Posts

Showing posts from September 11, 2013

POLISI TANZANIA KUPATA MAFUNZO YA UPELELEZI NCHINI UTURUKI

Image
Na Tamimu Adam, Jeshi la Polisi Jeshi la Polisi la Uturuki limetoa ufadhili wa masomo kwa  askari kumi na saba ( 17) wa Jeshi la Polisi Tanzania kupata mafunzo mbalimbali yakiwemo ya upelelezi wa wahalifu na mbinu za uchunguzi wa kimaabara pamoja na usimamizi na uendeshaji wa gari la matukio yatakayochukua muda wa mwezi mmoja nchini Uturuki. Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya jinai nchini (DCI) Kamishina Robart Manumba aliyasema hayo jana wakati wa kikao cha kazi kilichofanyika Makao Makuu ya Polisi. Alisema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya maboresho yanayolenga kuwaongezea askari weledi na kuwajengea uwezo wataalamu wa Maabara ya uchunguzi ya Polisi juu ya mbinu mbalimbali za kiuchunguzi na  upelelezi pamoja na matumizi sahihi ya vifaa  vya kiupelelezi. Aliongeza kuwa mafunzo hayo yatasaidia wataalamu wa Maabara ya uchunguzi ya Polisi kuweza kufanikisha kuwakamata wahalifu na kutambua   uhalifu uliotendeka kwa haraka,  hivyo, ku

ANGALIA PICHA ZA BOMOA BOMOA DAR YAMKUMBA ASHA BARAKA

Image
  Mkurugenzi wa bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’, ambaye pia ni Mjumbe wa NEC- CCM, Asha Baraka, akiwaka wakati akizungumza  na mtandao huu jana jioni alipokuwa akisimamia zoezi la kuwazuia wabomoaji kutobomoa nyumba na vibanda vya wananchi katika eneo hilo la Hanansifu bila kufikia muafaka kwa mazungumzo na wahusika.   Katapila likiendelea kubomoa….  Asha Baraka akisimama mbele ya Frem zake eneo hilo kuwazuia jamaa hao kuendelea na zoezi hilo hadi upatikane muafaka na wahusika kwanza. Chazo : Sufiani Mafoto   Asha Baraka, akionyesha alama ya pili iliyowekwa jana na kuanza kubomoa jana hiyo hiyo…..   Wananchi wakimsikiliza Asha Baraka…..   Sehemu ya madimbwi yaliyoachwa na wachimbaji hao mara ya kwanza ambayo kwa sasaa yameanza kukauka.   Nyumba ya Asha Baraka (kushoto) inayotakiwa kubomolewa na (kulia) ndiyo Ghorofa lilalokwepwa ili kupindisha barabara hiyo jambo linalofanya kubomolewa kwa nyumba za up

ANGALIA PICHA ZA MAZISHI YA MWANADADA ''MELISA'' WA BONGO MOVIE

Image
 Msanii wa Bongo Movie Steve Nyerere akiwa ameduwaa wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Zuhura Maftah Malisa nyumbani kwao Mikocheni jijini Dar es Salaam leo  Mtoto wa Marehemu akiaga mwili wa mama ake mzazi  Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza tayari kwa safari ya kwenda kuusitili mwili wa marehemu katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar. PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

HATARII...MBUNGE AFYATUA RISASI (AK-47) NDANI YA BUNGE BAADA YA KUTOKEA MABISHANO KATI YAKE NA SPIKA.

Image
MP fires AK-47 during Jordanian parliament session! Katikhali isiyo ya kawaida mbunge mmoja nchini Jordan alifyatua risasi ndani ya bunge baada ya kutokea mabishano kati yake na mbunge mwenzake ambaye ni Spika wa bunge. Hata hivyo hakuna mtu aliejeruhiwa na imekuwa ni kawaida kwa Wabunge wa bunge la Jordan kushikana mashati na kurushiana ngumi. Source: BBC swahili habari saa 3:00 usiku. A Jordanian MP opened fire on his colleague inside the Jordanian House of Representatives on Tuesday morning, following an argument during the parliamentary session. According to Roya News, an Amman-based news service, MP Talal Al Sharif opened fire using a Kalashnikov automatic weapon on his colleague MP Qusai Dmeisi the inside of the House of Representatives on Tuesday. Early reports from Al Ghad news, a Jordanian newspaper, Sharif opened fire using the AK-47 during a Foreign Affairs Council meeting at the House of Representatives , which lies in the Abda

