuwa ndiye mbadala wa Barnaba ambaye ni baba mtoto wake.