China Yaipatia Tanzania Msaada Wa Sh. Bilioni 29.4
Serikali ya China imeipatia Tanzania msaada wa Shilingi 29.4bilioni kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu, utalii wa kijiolojia na kuukarabati Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. Makubaliano ya msaada huo yametiwa saini Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James, kwa niaba ya Serikali, na Kaimu Balozi wa China hapa nchini, Gou Haodong. Katibu huyo amesema 22.4bilioni zitatumika kujenga Chuo cha Ufundi Stadi-VETA wilayani Ngara mkoani Kagera. “Fedha hizo zitatumika kujenga vyumba 19 vya madarasa, ujenzi wa karakana 9 za kutolea mafunzo ya elektroniki, ufundi bomba, useremala, ufundi uashi na upakaji rangi” amesema James Ameeleza kwamba kiasi hicho pia kitatumika kujenga majengo ya utawala, mabweni, nyumba za walimu na miundombinu mingine itakayosaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwenye chuo hicho. “Tunaamini kwamba msaada huo utakuwa sehemu ya kusaidia jitihada za Serikali za kuj...