Hakimu apigwa na wanajeshi wa JWTZ huko karagwe kwa kudhaniwa kuwa ni Mnyarwanda

Image
Matendo Manono (kushoto) Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Matendo Manono ambaye ni Hakimu Mkazi katika Mahakama ya Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera amelalamikia kitendo cha kupigwa na kujeruhiwa vibaya na Askari wa Tanzania, katika zoezi la kuwaswaga wahamiaji haramu wa kinyarwanda wanao ishi nchini Tanzania.    Soma maelezo ya hakimu huyo hapo chini... " i have a serious contempt of this country...while they know for sure that this country has no National ID stil they want us to show Citizenship ID...   Imagine this was travelling to western part of TZ (Karagwe) today i have been arrested by the damned Immigration, police officers and JW people that am a prohibited immigrant simply because am tall with big (long,edged?)nose .. i have been seriously humiliated and beaten simply because i resemble Rwandese something which is neither sin nor unlawful under The Immigration Act or The Citizenship Act.... I don't know if those people o

ANGALIA PICHA ZA SHOW YA AZONTO FUNIKA MBAYA DAR ES SALAAM

Image
  Menina akifanya yake jukwaani.  Vanessa jukwaani akiimba Closer  Snura Majanga akitoa burudani Walter Chillambo akiimba     Mashabiki waliojitokeza wakishangilia    Fuse ODG akifundishwa kucheza kiduku na shabiki Wasanii wa Marco Chali Foundation wakiwa katika picha ya pamoja. ********************************************* MSANII wa muziki wa kileo kutoka nchini Ghana Fuse ODG, Azonto amewapagawisha mashabiki wake wa Bongo baada ya kuchanganya staili yake ya uchezaji Azonto pamoja na ile ya Kiduku ambayo ni maarufu ya hapa nchini, wakati wa shoo yake iliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Ustawi, mwishoni mwa wiki. Fuse ODG ambae anajulikana zaidi kama Azonto alipanda jukwanii majira ya saa tisa kasoro usiku baada ya wasanii wengine wengi kumaliza kutoa burudani.  Ilikuwa ni baada ya kupanda kwa kundi la Tip Top Connection huku likiongozwa na msanii Madee pamoja na msanii Chid Benz ambae alii

NAPE:CHADEMA WAMEPEWA MABILIONI TOKA NJE KUVURUGA MCHAKATO WA KATIBA.

Image
Adai ndio chanzo cha kupigana bungeni Asema ndizo walizotumia kuzunguka na helkopta nchini. Aeleza yaliyotokea bungeni sio bahati mbaya, Chadema waliyapanga Ashukuru bunge kuendelea kuonyeshwa"live" ili wananchi waone ujinga wao. Awatuhumu kuweka masilahi yao mbele badala ya nchi. Asisitiza CCM kuendelea kuheshimu uamuzi wa wananchi juu ya katiba. Aonyesha madai ya Chadema kitakwimu yasivyojali wakulima na wafanyakazi. Katibu wa NEC ya CCM itikadi na Uenezi amesema kinachowasumbua Chadema mpaka wanafanya yote waliyoyafanya hasa ngumi na vurugu bungeni ni namna watakavyoeleza kwa waliowapa pesa za kuvuruga mchakato wa katiba nchini kwani wanatakiwa kupeleka mrejesho jinsi walivyofanikiwa na jinsi walivyotumia mabilioni hayo. Nape ameyasema hayo kwenye mkutano mkubwa wa hadhara mjini Kahama kwenye ziara ya karibu siku ishirini kanda ya ziwa kwa mikoa mitatu yaani Shinyanga,Simiyu na Mara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndg. Abralhaman Kinana. &

KILICHOMUUA MSANII HUYU KINASIKITISHA.....

Image
TASNIA ya filamu Bongo imepata pigo lingine baada ya mwishoni mwa wiki iliyopita kuondokewa na msanii aliyekuwa akichipukia kwa kasi aliyefahamika kwa jina la Zuhura Maftah ‘Malisa’. Malisa alifariki dunia katika Hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar baada ya kusumbuliwa na uvimbe kichwani kwa takriban miezi mitatu. Wakizungumza na gazeti hili mara baada ya kifo hicho, baadhi ya wasanii wa filamu walielezea masikitiko yao na kusema hakika wamemkosa msanii ambaye siku za baadaye angekuwa moto wa kuotea mbali. “Kifo chake kimetusikitisha sana, Malisa alikuwa mmoja wa wasanii ambao walikuwa wakija kwa kasi, amefariki dunia wakati ndiyo kwanza nyota yake ilikuwa imeanza kung’ara lakini kazi ya Mungu siku zote haina makosa, akapumzike kwa amani,” alisema mmoja wasanii aliyeomba hifadhi ya jina lake. Msanii mwingine wa filamu ambaye huenda kifo hicho kimemgusa kuliko wengine ni Yvonne Cheryl ‘Monalisa’ ambaye inadaiwa muda mfupi kabla ya Malisa kufariki waliongea na kumw

