HUMPHREY POLEPOLE ATOA MSIMAMO WAKEKUHUSU KATIBA MPYA
Aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambaye kwa sasa ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole ameweka wazi msimamo wake kuhusu mchakato wa katiba mpya, na kusema kuwa hajalitelekeza suala hilo. Humphrey Polepole akiwa Kikaangoni Polepole aliyekuwa kwenye kipindi cha Kikaangoni cha EATV kupitia facebook.com/eatv.tv, katika mahojiano yake na East Africa Radio amesema kuwa mchakato wa kuipata katiba mpya kwa Tanzania uko kwenye mikono salama chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, na kuwataka watanzania waiache serikali irekebishe kwanza baadhi ya mambo ili mchakato huo utakapoanza usikumbwe na vikwazo. Polepole amesema kwa uzoefu wake kama mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa chini ya Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba, anafahamu mambo ambayo watanzania waliyataka na kwamba mambo hayo ndiyo ambayo yameanza kutekelezwa na serikali ya awamu ya tano ikiwemo kuwa kujali utu, kud...