Posts

Showing posts from November 7, 2017

Rais Magufuli Anastahili Pongezi, Amefunua Blanketi Lililotufunika

Image
Rais Dk. John Pombe Magufuli. M UNGU ni mwema kwa sababu ametufikisha leo tukiwa wazima, hakika ahimidiwe daima. Leo nachukua nafasi hii kumpongeza Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa mafanikio aliyotuletea ndani ya miaka miwili ya utawala wake. Ninapofanya tathmini ya miaka miwili ya uongozi wa Rais Magufuli, ni kama narudia kwa sababu juzi na jana wengine wameandika au kusema kupitia vyombo vya habari. Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2015 na Rais Magufuli kuibuka mshindi, alianza kuonesha kwa haraka kuwa yeye ni kiongozi asiyetaka mchezo kwenye kazi. Aliliambia taifa kuwa alipokea nchi ikiwa imejaa uozo kila idara na alitumia hoja hiyo kukataa hoja ya kupendekezwa kwa Katiba Mpya, iliyowahi kutolewa na baadhi ya watu wakati alipotimiza mwaka mmoja madarakani kwa kusema wazi, ‘niacheni niisafishe nchi kwanza.’ Mwaka wake wa kwanza alifanya mengi yaliyowafurahisha wananchi wengi, kama vile kufuta safari za nje kwa maofisa wa serikali labda kama ni za lazima s...

Waziri Wa Tamisemi Atoa Maagizo 6 Kwa Wakuu Wa Mikoa

Image
Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo. Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo, ametoa maelekezo kwa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kufuatia kutangazwa kwa matokeo ya darasa la saba. Waziri Jafo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo, ameeleza kwamba jumla ya watahiniwa 909,950 walifanya mtihani ambapo watahiniwa 662,035 wamefauli kwa daraja A – C ikiwa ni sawa na 72.76% ya watahiniwa wote. Kufuatia ufaulu mkubwa uliojitokeza ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikalli za Mitaa, imetoa maelekezo kwa mikoa yote ili waweze kuanza maandalizi mapema ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mapema mwakani kabla ya kukamilika kwa uchaguzi wa wanafunzi hao. Ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wote waliofaulu mitihani wanapata nafasi ya kujiunga kidato cha kwanza Januari 2018, maelekezo yafuatayo yametolewa. 1. Wakuu wa Mikoa yote wametakiwa kuhakikisha kuwa miundo...

BREAKING NEWS: Gavana afariki katika ajali, Kenya

Image
Gavana wa kaunti ya Nyeri nchini Kenya, Wahome Gakuru amefariki mapema siku ya Jumanne kufuatia ajali mbaya ya barabarani katika eneo la Kabati katika barabara kuu ya Thika-Sagana katika kaunti ya Murang’a. Alikimbizwa katika Hospitali ya Thika Level 5 kwa matibabu ya dharura lakini akaaga dunia. Kaunti kamishna wa Murang’a John Elungata alithibitisha kifo hicho. Bwana Elungata alisema kuwa kabati ni eneo hatari na madereva hukosa mwelekeo kila kunaponyesha. Maafisa wa polisi wanasema kuwa gari la gavana huyo lilikuwa na abiria wanne wakati wa ajali hiyo ,akiwemo msaidizi wake wa kibinafsi, mlinzi wake na Dereva. Mkono na mguu wa msaidizi wake wa kibinafsi ilivunjika huku miguu ya mlinzi wake ikijeruhiwa vibaya huku Dereva akidaiwa kuwa katika hali nzuri. Polisi wanasema kuwa ajali hiyo ilitokea baada ya gurudumo moja la gari hilo kupasuka wakati mvua kali ilipokuwa ikinyesha. Mwili wa Gavana huyo umesafirishwa hadi katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Le...

NDOA YA IRENE UWOYA NA DOGO JANJA NI BATILI,MASHEHE WAFUNGUKA HAYA LIVE

Image
Msanii wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ na mwigizaji Irene Pancras Uwoya wakifanya yao baada ya kufunga ndoa.WAKATI sakata la ‘ndoa’ ya msanii wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ na mwigizaji Irene Pancras Uwoya likizidi kupamba moto, mashehe mbalimbali wameibuka na kutoa sababu zinazodhihirisha kuwa ndoa hiyo ni batili, Ijumaa Wikienda linakupakulia ubuyu wa motomoto. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Ijumaa Wikienda, mashehe watatu wa misikiti tofauti jijini Dar, walioomba hifadhi ya majina, walimkosoa Uwoya na Dogo Janja kwa kuonesha kwamba walichokifanya si sahihi. NI BATILI Mashehe hao walisema kuwa, ndoa hiyo ni batili kutokana na jinsi ilivyofungwa, lakini pia hata kama walikuwa wanafanya filamu, bado walikiuka taratibu za Dini ya Kiislam. Akizungumza kwa niaba ya wenzake, mmoja wa mashehe hao alianika sababu tano (5) zinazodhihirisha kwamba ndoa hiyo ni batili; SABABU YA KWANZA (MATITI NJE) Alisema kuwa, katika picha mbalimbali z...

SERIKALI YASEMA HAIWEZI KUAJIRI VIJANA WOTE NCHINI

Image
Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Peter Mavunde. Serikali kupitia Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Peter Mavunde amesema kuwa si kweli kwamba serikali inaweza kuwaajiri wote kwenye sekta ya umma ila inachokifanya ni kuwahamasisha vijana kushiriki katika sekta za uzalishaji mali ikiwemo kilimo ufugaji na biashara.Mh. Mavunde ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Aida Joseph Kenani lililohoji, serikali ya awamu ya tano imepunguza wafanyakazi kwenye kada mbalimbali kwa kigezo cha kutokuwa na sifa. Je, ni lini sasa serikali itatoa ajira kwa kuwapa kipaumbele vijana wa nchi ambao kwa sasa ni wengi wamerundikana mtaani. “Katika azma ya kutengeneza nafasi nyingi za ajira hasa kwa kundi kubwa hilo la vijana serikali, imekuja na mipango mikakati mbalimbali, si kweli kwamba tunaweza tukawa tuna nafasi za kuwaajiri wote kwenye sekta ya ...

Vyakula Vinavyosaidia Kuondoa Maumivu Wakati Wa Hedhi

Image
WIKI iliyopita tuliona jinsi matunda yanavyosaidia kutibu maradhi mbalimbali mwilini, leo tutaangalia aina mbalimbali za matunda yanayoweza kutibu matatizo mbalimbali yanayowahusu wanawake wakati wa siku zao (menstruation period). Miongoni mwa matunda hayo ni papai bichi lakini lililokomaa ambalo lina uwezo wa kulainisha misuli ya njia ya uzazi hivyo kufanya kipindi cha hedhi kutokuwa na maumivu. Katika suala hili, ili wanawake kujiepusha na kupatwa na matatizo ya maumivu, kutokwa damu kwa wingi kusiko kawaida, kuchelewa kuona siku zao, wanashauriwa kuzingatia suala la lishe. Wanapaswa kujua vyakula gani wale na vipi wasile ili kujiwekea kinga ya kudumu dhidi ya tatizo hili. LISHE YA KUDHIBITI MATATIZO YA HEDHI Matatizo mbalimbali yanayohusiana na hedhi, yanaweza kudhibitiwa na hatimaye kutokomezwa kabisa kwa kutibu mfumo mzima wa mwili, ili kuondoa sumu iliyojilimbikiza katika mwili wa mgonjwa kwa kipindi cha muda mrefu, sumu ambayo imegeuka na kuwa chanzo ch...