ANGALIA PICHA NA STORY YA KIJANA ALIYEAMUA KUMCHINJA MPENZI WAKE KAMA KUKU

Image
Jessica Elialinga baada ya kuchinjwa. Tukio hilo lililoibua simanzi kubwa kutokana na marehemu kuhitimu Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari ya Kata ya Nyihogo, Kahama mwaka jana, lilijiri saa 12:45 Februari 6, mwaka huu. Kitendo hicho kilifanyika katika banda la mbuzi lililopo nyumbani kwa kijana huyo ambaye baada ya kutekeleza mauaji na yeye alifanya jaribio la kutaka kujitoa roho kwa kisu. Akisimulia juu ya tukio hilo, rafiki wa karibu wa Musa ambaye aliomba hifadhi ya jina lake kwa ajili ya usalama, alisema wiki moja kabla ya tukio hilo, mtuhumiwa huyo alikuwa akiwatangazia jamaa zake kwamba ana dhamira ya kumuua binti huyo kufuatia kubaini kuwa anamsaliti kimapenzi.   Muuaji Musa Petro.   “Unajua Musa anafanya kazi ya kuchuna ngozi za wanyama machinjio ya Wilaya ya Kahama, alitutangazia dhamira yake hiyo, lakini tulichukulia kauli yake kama mzaha. “Alisema anataka kufanya hivyo kwa sababu amekuwa akitumia gharama kubwa

Profesa Maina auponda muundo wa Bunge la Katiba

Image
Mwanasheria maarufu, Profesa Chris Peter Maina ameuponda muundo wa Bunge la Katiba la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kushauri utizamwe upya kabla ya kufanyika kwa kura ya maoni mwakani.Profesa huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, alisema kama hilo lisipofanyika inaweza kupatikana Katiba Mpya yenye mlengo wa chama kimoja cha siasa na kufafanua kuwa tatizo hilo limetokana na upungufu katika sheria ya mabadiliko ya Katiba ambayo imefanyiwa marekebisho kidogo na kupitishwa na wabunge mjini Dodoma wiki iliyopita. "Vyama vya siasa vinaweza kujipanga na kuweka watu wao katika zile nafasi 166 za wawakilishi wa kawaida katika Bunge maalumu la Katiba, hapohapo kumbuka kuwa wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Baraza la Wawakilishi Zanzibar wanaingia katika Bunge hilo," alisema. Wakati Profesa Maina akieleza hayo, Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar

Mashitaka matatu aliyosomewa makamu wa Rais wa Kenya mbele ya mahakama ya ICC

Image
  William Ruto amekana mashtaka yote yanayomkabili kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).  Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama hiyo, Fatou Bensouda anayesimamia kesi hiyo, alisema watuhumiwa wawili waliofikishwa mahakamani hapo jana, Ruto na mtangazaji wa Redio, Joshua arap Sang wanakabiliwa na mashtaka matatu kila mmoja, ambayo ni kuwalazimisha watu kukimbia makazi yao, mauaji na kuchochea ghasia. Kesi hiyo imeanza kusikilizwa siku chache baada ya Bunge la Kenya kupiga kura kutaka nchi hiyo ijitoe uanachama wa ICC, wakieleza kwamba imekuwa haina tija na inatumiwa kuwakandamiza Waafrika.

Mama Maria Nyerere adhulumiwa viwanja

Image
MJANE wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Mama Maria amedhulumiwa viwanja vitatu tofauti mjini Dar es Salaam. Hali hiyo, imesababisha kuwapo na mgogoro mkubwa kati ya familia ya Nyerere na watu ambao wanadai wameuziwa viwanja hivyo miaka kadhaa iliyopita. Viwanja hivyo ambavyo vipo katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam, kimoja kipo Mikocheni 'B' Plot 402 Block C na kingine kipo Msasani Beach Namba 778, ambacho kinadaiwa kugawanywa kwa watu wawili. Viwanja hivyo, vinadaiwa kuvamiwa na mfanyabiashara maarufu Dar es Salaam, Paul Mushi na mkwe wa Hayati Rashid Kawawa aitwaye Issa Majura Mshangama. Habari za uhakika kutoka ndani ya familia hiyo, zilizothibitishwa kwa MTANZANIA Jumatano na nyaraka mbalimbali, zinasema kutokana na hali hiyo, Mama Maria amelazimika kuiandikia Serikali barua akitaka msaada wa kurudishiwa viwanja vyake. Katika nyaraka hizo, zinaonyesha viwanja hivyo ni mali halali ya mtoto wa tatu wa Mwalimu, John Nyerere. Katika bar